Design a site like this with WordPress.com
Get started

“Kwa Mkapa Hatoki Mtu”

Ni kauli ya hamasa ambayo klabu ya Simba nchini Tanzania huwa wanaitumia pale wanapokuwa wanacheza na timu inayotoka nje ya Tanzania. Pata nakala yako leo kwa bei ya ofa ya shilingi elfu 5, kupata kitabu chako wasiliana nasi kwa namba 0717101505/0767101504 Imekuwa ni kauli ambayo huwa inawapa hamasa na hatimaye wanaitumia vizuri sana kuhakikisha hakuna …

Hiki Ndicho Kinachokupelekea Kuwa Na Laana

Kinachokupelekea wewe kupata laana ni tabia zako. Unapata laana kwa ajili ya tabia zako mwenyewe. Kwa sababu unatengeneza tabia kisha na tabia zinakutengeneza. Kwa mfano, unatengeneza tabia za uvivu kwenye maisha yako, hujitumi halafu baadaye hufanikiwi unasema unalaana, huna bahati kumbe chanzo kikuu ni tabia ulizojijengea. Kwa mfano, wazazi wengi huwa wanaangalia tabia za watoto …

Kutokujua Sheria Siyo Kigezo Cha Kusamehewa Kosa Lako

Ni kauli ya sheria ambayo inatumika karibu kwenye kila eneo la maisha yetu. Usipofanya kitu kwa sababu hujui usifikiri asili itakuacha salama. Lazima itakupa adhabu ya kutokujua kwako, kwa mfano, unavunja sheria kwa sababu ya ujinga wa kutokujua sheria, usifikiri kutokujua kwako kunaweza kukusaidia, hapana. Angalia sheria za asili zinavyofanya kazi. Watu hawajui misingi ya …

Jinsi Ya Kuepuka Kujitengenezea Balaa

Vitu vingi katika maisha yetu, huwa tunavitengeneza sisi wenyewe, kwa mfano, tunatengeneza tabia na kisha tabia zinatutengeneza. Hata wakati mwingine, balaa huwa mtu anajitengenezea, utaweza kushangaa sasa inakuwaje mtu anajitengenezea. Kuna msemo mwingine unasema akili isiyoshughulika inakuwa ni karakana ya shetani. Mtu ambaye ameamka asubuhi na akaupangilia muda wa vizuri, hata shetani ni ngumu kumjaribu …

Ifanye Siku Ya Mwenzako Kuwa Bora Kupitia Hiki Hapa

Huwezi kuishiwa pale unapotoa thamani kubwa kwa wengine. Kwa mfano, watu wanakula samaki kila siku lakini ulishawahi kusikia samaki wameisha baharini? Ifanye siku ya mwenzako kuwa bora kupitia kile unachofanya.Kile unachofanya kina msaidia mwenzako kuwa bora kwa namna moja au nyingine. Kuna watu wanakutegemea kupitia kile ambacho, hata kama huoni mrejesho wake, lakini jua kuna …

Rudia Tena Kufanya

Karibu kila mtanzania anajua kuimba wimbo wa Taifa bila shida yoyote ile. Na watu wanaweza kuimba wimbo wa Taifa kwa sababu walivyokuwa shuleni walikuwa wanauimba karibu kila siku. Hii imepelekea hata watu wengi kuunasa kichwani na kuuelewa bila shida. Hapa tunajifunza kitu kikubwa sana, ukitaka watu wakielewe kitu, unapaswa kukirudia rudia kitu mara kwa mara …

Huu Ndiyo Upande Wa Kuzingatia Kama Unataka Kitu Chako Kisomwe

Februari 28 tuliyojifunza bidhaa inayonunulia sana ni ile ambayo iko usawa wa macho. Tulijifunza kwamba ni ngumu mtu kuinama na kutafuta bidhaa au kuangalia juu kutafuta vitu. Watu wanapenda urahisi, hawapendi kujisumbua hivyo basi, watakachoona kitu ambacho kipo usawa wa macho yao ndiyo wanashughulika nalo. Leo napenda kukuongea mbinu nyingine ya mauzo, kama unaandaa tangazo …

Usishangae Kuona Mabadiliko Haya Hapa Kwenye Maisha Yako

Unapaswa kuelewa kwamba dunia haisimami. Na wewe pia hausimami, aidha hapo ulipo unaenda mbele au unarudi nyuma. Jichunguze, je, unaenda wapi? Kama dunia haisimami, basi unapaswa kujua kwamba kila kitu kinabadilika. Usishangazwe na mabadiliko unayoyaona kwa watu wengine. Watu wanabadilika na kila kitu kinabadilika. Watoto wanabadilika, ndugu, jamaa, marafiki na hata wenza wetu wanabadilika. Ishi …

Kifahamu Kichocheo Cha Kufanya Au Kutokufanya

Pale unapofanya mambo mazuri unakuwa unajisikia vizuri wewe mwenyewe, na pale unapofanya mambo mabaya unakuwa unajisikia vibaya wewe mwenyewe. Kufanya au kutokufanya huwa kunachochewa na kitu kimoja ambacho ni msukumo wa ndani. Msukumo wa ndani ndiyo mchezo wa mambo yote yale. Hapa ndiyo injini ya sababu je, nifanye au nisifanye. Mtu anafanya kadiri ya msukumo …

Kinachoendelea Ndani Yako Kinaonekana Kwa Nje

Mwandishi Earl Nightingale aliwahi kunukuliwa akisema, kinachoendelea ndani yako kinaonekana kwa nje. Kile unachofikiri kinaamua ni nini utafanya. Kila unachofikiri kila mara kitaamua ni wapi utakapoishia na maisha yako. Hapo wala hakuna ubishi. Mawazo yako unayowaza yawe ni chanya au hasi ndiyo yanakufanya wewe uonekane hivyo ulivyo. Ukifikiria mawazo ya kujenga, utaona matokeo mazuri unayotaka …