Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usitafute Huruma Kwa Watu Wengine

Ni kawaida yetu sisi binadamu pale tunapopitia changamoto mbalimbali zinazotukabili huwa tunaona ni vema na haki kutafuta huruma kwa watu wengine juu ya yale tunayopitia. Tunafikiri kwamba, kwa njia ya kuwaelezea wengine matatizo yetu ili watuhurumie ndiyo tunaweza kutatua tatizo. Pambana na hali yako, usitafute huruma kwa watu, kila mtu ana changamoto zake hivyo yakabili …

Naweza Kuajiri Watu Kunisaidia Kufanya Kila Kitu, Isipokuwa Vitu Hivi Viwili

Frank Bettger katika kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling aliweza kumnukuu na kujifunza kauli moja kutoka kwa aliyekuwa mmiliki wa viwanda alisema hivi, naweza kuajiri watu kunisaidia kufanya kila kitu isipokuwa vitu viwili tu, kufikiri na kufanya vitu kwa mpangilio wa umuhimu wake. Rafiki yangu, huwa nakushirikisha hapa vitu …

Hiki Ndiyo Kinaathiri Maisha Yako

Dunia inatufundisha vitu vingi, kwa kuona, kusikia na kwa kufanya. Asili huwa inatufundisha vitu vingi sana katika maisha lakini changamoto kubwa ya watu wengi hawajui namna ya kukielewa kile ambacho asili huwa inawafundisha. Ruben Gonzalez aliwahi kunukuliwa akisema, kinachoathiri maisha yako siyo kinachotokea, bali jinsi unavyopokea na kufanyia kazi kinachotokea. Nakubaliana na Ruben Gonzalez kwa …

Usifanye Chochote Kwa Sababu Unataka Kuwafurahisha Watu

Kwa chochote unachofanya kwenye maisha yako ni kawaida kukutana na makundi ya aina tatu ya watu. Wapo ambao watakubaliana na wewe.Wapo ambao watapingana na wewe.Na wapo ambao hawatajali hata unafanya nini. Kwenye maisha usifanye kitu kwa kutaka uwafurahishe watu, hiyo ni kazi ngumu ambayo hutakuja kuimaliza kamwe. Kama kuna chochote unataka kukifanya kwenye maisha yako, …

Ili Uweze Kufanikiwa Usizame Kwenye Haya Mambo Kabisa

Pata picha umewahi kukutana na mambo mabaya na katika maisha yako kiasi kwamba ukifikiria unazidi kuumia zaidi. Kuna watu walikunyanyasa, kukutesa, kukudhulumu na kukuumiza sana kwenye maisha yako. Hata ukikumbuka yaliyopita hayataweza kukusaidia kitu, upo hapo ulipo sasa unachagua nini? Unachagua kuendelea kuzama kwenye yaliyopita au kuangalia wapi unakokwenda? Shabaha yangu kubwa leo ni kukutaka …

Mbinu Mbili Za Kumshawishi Mtu Aliyekuzidi

Kuna wakati unataka kumshawishi mtu aweze kukubaliana na wewe lakini unajikuta unashindwa kufanya zoezi hilo labda kwa kuona yule unayetaka kumshawishi amekuzidi karibu kila kitu. Sasa kama mtu ameshakuzidi kwa kila kitu wewe utamwambia nini sasa? Kama ulikuwa na tatizo kama hilo, leo nakwenda kukupatia suluhisho lako. Pata picha kwamba unaenda kumshawishi mtu aliyekuzidi na …

Kitu Cha Kutegemea Kwa Binadamu

Ni mabadiliko. Unapokuwa na mtu yeyote yule mpe nafasi kwamba iko siku atakuja kubadilika na ukishajiandaa hivyo kisaikolojia na likija kutokea kweli halitakuumiza. Unapaswa uishi falsafa ya ustoa, unapaswa kutegemea mambo kwenda tofauti na unavyotarajia. Unapaswa kutarajia kwamba watu wanabadilika, hivyo kuwa tayari kupokea chochote kile kutoka kwa mtu hata ambaye ulikuwa hutarajii kama anaweza …

Fuata Moyo Wako

Mara nyingi sisi binadamu huwa tunapata ishara mbalimbali kupitia miili yetu juu ya kitu fulani kutokea. Kwa mfano, unaweza kukutana na mtu ambaye si salama kwako, kwa kumuangalia tu mwili wako unasisimka na kukupa ishara kwamba mtu fulani siyo salama. Ni muhimu sana kuheshimu ishara tunazopata. Heshimu machale unayopata kupitia vitu mbalimbali kwenye maisha yako. …

Usitaharuki Unapokutana Na Changamoto Bali Nunua Hiki Hapa

Unapokutana na changamoto hutakiwi kutaharuki badala yake unatakiwa kununua utulivu wa hali ya juu. Karibu sana ujiunge na Mimi Ni Mshindi Klabu ili uweze kupata mafunzo mbalimbali ninayoendelea kuyatoa. 0717101505 kwa mawasiliano ya jinsi ya kujiunga. Kwani, unapotaharuki uwezo wako wa kufanya maamuzi sahihi kifikra unakuwa chini na hisia zinakuwa juu. Huwezi kuamua jambo wakati …

Mchezo Unaongoza Kuchezwa Na Watu Wengi

Ni mchezo wa kulaumu. Huwa tunashiriki mchezo wa kulaumu, kwa kuangalia mtu wa kumnyooshea kidole ambaye anahusika na kile ambacho kimetokea. Tatizo lolote lile linapotokea, huwa tunatafuta mtu wa kumlaumu na mara nyingi mtu wa kumlaumu huwa hakosekani kabisa. Lakini, kwenye kila tunacholaumu, huwa tunajionesha sisi zaidi kuliko hata wale tunaowalaumu.. Tuache kuangalia wengine kama …