Design a site like this with WordPress.com
Get started

Huwa Unapendelea Kuwekeza Eneo Gani Zaidi Kati Ya Haya?

Maisha ya binadamu yana utatu. Utatu huo ni mwili, akili na roho. Na kufanikiwa kwenye maisha ni lazima ufanikiwe kwenye maeneo hayo yote matatu, kimwili, kiroho na kiakili. Watu wengi huwa wanapendelea kuwekeza kwenye eneo moja zaidi ambalo ni eneo la mwili. Je, wewe mwenyewe unapendelea kuwekeza eneo gani zaidi? Maisha yako yanapaswa kuwa na …

Hii Ndiyo Hofu Unayoweza Kuikwepa

Zeno mwanafalsafa wa kistoa aliwahi kunukuliwa akisema, siwezi kukwepa kifo bali; ninaweza kukwepa hofu ya kifo. Usipoteze muda wako kama utaweza kukwepa kifo. Hutaweza ila utaweza kukwepa hofu ya kifo. Hofu ya kifo inaua wengi kuliko hata kifo chenyewe. Wewe ishi maisha yako na kifo kitakukuta kwa namna kitakavyokukuta. Usiache kufanya mambo makubwa kwa kuhofia …

Je, Unataka Nikufanyie Nini?

Ukiwa unatoka nyumbani na kwenda stendi kwa ajili ya kusafiri ukifika stendi wale wakata tiketi watakuuliza unaenda wapi? Ukiwajibu hujui unakokwenda hawatakua na habari na wewe bali watakuacha na kutafuta mtu anayejua kule anakokwenda. Katika maisha yetu ya kiimani, ya kawaida kama usiposema unataka nini huwezi kusaidiwa. Kwa mfano, simulizi kutoka kwenye kitabu cha Biblia …

Hiki Ndiyo Kiunganishi Muhimu Cha Kukuwezesha Kupata Kile Unachotaka

Sisi binadamu ni viumbe vya hisia. Na karibu kila mmoja wetu ana husiana na wengine. Kitu kimoja kinachotuwezesha sisi kupata kile tunachotaka kutoka kwa wengine ni mawasiliano mazuri. Hakuna kitu ambacho unaweza kukipata bila kuwa na mawasiliano na wengine. Mawasiliano ndiyo kiunganishi muhimu kinachotuwezesha sisi kupata kile tunachotaka. Chochote unachotaka kutoka kwa wengine utakipata kwa …

Watu Huwa Wanapenda Kujihusisha Na Watu Hawa

Iko wazi kuwa watu huwa wanapenda kujihusisha na watu wanaowajua. Ni ngumu sana watu kujihusisha na watu wasiowajua. Wewe hushangai ule usemi unaosema haijalishi unajua nini bali unamjua nani. Huu msemo huwa unasema kweli. Kama unataka kufanikiwa hakikisha unakuwa na watu. Kwani utajiri wako ni wastani wa watu unaojihusisha nao. Mafanikio unayotafuta yako tayari kwa …

Huu Ndiyo Msamiati Usiofaa Kujiambia

Kwenye maisha yako, kamwe usijiambie umeshindwa. Futa kabisa msamiati wa kujiambia umeshindwa kwenye fikra zako. Akili yako inatakiwa iamini kwenye uwezekano tu. Kama dunia ina utele kwa nini weweujiaminishe kwenye uhaba? Unajipunja vitu vingi pale akili yako inapofikiria kwenye kushindwa. Anayejiwazia kushindwa ni amekubali kwa makusudi kuwa na fikra za kimasikini. Hata kama huna fedha …

Haya Ndiyo Malengo Makubwa Mawili Ya Visingizio

Mara nyingi mtafuta sababu huwa haishiwi sababu. Watu wengi wanaokuwa na visingizio huwa wana malengo yao pia. Hivyo leo kupitia makala yetu ya leo tunakwenda kujifunza malengo makubwa mawili ya watu wenye visingizio. Moja ni kujitetea baada ya kushindwa. Mtu anapokuwa ameshindwa anatafuta sababu nyingi ili kuhalalisha kushindwa kwake.Kwa mfano, kamuulize mwanafunzi yeyote aliyepata daraja …

Je, Ni Mapenzi Ya Mungu Kweli Kufanya Hivi?

Ni swali ambalo kila mtu anapaswa kujiuliza pale anapotaka kuomba au kufanya kitu fulani. Ukiomba chochote kile, jiulize, je haya ni mapenzi ya Mungu kweli? Jibu likiwa siyo acha. Hata kikiwa ni kizuri namna gani. Kwa sababu tunajikuta tunaingia kwenye mitego na kufanya vitu ambavyo si mapenzi ya Mungu bali mapenzi ya binadamu. Tunajua kabisa …

Ubongo Wetu Hauridhiki Mpaka Upate Kitu Hiki

Binadamu ni watu wa kuhusishanisha vitu. Kitu chochote kikitokea lazima binadamu watahusishanisha matukio. Kwa mfano, ajali ikitokea watu walikuwa sita na wakafariki watu wa 5 na kupona mmoja lazima huyo mmoja ataandamwa na watu kwamba yeye ndiyo aliwatoa kafara watu wenzake. Tukiachana na hilo, katika sehemu yoyote ambayo watu wanatoa fedha zao na wakitegemea kupata …

Haya Ndiyo Mambo Matatu Ambayo Hupaswi Kuwaambia Watu Wa Nje

Mpendwa rafiki yangu, Siyo kila kitu unapaswa kumwambia mtu, siyo lazima kila mtu ajue undani wa maisha yako. Pale watu wanapokuwa wanakuja undani wako ni rahisi kufanya kile wanachotaka kadiri ya taarifa ulizo nazo. Mambo matatu ambayo ni siri yako tu na hupaswi kuwaambia watu ni kama yafuatavyo; Kipato chako; usiwaambie watu juu ya kipato …