Mpendwa rafiki yangu,
Bila kuwa na utulivu wa akili hatuwezi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Akili zetu zinapokuwa zinataharuki basi huwa tunafanya uzalisha mbovu na hata maamuzi yanakuwa siyo mazuri sana ukilinganisha na akili inapokuwa na utulivu wa kutosha.
Kuna mambo mengi ya kila siku ambayo yanavuruga kabisa utulivu wa akili zetu hivyo yanapelekea kuwa na msongo wa mawazo. Tusitegemee mambo mazuri kama akili zetu hazina utulivu.
Kuna mambo ya nje huwa tunayaruhusu yatukamate ufahamu wetu, yaani kama yakienda vizuri basi tuna kuwa na furaha na yasipoenda vizuri tunakosa raha kabisa na hata akili zetu zinakuwa hazina utulivu.
Usikubali mambo ya nje ya kuharibie utulivu wako kwa mfano, mtu anakuwa labda ni shabiki wa timu fulani inapotokea timu yake imefungwa basi na yeye anakuwa hana raha kabisa, kama ni kufanya kazi anashindwa kabisa kisa timu yake imefungwa. Usikubali vitu kama hivi vikutawale, kuwa shabiki lakini usiruhusu utawaliwe na ule ushabiki.
Usikubali furaha yako ibebwe na vitu hivyo pale mambo yanapoenda ndivyo sivyo wewe ubaki kawaida tu, yaani ukifungwa sawa usipofungwa sawa. Ni utumwa wa ajabu sana, wengine wanabishana na hata kupigana kwa sababu ya mambo ambayo hayawasaidii wala kuwaingizia shilingi mfukoni. Huenda hata timu anayoshabikia hana hata hisa moja kule na hakuna mtu anayemfahamu lakini anajiweka katika uteja wa kijinga.
SOMA; Usikubali Kutawaliwa Na Kitu Hiki Kwa Sababu Kipo Ndani Ya Uwezo Wako
Kuna muda mfupi sana, usijiingize kwenye kila kitu ambacho hakikusaidii katika kufanikisha malengo yako. Jinsi unavyokosa raha pale timu unayoshabikia inapofungwa hebu iweke kwenye mafanikio ukikosa kutimiza malengo ukose raha uhisi uchungu lakini siyo kwenye mambo ambayo hayana maana kwako.
Hatua ya kuchukua leo; kamwe usikubali mambo ya nje ya kutawale. Tawala akili yako na usikubali kitu chochote kiwe kikwazo cha kukufanya utawaliwe. Chunga sana akili yako kwani ndiyo inabeba mwili wako vizuri.
Mwisho kabisa, kama kuna kitu ambacho hakina faida na kinakuumiza kichwa tafadhali kiondoe, usijitese kwa vitu ambavyo havina mchango chanya kwako. Usilalamike wala kumuelezea kila mtu shida zako wajibika na maisha yako.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana