Kitu Ambacho Hakitokusaidia Kubadilisha Maisha Yako

Mpendwa rafiki yangu,

Tuna muda mfupi sana hapana duniani wa kufanya yale muhimu lakini siyo kufanya kila kitu kinachojitokeza katika maisha yako. unapoianza siku yako unatakiwa kuwa na ratiba ya ushindi ambayo umeandika mambo unayopaswa kuyafanya ndani ya siku husika. Hivyo, yakijitokeza mambo ambayo hayapo katika ratiba yako wala hata usihangaike nayo ni usumbufu tu kwako.

Kitu chochote ambacho hakina faida kwako na hakikusaidii kutimiza ndoto yako ni usumbufu kwako. Watu wengi wanaogopa kuishi maisha yao kwa sababu yale watashindwa kuwafurahisha watu na mambo mengi ya kijinga ndiyo unakuta yanafanywa na wengi hivyo mtu anaona mambo ya wengi sahihi kumbe siyo sawa.

Kitu ambacho hakitukusaidia kubadilisha maisha yako ni kufuatilia mambo ambayo hayahusiani na kile ambacho unataka. Ili ufanikiwe jua kwanza unataka nini halafu kuwa tayari kulipia gharama. Huwezi kubadilisha maisha yako kwa kufuatilia wasanii fulani, leo wamefanya nini, kuzurura kwenye mitandao ya kijamii kutafuta habari ambazo hazichangii hata kidogo kubadilisha maisha yako.

Tafadhali rafiki, jitoe kwenye vitu muhimu ambavyo vinachangia kubadilisha maisha yako, dunia ina kelele nyingi hivyo usipokuwa makini huwezi kufanikiwa. Kuwa mbabe wa malengo yako ndiyo utafanikiwa acha kupoteza muda kwenye mambo ambayo hayakuiingizii hata senti ndani ya siku moja lakini cha ajabu unayoyahangaikia ndiyo yanakumalizia muda wako na fedha pia.

SOMA; Vitu Viwili Vya Kuwa Navyo Katika Safari Ya Mafanikio

Nguvu unazoweka katika mambo ambayo hayakusaidii hebu zielekeze katika mambo yanayokusaidia. Najua kuna mambo ambayo hayana maana kwako hebu yaache kwani hujafunga nayo ndoa na wala hujazaliwa nayo. Kitu pekee ambacho unaweza kusema huwezi kuishi bila hicho ni pumzi tu lakini haya mengine yote yanawezekana kwa sababu yako ndani ya uwezo wako.

Hatua ya kuchukua leo; amka na badilika, chukua hatua chanya zitakazokukusaidia kutoka hapo ulipo na kwenda mbele kimaendeleo, pambana kuwa bora na siyo kupambana kurudi nyuma.

Kila kitu kina kazi, hata kuwa masikini ni kazi na kuwa tajiri ni kazi pia. Kupata alama A kwa mwanafunzi ni kazi na hata kupata alama F ni kazi pia. Chagua unataka nini na weka juhudi.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started