Kwenye kila eneo la maisha yetu, tumekuwa na watu ambao wamekuwa wanafanya vizuri sana kwenye eneo fulani.
Ukija kwenye upande wa sanaa ya uchoraji alikuwepo Leonard Da Vinci na alichora picha nyingi na moja wapo ni ile ambayo Yesu alikuwa anapata chakula cha mwisho na wanafunzi wake.
Ukija kwenye michezo kama vile mpira wa miguu, alikuwepo watu kama kina Pele. Walifanya makubwa sana kwenye eneo hilo na leo watu wa michezo wanamkumbuka.
Ukija kwenye uimbaji wa muziki alikuwepo mtu kama vile Michael Jackson. Na dunia inamjua vizuri kwa jinsi alivyokuwa anaimba kwa sauti nzuri na kucheza vizuri.
Kumbe basi, kwenye kila eneo la maisha yetu, wako watu wengi sana ambao wanafanya kile tunachofanya kwenye maisha yetu.
Lakini ni wangapi mpaka sasa wanakumbukwa kwa yale waliyofanya? Kama hutafanya makubwa, miaka 100 ijayo hutakuja kukumbukwa kama vile unavyowakumbuka watu waliofanya makubwa hapo awali.
Ili uweze kukumbukwa na vizazi vijavyo, unapaswa kutoa kazi bora ambayo itadumu vizazi vyote. Unapaswa kufanya kitu ambacho kitadumu kwa muda mrefu. La sivyo, miaka 100 ijayo hakuna atakayejua kama hata uwepo wako hapa duniani ulikuwepo.
Watu wanakuja, na watu wanaondoka. Ndivyo asili ya maisha ilivyo. Pata picha tokea kuanzishwa hii dunia walikuwepo watu wa ngapi ? Ni wangapi ambao unawakumbuka mpaka sasa? Ni wa chache, na hawa chache ni kwa sababu walifanya kitu kikubwa kwa ajili ya watu.
Kwa mfano, Yesu Kristu, Mohammad, Socrates, Seneca wanakumbukwa mpaka leo kwa sababu walijitoa kwa ajili ya jamii.
Ukitaka jamii ikukumbuke, fanya kitu kwa ajili ya wengine na siyo kwa ajili yako tu.
Ubinafsi ni shetani wa karne ya ishirini na moja, mtu ambaye ni mbinafsi hawezi kufika mbali. Mtu ambaye ndoto yake ni kuwa na nyumba, gari na kusaidia familia yake tu hawezi kufika mbali.
Angalia watu waliofanya makubwa wote hawakuwa wabinafsi bali walifanya makubwa kwa ajili ya dunia nzima.
Hatua ya kuchukua leo; Fanya kitu bora kwa ajili ya wengine na dunia itakukumbuka.
Toa kwa ajili ya wengine, kama una kitu na unajua kitakua na msaada kwa wengine toa wala usiwe na wasiwasi.
Wasaidie wengine kupata kile wanachotaka na wewe utapata kile unachotaka kwenye maisha yako.
Jiulize walioishi miaka 100 iliyopita wako wapi na wewe 100 ijayo utakumbukwa na nini?
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog