Design a site like this with WordPress.com
Get started

Watu Huwa Wanaona Na Kusikia Hiki Hapa

Unapotaka kuongea na watu hakikisha watu unaotaka kuongea nao wanataka kusikia nini, usipofanya hivyo utakua unajisumbua bure. Kama ulikuwa hujui tabia ya watu iko hivi, kwa kawaida, sisi binadamu huwa tunaona kile tunachotaka kuona. Ndiyo maana unaweza kwenda kwenye maonesho ya vitu au ununuzi wa vitu fulani wewe ukaona kile unachotaka. Watu wana ubinafsi wa …

Mtihani Mkubwa Tuliopewa Binadamu

Tumepewa amri tuweze kuziishi ili maisha yetu yaweze kuwa bora na tusiende kinyume na asili. Ni rahisi sana kuwa na kanuni au amri kwenye maisha yetu lakini kuishi amri hizo ni kazi sana. Amri ambayo binadamu imemshinda mpaka sasa ni mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe. Hapa ni mtihani mkubwa kwa watu wengi. Kama watu …

Usikubali Majuto Haya Yakupate Kwenye Maisha Yako

Majuto au maumivu kwenye maisha huwa hayakosekani , kuna mambo mengi huwa yanakwenda kinyume na matarajio yetu. Kuna aina mbili za majuto. Majuto ya kufanya na majuto ya kutokufanya. Hakuna majuto mabaya kama yale ya kutokufanya. Majuto ya kutokufanya kitu ambacho kipo ndani ya uwezo halafu kinakuja kukutesa maisha yako yote. Ni bora ufanye kwa …

Una Mchango Gani Katika Gurudumu La Maisha?

Dunia isingekuwa hivi ilivyo leo kama watu wasingekuwa wanachangia katika gurudumu la maisha. Je, kwa dunia kuwa hivi ilivyo leo wewe umechangiaje kwenye gurudumu la maisha? Kila mtu lazima afanye kitu au kazi ili maisha yaweze kwenda,ili gurudumu la maisha liweze kwenda. Kwa mfano, wako ambao kazi yao ni kulima hivyo wanachangia chakula kwenye gurudumu …

Jinsi Ya Kuwahamasisha Watu Kujituma Zaidi

Kiasili sisi binadamu ni watu wa kupenda mashindano. Huwa tunapomuona mwenzetu ana kitu fulani na sisi tunahakikisha tunapambana ili tuweze kukipata. Watu wanapenda mashindano kwa sababu hakuna anayetaka kuonekana ni mzembe. Kwa mfano, ulikuwa unakimbia mbio zako mwenyewe katika mazoezi mara anapokuja mtu mwingine akakupita kiasili utashangaa na wewe unaongeza mwendo ili uweze kumfikia na …

Njia Rahisi Ya Kukubaliana Na Watu Katika Majadiliano

Ukitaka mtu akubaliane na wewe kirahisi katika mazungumzo yoyote yale, tafuta kitu ambacho mtu huyo utaanza kumuuliza na akasema ndiyo. Mtu akishasema ndiyo kama mara tatu na ukimwambia kile unachotaka kumwambia anakuwa rahisi kukubaliana na wewe. Kwa mfano, wako watu ambao walitaka kwenda kuweka alama za mabango makubwa barabarani kwa ajili ya kuzuia ajali za …

Hii Ndiyo Kazi Yako Ya Kwanza Kwenye Maisha

Ukishazaliwa tu hapa duniani kazi yako ya kwanza kabisa ni kushughulika na watu. Ni kitu gani ambacho unaweza kufanya bila kushughulika na watu? HAKUNA. Kila kazi tunayofanya inahitaji kushughulika na watu wengine ili tuweze kupata kile tunachotaka. Kama kazi yako ya kwanza ni kushughulika na watu unapaswa kujua saikolojia ya kushughulika na watu. Kushughulika na …

Acha Kuteseka Na Hiki Kitu Hapa

Kwa jinsi akili ya binadamu jinsi ilivyo, wako watu ambao wanachoka bila hata ya kufanya kazi kwa sababu ya kufikiria vitu ambavyo hata havipo. Wako watu ambao wanakuwa wanatengeneza picha ya vitu ambavyo hata havipo, kisha ile picha ya vitu waliyoitengeneza inakuja kuwatesa na kuwatengeneza kweli. Aliyekuwa mwanafalsafa wa ustoa, mwanafalsafa Seneca aliwahi kunukuliwa akisema, …

Mtu Pekee Unayepaswa Kushindana Naye

Usishindane au kujilinganisga na mtu yeyote maana utaibua matatizo mengi na tayari matatizo uliyonayo yanakutosha. Huna haja ya kuongeza mengine wakati uliyokuwa nayo hujayamaliza. Usishindane na mtu, bali shindana na wewe mwenyewe wa jana. Kila siku pambana uwe bora uwe bora kuliko ulivyokuwa siku iliyopita. Usikubali siku zako mbili zifanane. Kila siku hakikisha umejifunza na …

Huwezi Kueleweka Na Kila Mtu

Hakuna kazi ngumu sana duniani kama ya kutaka kueleweka na kila mtu. Ukichagua kutaka kueleweka na kila mtu maana yake umechagua kushindwa kabla hata hujaanza kazi. Watu hawajui unachojua, hawaamini unachoamini na hawataki unachotaka. Sentensi hiyo hapo juu isome mara mbili ili ujue watu walivyo badala ya kutaka kueleweka na kila mtu. Lakini, hilo halipaswi …