Design a site like this with WordPress.com
Get started

Shughuli Na Maeneo Unayopaswa Kuyapa Kipaumbele

Kila mmoja wetu anajua ni maeneo gani yuko vizuri sana na maeneo gani hayuko vizuri. Kwa kulijua hilo, tunapaswa kuyapa kipaumbele yale maeneo ambayo yanafanya vizuri sana. Shughuli na maeneo unayopaswa kuyapa kipaumbele sana ni yale yanayokupa furaha. Shughuli na maeneo yanayokupa furaha ndiyo unayopaswa kuyapa kipaumbele zaidi. Usiendelee kujisumbua na mambo mengi. Tulia na …

Badili Mtazamo Huu Kama Unataka Kufanikiwa Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako

Watu wengi wamekuwa na mtazamo mbaya sana ambao unawafanya wasifanikiwe. Kwa mfano, wana mtazamo wa kuchukua au kupewa zaidi kuliko wanavyotoa. Kwa chochote kile ambacho watu wanafanya huwa wanajiandaa na kujiangalia kwanza wao wananufaikaje. Watu hawajali wanawanufaishaje wengine. Kwa mfano, kwa hali kama hii ndiyo maana ukiritimba, rushwa na ufisadi unaendelea kuwepo sehemu nyingi kwa …

Acha Kurusha Mawe Gizani

Kwa sababu hujui nani litampata. Mtenda wa jambo huwa hakumbuki sana kuliko yule anayetendewa. Kumbe basi, unapofanya jambo lolote lile, kumbuka yule anayepokea ndiyo anaona uzito wake. Ndiyo maana unatakiwa kufanya mambo ambayo ni chanya sana kwa sababu unapofanya mambo hasi ni kama unarusha mawe gizani unaweza ukampiga hata mtu ambaye hana hatia yoyote ile. …

Usikimbilie Kuvuka Daraja Kabla Hujalifikia

Huwa tunahangaika na mambo ambayo hata kiuhalisia bado hatujayafikia. Ni kama vile tunafikiria kuvuka daraja kabla hata hatujalifikia. Endelea kufanya kile unachofanya na ukifika wakati wa kuvuka daraja utalivuka. Utashindwa kufanya kile ulichopanga kufanya kwa wakati huu kama akili yako inafikiria kuvuka daraja kabla hujalifikia. Kukimbilia kuvuka daraja kabla hujalifikia ni kuhangaika na mambo ambayo …

Kitu Ambacho Kimepuuzwa Na Watu Wengi Zama Hizi

Katika zama tunazoishi, watu hawapumziki wala hawafanyi kazi. Hapa ninamaanisha kwamba wakati wa kazi mtu anafikiria mapumziko na wakati wa mapumziko mtu anafikiria kazi. Mtu akiwa anakula, uwepo wake hauko kwenye kula bali anafikiria kumaliza aende kufanya kitu kingine. Hii inawafanya hata watu wakila hawaoni ile ladha ya chakula kwa sababu wakati wa kula akili …

Ukikutana Na Mtu Mwenye Akili Hii Muulize Swali Hili

Hata uwe vizuri sana kiasi gani, huwezi ukajitegemea kwa kila kitu. Kwa sababu kujitegemea siyo kujitosheleza. Kadiri unavyotaka kufanikiwa ndivyo unavyozidi kuwahitaji watu wengi zaidi. Na kitu kingine ni kwamba, kadiri unavyojifunza zaidi ndiyo unajikuta hujui. Yaani ukiishi katika falsafa ya aliyekuwa baba wa falsafa mwanafalsafa Socrates ambayo inasema hekima pekee aliyonayo ni kwamba hajui …

Hii Ndiyo Hisia Ya Hovyo Kabisa

Ni chuki. Ni bora hisia nyingine zinaweza kukupa raha lakini chuki inakupa raha gani wewe? Zaidi ya kujiumiza wewe mwenyewe? Chuki na malalamiko hayakufanyi upige hatua hata siku moja. Hii ni kama kujikaanga na mafuta yako mwenyewe. Shabaha yangu kwako leo, usiwe na chuki na watu. Usitengeneze maadui kabisa kwenye maisha yako. Wapende watu, hata …

Sababu Mbili Zinazopelekea Kuwa Tofauti Kwenye Mazungumzo

Siku zote katika mazungumzo kubishana ni njia mbovu sana ya kufikia maamuzi. Kila mtu anakazana kusimamia kile anachoamini. Ni muhimu sana uelewe kwamba kwenye mazungumzo kila mmoja anaweza kuwa na mtazamo tofauti. Leo nimekuandalia sababu mbili zinazopelekea watu kuwa tofauti kwenye mazungumzo. Na mara nyingi mitazamo yetu inakuwa tofauti kwa sababu kuu mbili; Moja, tumepitia …

Mbinu Ya Kufanya Makubwa Kwenye Maisha Yako

Kama unataka kufanya makubwa kwenye maisha, geuza kila maumivu unayopitia au uliyopitia kuwa mwalimu wako. Yatumie maumivu unayokutana nayo kama sababu ya kufanya makubwa. Kwa mfano, kama unateseka katika nyumba za kupanga tumia maumivu hayo kama msukumo wa kujenga nyumba yako.Kama unapata shida kwenye usafiri wa umma, tumia hayo maumivu kupata usafiri wako binafsi. Mateso …

Kuwa Makini Na Kitu Hiki

Na kile unachokiwaza sana. Kwa nini?Kwa sababu kile unachokiwaza au kukifikiria sana huwa kinakuja katika uhalisia wa kawaida. Mawazo yako huwa yanaumba kile unachotaka kwenye maisha yako. Kama unakitaka kitu, kifikirie sana kile kitu na utashangaa kinatokea. Akili zetu ni kama sumaku huwa zinavuta kile tunachokifikiria muda mwingi. Usipoteze nguvu zako kuwaza kitu ambacho hukitaki. …