Jinsi Wazazi Wanavyochangia Kuwalaani Na Kuwaharibu Watoto Wao

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa KESSY DEO? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri. Hongera sana rafiki kwa zawadi nzuri ya siku hii ya leo kwani kuamka salama ni ushindi mkubwa katika maisha yako hivyo tumia ushindi huo wa uhai kuacha alama siku hii ya leo kumbuka kuwa maisha ni muda. Kumbuka kuiendea siku hii ya leo kwa kauli mbiu yetu ya wakati sahihi ni sasa, usisubiri kupewa ruhusa.

Rafiki, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena siku hii ya leo katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Kwa namna ya pekee rafiki yangu, nakusihi sana tusafiri pamoja hadi mwisho wa somo letu la leo ambapo leo tutakwenda kujifunza jinsi wazazi wanavyochangia kuwalaani na kuwaharibu watoto.

Wazazi ndiyo makuhani wakuu katika malezi ya watoto, wao ndiyo wamepewa mamlaka makubwa juu ya watoto wao katika maisha ya kimwili, kiroho na kiakili. Wazazi wanatakiwa kuwapa watoto mwongozo bora lakini pia misingi au falsafa ambayo itakuwa msaada mkubwa katika maisha yao ya baadaye.

Huwa tunatafuta mchawi ni nani pale watoto wanapokuwa wameharibika, lakini kama tukichunguza kwa  makini wazazi wenyewe ndiyo wanachangia kwa kiasi kikubwa sana katika kuwalaani au kuwaharibu watoto wao. Jinsi wazazi wanavyowapa watoto wao malezi aidha ni mazuri au mabaya hayo ndiyo yanachangia kuwajenga watoto bora au kuwaharibu.

SOMA; Kosa Moja Kubwa Wanalofanya Wazazi Na Walezi Katika Malezi Ya Watoto Wao

Malezi ya watoto ni kazi kama kazi nyingine na hii ni kazi ngumu sana kwa sababu pale mzazi anapofanikiwa kupata mtoto hakuna kitabu au mtaala anaopewa  mzazi wa kumwongoza katika malezi ya watoto ukilinganisha na vitu vingine. Shuleni kuna mwongozo kuanzia darasa la awali mpaka elimu ya juu. Hivyo mzazi anamlea mtoto kadiri anavyoona yeye inafaa kulingana na malezi aliyopata kutoka kwa wazazi wake, na hapo ndipo pagumu kwa sababu kama mtoto alifundishwa malezi ambayo siyo sahihi naye anakuja kurithisha kizazi chake.

Wazazi wanakuwa wanapandikiza miiko isiyofaa kabisa kwa watoto wao na utamaduni ambao muda mwingine hauna nafasi tena katika dunia ya leo. Wazazi wamekuwa watumwa wakufanya mambo ambayo hata wao wenyewe ukiwauliza hawajui kwanini wanafanya hivyo, kwa kuwa jamii ameikuta iko hivyo naye anapokea vivyo hivyo.

Mpendwa msomaji, sasa namna gani mzazi anachangia kumlaani na kumharibu mtoto? Wazazi wanachangia kuwalaani na kuwaharibu watoto wao kwa kutumia kinywa chao, hakuna laana mbaya kama ya kumnenea mtoto kitu hasi juu yake hapo unakuwa umempa tiketi ya kuwa mshindwa katika maisha yake yote. Wazazi wanaalikwa kutumia vinywa vyao kubariki na siyo kulaani kwa mfano, mzazi badala ya kumwambia mtoto wako mjinga mwambie una akili sana. mjaze maneno chanya ambayo hatokuja kuambiwa na mtu yeyote yule.

SOMA; Jifunze Mambo Muhimu Ya Malezi Kwa Watoto Katika Kitabu Cha Selfish Reasons To Have More Kids

Kama mzazi unamwambia mtoto wako wewe ni mbwa halafu sikupendi sijui hata nimekuokota wapi, maneno kama hayo ni sumu kubwa kwa mtoto kwani unakuwa unaua uwezo wake wa akili lakini pia wa kujiamini na kusabisha kuwa na magonjwa mbalimbali ya akili. Mbariki mtoto kwa kutumia kinywa chako na siyo kutumia kinywa chako kulaani.

Hatua ya kuchukua leo, tumia kinywa chako kubariki familia yako, watoto wako, ndugu na watu wnegine. Usitumie kinywa chako kusema maneno hasi juu ya mtoto wako au mtu yeyote yule, laana mbaya ni ile ya kumnenea mtoto wako vitu vibaya kwa mdomo wako mwenyewe. Chunga sana kinywa chako kwani kinywa huwa kinaumba.

Mwisho, nawaalikwa wazazi na walezi wote kujifunza juu ya malezi ya watoto, kujifunza hakuna mwisho na tusiwalee watoto wetu kwa mazoea. Fanya yale chanya juu ya mtoto wako, mlee kiasi kwamba mtoto ajihisi ni mwenye bahati sana, mlee kwa upendo wa hali ya juu kwani upendo ni dawa ya kila kitu maisha ya binadamu.

Rafiki, kupata vitabu vya mafundisho mazuri yatakayokupa mwongozo mzuri wa kuishi maisha ya furaha na mafanikio makubwa tafadhali BONYEZA HAPA au wasiliana nasi kupitia namba hizi tuweze kukuhudumia 0717101505/0767101505. Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email tafadhali jiunge na kwa kujaza fomu hapo chini ya makala. karibu sana na asante sana.

Nikutakie kila la heri rafiki yangu na fanyia kazi haya uliyojifunza leo.

Ni mimi rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started