Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa KESSY DEO? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri. Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii ya leo kwani kuamka salama ni ushindi mkubwa katika maisha yako hivyo tumia ushindi huo wa uhai kuacha alama siku hii ya leo kumbuka kuwa maisha ni muda.

Rafiki, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena siku hii ya leo katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Kwa namna ya pekee rafiki yangu, nakusihi sana tusafiri pamoja hadi mwisho wa somo letu la leo ambapo leo tutakwenda kujifunza jinsi unavyojimaliza nguvu wewe mwenywe hivyo basi, karibu tujifunze. PIA NAPENDA KUKUALIKA UJIUNGE NA KUNDI JIPYA LA WASAPU LA MIMI NI MSHINDI AMBALO LIMEWAKUTANISHA MARAFIKI NA WASOMAJI WA MTANDAO WA KESSY DEO KUJIUNGA TUWASILIANE KWA NAMBA 0717101505 KWA WASAPU AU TELEGRAM AU BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA KUNDI HILO.
Kuna vitu huwa vinawamaliza watu nguvu bila ya wao wenyewe kujua. Wako watu wanaokupa hamasa na kukuongezea nguvu kuthubutu lakini pia wako watu wanaokurudisha nyuma aidha kwa kukukatisha tamaa katika kile unachofanya.
Rafiki, kuna muda mwingine tunajimaliza nguvu sisi wenyewe kwa kukubali vitu fulani viweze kutawala maisha yetu. kuna mambo mengine watu wanaamua kuyaruhusu lakini yanawaumiza sana kiakili, kimwili na hata kiroho.
Watu wanajimaliza wao wenyewe kwa kutotaka kusamehe hivyo wanaendelea kubaki na uchungu ndani ya mioyo yao. Kutosamehe huwa inamaliza nguvu na kushindwa kufanya mambo yako mwingine. Unapokataa kusamehe unakuwa unamruhusu yule aliyekukosea akutawale na ukishamruhusu sasa ndiyo umejipa tiketi ya kujimaliza nguvu zako.
Nguvu unazozipoteza katika kumbeba mtu ni bora ungezielekeza katika uzalishaji ungekuwa mbali kwa sababu hakuna anayepata faida pale anapokataa kusamehe. Bila msamaha maisha yetu yanakuwa ni magumu kwa sababu kila siku wako watu ambao watakukwaza na ukiwa ni mtu wa kukasirika utakuwa unakasirika kila siku.
Ndugu msomaji, kadiri ya Yoshua binsira ‘’ uchungu wa rohoni hula nguvu na huzuni izidiyo huleta mauti’’. Kumbe basi, tunapokuwa na uchungu wa rohoni tunakuwa tumechagua sisi wenyewe uchungu huo ule nguvu zetu. Unapokosa kusamehe huwezi kuona huruma ya Mungu ndani yako kwani mwasisi wa msamaha ni Mungu mwenyewe.
SOMA; Hili Hapa Ndiyo Suluhisho La Watu Waliomizwa Na Kujeruhiwa Nafsi Katika Mahusiano Yetu
Hatua ya kuchukua leo, tafadhali samehe ili uweze kusamehewa. Ondoa uchungu wa rohoni kwa kuchukua hatua ya kusamehe leo na kama yuko mtu anayekumalizia nguvu kwa sababu ya kutosamehe basi msamehe ili hizo nguvu uziweke katika uzalishaji.
Rafiki, nakualika uweze kujifunza zaidi juu ya nguvu ya msamaha kupitia kitabu change cha kwanini msamaha ni muhimu sana kujifunza msamaha kwa sababu kila mtu anaalikwa kusamehe kila siku. Kitabu cha kwanini msamaha kinapatikana katika mfumo wa soft copy yaani nakala tete kwa shilingi elfu tano tu hivyo kukipata kitabu hiki tafadhali usisite kuwasiliana nami kwa mawasiliano yafuatayo 0717101505/0767101504.
Rafiki, kupata vitabu vya mafundisho mazuri yatakayokupa mwongozo mzuri wa kuishi maisha ya furaha na mafanikio makubwa tafadhali BONYEZA HAPA au wasiliana nasi kupitia namba hizi tuweze kukuhudumia 0717101505/0767101505. Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email tafadhali jiunge na kwa kujaza fomu hapo chini ya makala. karibu sana na asante sana.
Nikutakie kila la heri rafiki yangu na fanyia kazi haya uliyojifunza leo.
Ni mimi rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504 au deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana