Jinsi Ya Kutokubali Kujiingiza Katika Mikopo

Watu wengi wanadaiwa tena madeni mbalimbali tu. Leo hii watu wanadaiwa hata na mitandao ya simu kama vile voda, tigo nk katika simu zao. Kupitia tu mikopo ya kukopa salio kupitia mitandao ya simu ninaona ni jinsi gani watu wanavyopata shida na mikopo hiyo. Hakuna mkopo ambao haukupi fedhea, asili ya mikopo ni adhabu na utumwa.

Utawakuta watu wanadaiwa katika simu zao hivyo wanahangaika kuwatafuta watu ambao hawadaiwi ili wasaidie kuunganishwa juu kwa juu. Anajua kuwa kama akiweka kawaida atakatwa na alikuwa hana mpango wa kulipa kwa muda ule. Mkopo ni utumwa unawafanya watu wengi kuishi kwa wasiwasi na kukosa uhuru. Ni rahisi sana kukopa lakini ni ngumu kulipa na waswahili wanasema, kukopa harusi na kulipa matanga.

Nini suluhisho la kutokubali kujiingiza katika mikopo? Suluhisho ni kuweka akiba na kuiandaa akili yako kutokopa. Watu wengi wanasaikolojia fulani katika fedha, wanajua hata wakiishiwa wao watakopa na ndiyo imekuwa kama kimbilio lao. Jingee nidhamu kama huna sehemu ya kukopa na ipe akili yako kazi ni kwa namna gani inaweza kukusaidia kupata fedha kwa njia nyingine na siyo kukopa.

SOMA; Kitu Muhimu Cha Kuzingatia Kabla Hujachukua Mkopo

Kama unataka kukopa jiulize je hicho kitu ni muhimu sana mpaka unakopa? Je usipokuwa nacho utakufa? Kama kinaweza kuvumilia bila kukopa basi subiri. Wengine wanakopa kimazoea tu, yaani mtu akiwa hana fedha tu anakopa ili awe na fedha. Kukopa hovyo ni njia ya kukurudisha katika umasikini na siyo kukutoa katika umasikini. Unakuwa uko katika duara la matatizo unakopa kulipa deni hivyo hakuna kupunguza matatizo bali ni kuongeza matatizo mengi tu.

SOMA; Jinsi Yakujiondoa Katika Madeni

Hebu ishi kama vile hakuna mkopo ungefanyaje?

Hatua ya kuchukua leo, weka akiba. Ukiwa na akiba na ukipatwa na dharura hutakimbilia kukopa bali utaingia katika akiba yako na kuchukua itakusaidia. Lakini kama huna akiba lazima utakimbilia kukopa.

Hivyo basi, fanya kazi, toa thamani, weka akiba na kuwa kitajiri. Punguza matumizi na ongeza kipato na utakuwa na uhuru wa kifedha kama siyo kupumua kidogo kwa kero za kukopa kopa. Na usikope mikopo ambayo haizalishi.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started