Habari Mpendwa Rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini uko vizuri na unaendelea vema na shughuli zako za kila siku. Kama hauko vizuri rafiki pole nakuombea upate nafuu ya haraka na urudi katika hali yako ya kawaida. Kuna msemo unasema hivi rafiki, kama umeamka na huna malengo ya siku basi rudi kitandani ukalale. Ndio kama huna malengo uliyojiwekea ni vema tu ukarudi kulala.

Mpendwa msomaji, karibu tena katika makala yetu ya leo ambapo leo tutajifunza jambo muhimu la kuzingatia pale unapotaka kutoa hukumu juu ya jambo Fulani. Je unajua ni kitu gani rafiki unapaswa kuzingatia? Nakualika ungana nami tuweze kujifunza kwa pamoja mwanzo mpaka mwisho wa somo letu la leo.
Kuhukumu imekuwa ni desturi ya watu wengi katika jamii ya leo. Watu wanahukumu kama vile wamestahilishwa kuhukumu. Pale mtu anapokuwa amekosea juu ya jambo Fulani basi watu wanakuwa wanaanza kuhukumu utafikiri wamealikwa kuhukumu. Unapokuwa unamhukumu mwenzako na kumuona yeye ndiye anayestahili kukosea zaidi kuliko wewe unakua unakosea sana. unapomnyooshea mwenzako kidole angalia vidole vitatu vinaenda kwa nani? Nafikiri mpaka hapo utakua umepata jibu.
SOMA HAPA; Hizi Ndio Faida Kumi (10) Za Msamaha Katika Maisha Yako
Kulikuwa na watu wawili walipanda hekaluni kusali moja ya watu hao wawili mmoja alikuwa ni mfarisayo na wa pili alikuwa ni mtoza ushuru. Yule farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake Ee Mungu nakushukuru kwa kuwa mimi si kama wengine, wanayang’anyi,wadhalimu,wazinzi,wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma , hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini Yule mtoza ushuru alisimama mbali wala hata hakuthubutu kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga piga kifuani akisema, Ee Mungu uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
SOMA TENA; Fanya Tathimini Hii Muhimu Sana Kabla Hujaenda Kulala Leo
Kwahiyo, tumeona hapo juu kwa mfano ni jinsi gani watu wamekuwa wakihukumu mwenzao hata katika mambo ya imani na kujiona kuwa wao ndio wanastahili zaidi na kuanza kuyaona makosa ya mwenzake kuliko ya kwake. Watu wanahukumiana katika maswala ya kiimani na kuona kuwa imani yake yeye ni bora kuliko ya wengine na kuwadharau wengine juu ya imani yake. Ukianza tabia ya kuhukumu wengine na kuona makosa yao zaidi unakua unakosa upendo kama unamuona mwenzako yuko katika hatari kwanini usimsaidie badala ya kumhukumu?
Rafiki, malengo yetu mahususi nikutaka kujua ni jambo gani muhimu la kuzingatia kabla ya kutoa hukumu pale unapokuwa unasuluhishwa jambo. Kabla ya kutoa hukumu jambo la kwanza ni kuchunguza kiini cha kosa. Usianze kuhukumu tu au kuongea kama kasuku bali chunguza kwanza kiini cha kosa. Kama unataka kusuluhisha kesi Fulani ni vema kupata kiini cha kosa kwa kuchunguza taarifa na maelezo kutoka pande zote mbili kati ya mkosa na mkosewa. Usihukumu kama hujui kiini cha tatizo au kosa ni nini, pata taarifa za kujitosheleza kwanza ndio utoe hukumu. Ukimwona mwenzako anafanya mambo tofauti kabla hujamhukumu chunguza kwanza kiini cha kosa na wala usiwe mwepesi wa kutoa hukumu kabla ya kujirizisha na maalezo ya kutosha unapochunguza kiini cha kosa Fulani. Hivyo basi, ni muhimu sana kabla hujafanya suluhisho la kesi au unataka kupatanisha watu chunguza kiini cha kosa kwa kupata maelezo ya pande zote mbili.
SOMA MUHIMU; Haya Ndio Makosa Kumi Na Moja (11) Wanayofanya Wazazi Au Walezi Katika Malezi Ya Watoto
Mwisho, somo letu la leo lilitualika kuwa kabla ya kutoa hukumu ya jambo Fulani kitu cha kwanza chunguza kiini cha kosa au tatizo. Pili, somo lilitualika sisi sote tusiwe kama mafarisayo katika kuwahukumu mwenzetu na kujiona sisi tunashili zaidi au sisi ni bora kuliko wengine. Usiishi maisha ya kuhumu bali ishi maisha ya falsafa ya upendo. Hatua ya kuchukua leo, kabla hujalala jichunguze ni watu wangapi umewahukumu bila kuchunguza kiini cha kosa kwanini wako vile kama ulivyowaona,pili umetumiaje falsfa ya ufagio katika siku hiyo ambayo falsafa ya ufagio ni unyenyekevu katika kutoa huduma kulingana na kile unachofanya?
Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.
Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com