Mambo tuliyonayo tayari ni mengi. Muda wa kufanya vitu hivyo nao ni mchache.
Tunao muda wa kufanya vitu ambavyo ni muhimu tu.
Lakini, usijipe msongo na mambo haya.
Usijipe msongo kwa mambo ambayo yako nje ya uwezo wako.
Usijipe msongo kwamba wewe ni kiranja wa dunia. Kwamba unataka watu waishi kama vile unavyotaka wewe.
Usije msongo na yale yanayoendelea katika maisha ya watu. Maisha yako yenyewe bado hujayakamilisha.
Wewe ni mradi ambao bado hata haujakamilika. Ya nini kuhangaika na miradi ya wengine wakati wa kwako hujaumaliza?
Jiimarishe kwanza na kuwa vizuri wewe.
Ukiwa vizuri utaweza kuwasaidia wengine.
Usitegemee kwenye maisha yako kwamba, ipo siku utakuja kumaliza matatizo haya maisha yako.
Huwezi kuyamaliza matatizo yako na ya wengine mpaka unaondoka hapa duniani.
Usijipe msongo kwa vitu ambavyo huwezi kuvidhibiti moja kwa moja.
Mwisho, jipe msongo na maisha yako kwa sababu ndiyo mradi pekee unaotakiwa kuukamilisha.
Kabla hujahangaika na miradi ya wengine, jiulize vipi kuhusu mradi wako?
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog