Watu wengi waliovurugwa na maisha huwa wanataka kile ambacho kimewavuruga wao, na wengine pia kiwavuruge.
Watu wanakuwa na matatizo yao binafsi, hivyo wanatamani na wengine pia wawe kama wao.
Usikubali kununua matatizo ya mtu, na njia nzuri ya kutokununua matatizo ya mtu ni kutokuwa kama wao. Kifupi, tulia, pale ambapo wanakuongelesha kwa jazba, wewe tulia waangalie tu bila kuwajibu.
Unanunua matatizo ya watu pale unapokubali matatizo yao yakuvuruge. Chochote kile ambacho watu wanakuambia usikubali kutaharuki. Unapotaharuki, unakuwa unawaruhusu wao kukutumia na kuwa kama wao.
Usikubali kuwa kama wao, tulia na waangalie tu, usiwajibu na ukijaribu kuwajibu ni kama vile umewaruhusu wewe kuwa kama wao.
Hekima inatakiwa sana kwenye maisha yako, kuishi na wale ambao bado uelewa wao ni mdogo. Wachukulie watu wote ambao wanasumbuliwa na matatizo yao binafsi kama vile ni watu ambao wanahitaji msaada na msaada mkubwa wa kuwapa ni kutokuwa kama wao.
Hatua ya kuchukua leo; njia nzuri ya kumwadhibu mtu ambaye amevurugwa na matatizo yake binafsi ni kutokuwa kama yeye, kwa kutokumjibu na kumpuuza.
Kuwa mtu wa kupuuza, na usikubali kununua matatizo ya watu, waangalie tu bila kuwajibu watajiona ni wajinga. Kuwajibu ni kununua matatizo ya watu, na matatizo uliyonayo tayari yanakutosha.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog