Kuanzia Leo Acha Kuimba Wimbo Huu

Mpendwa rafiki yangu,

Unafikiri ni wimbo gani huo rafiki nao kuambia acha kuimba? Natumaini kuna wimbo unaopenda kuimba na kama siyo kuimba basi hata kusikiliza kwa sababu dunia yetu ni dunia ya kifasihi hivyo kwa namna yoyote ile hatuwezi kukwepa fasihi kwani fasihi ndiyo maisha yetu ya kila siku yanayoelezea uhalisia wake.

Ziko nyimbo nyingi sana ambazo watu wanapenda kuziimba na kuzisikiliza lakini kuna wimbo ambao unapendwa sana kusikilizwa na na kuimbwa na jamii yetu kwa wingi. Watu wamekuwa wanaupenda na huenda umekuwa ni kama wimbo bora ambao hautoki katika maisha yao.

Je huo ni wimbo gani? Rafiki, ukisikiliza jamii na wengine walioshindwa huwezi kuacha kuwasikia wakilalamika au kuimba wimbo huo. Wimbo ambao nakusihi sana wewe rafiki yangu usiuimbe ni wimbo wa hali ngumu na sina pesa. Watu wamekuwa mahodari sana wa kusema hali ngumu ukilinganisha na juhudi wanazoweka kupambana na hali ngumu. Huwezi kupambana na hali ngumu ya kifedha kama huchukui hatua chanya za kuongeza thamani ili upate fedha zaidi.

Kuna watu wanalalamika kiwa awamu hii fedha ni ngumu sana lakini mimi ninakataa kwa sababu mbona ukiangalia maisha ya watu yanaendelea kama kawaida? Kama unatoa thamani huwezi kusema au kuimba wimbo wa hali ngumu.

Rafiki, eti utamsikia mtu anakuambia awamu hii ni ngumu je kama awamu hii ni ngumu je awamu zilizopita umefanya nini? Kulikuwa na awamu ya Nyerere, ikaja ya Mwinyi,Achaea Mkapa, Kikwete na kwa sasa Magufuli lakini utamkuta mtu analalamikia awamu hii ni ngumu, mambo hayaendi je kama awamu hii ni ngumu je hizo zingine ulifanya nini? Acha kuimba wimbo huu hali ngumu bali ingia mzima mzima kutoa thamani na utapata pesa. Acha visingizio vya kusema awamu hii mambo ni magumu na futa kabisa aina hiyo ya wimbo na sikiliza wimbo ambao unakuambia hakuna hali ngumu na kuwa fedha ziko nyingi sana kama uko tayari kutatua matatizo ya watu basi utafanikiwa sana na utaona kile unachoongea na hakina uhalisia.

Nina uhakika wanaosema hali ni ngumu ndiyo wale ambao hawachukui hatua yoyote katika maisha yao. Hali itaendelea kuwa ngumu mpaka unaingia kaburini kama hujachukua hatua sahihi.

Fedha ziko nyingi na ili uzipate unatakiwa kutoa thamani na fedha ni mbadilishano wa thamani na kama huna fedha jua kabisa huna thamani unayoitoa. Kadiri unavyopata fedha zaidi ndivyo na kiwango chako cha kutoa thamani bora kinaongezeka.

Hatua ya kuchukua leo, toa thamani na utaona hakuna hali ngumu, huwezi kuondoa hali ngumu kwa kuweka mikono mifukoni bali kwa kuchukua.

Kwahiyo mpendwa rafiki yangu, unalipwa kadiri ya thamani unayoitoa sokoni. Je unatoa thamani gani ili uweze kulipwa zaidi?

Ukawe na siku bora sana Rafiki yangu. Nenda kafanye kazi na futa wimbo wa hali ngumu katika maisha yako.

Rafiki, kama bado hujajiunga na mimi ni mshindi basi unajidhulumu kupata kupata maarifa mazuri sana ambayo huyapati hapa, hivyo nakusihi jiunge leo ushangae na unufaike.

Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
http://www.mtaalamu.net/kessydeo
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started