Design a site like this with WordPress.com
Get started

Sababu Mbili Zinazowapelekea Watu Kununua

Kwanza unapaswa kujua kwamba watu hawanunui kwa sababu ya bei. Watu wananunua kwa sababu ya thamani na mapenzi. Usijidanganye kwamba watu wananunua kwa sababu ya bei kuwa chini. Kwenye mauzo watu wamekuwa wanajidanganya kwamba sababu za watu kutokununua ni kwa sababu hawana fedha au kitu ni bei ghali. Hivyo wengi hukimbilia kupunguza bei wakiamini ndiyo …

Ukitaka Kuuza Sana Gusa Hisia Hizi Za Mteja Wako

Watu huwa wanaongozwa na hisia kuu mbili.Moja hisia ya kupata na mbili ni hisia ya kupoteza. Ukitaka kuuza, hakikisha unagusa hisia za wateja wako. Hisia kama za maumivu, kupoteza, matumaini, hofu nk. Unapaswa kujua kwamba, watu hawafanyi manunuzi kwa njia ya fikra bali hisia. Unagusa hisia za wateja wako pale biashara yako inapokuwa halisi na …

Changamoto Zote Kwenye Biashara Zinatatuliwa Na Kitu Hiki Kimoja

Ni mauzo tu. Mauzo ndiyo yanayotatua changamoto kwenye biashara. Kama biashara haina mauzo lazima itakua na changamoto nyingi. Kwa sababu mauzo ndiyo yanaleta fedha kwenye biashara. Na fedha ikiwepo kwenye biashara, biashara lazima itaenda vizuri. Fedha itakusaidia kujilipa, kulipa gharama za biashara, kuajiri watu bora, kulipa kodi na gharama zingine ambazo fedha inaweza kutatua. Mauzo …

Kitu Kimoja Muhimu Sana Cha Kujifunza Kuhusu Mauzo Kutoka Kwa Aliyekuwa Muuzaji Bora Wa Magari Duniani

Joe Girard alikuwa ni muuzaji bora wa magari na alifanikiwa kuingia kwenye kitabu cha maajabu ya dunia GUINESS kwa sababu ya kuuza sana. Ni muuzaji ambaye hajawahi kutokea duniani, na kwa kuwa maisha ya binadamu ni mauzo nasi pia tunatakiwa kujifunza mbinu za mauzo. Kila mtu ni muuzaji, kila mtu ana kitu anauza. Kwenye kitabu …

Hii Ndiyo Biashara Inayofanikiwa

Watu wengi wanajua kwamba, biashara inayofanikiwa ni ile ambayo inakuwa bora. Lakini, biashara inayofanikiwa siyo ile inayokuwa bora,Bali, ni ile inayokuwa ya kwanza kwenye akili za wateja. Kazi yako kubwa kwenye biashara yako, ni kuifanya biashara yako ifikiriwe na wateja kwenye akili zao. Mteja akishaifikiria biashara yako, pale anapokuwa anauhitaji wa kununua kitu, hana sehemu …

Inafanya Kazi Vizuri Sana

Kabla mteja hajanunua kitu kwako anachotaka ni kupata uhakika juu ya kile unachouza kwanza. Sasa wauzaji wengi huwa hawawapi wateja uhakika. Hata mgonjwa akiwa anaumwa akimuuliza daktari je, nitapona na daktari akimpa matumaini ndiyo utapona mgonjwa anakuwa na matumaini lakini akimwambia huponi atampoteza. Na unaweza kumpoteza mteja kama hujampa uhakika wa kile unachouza. Ukimwambia hakifanyi …

Kama Unataka Kuwa Muuzaji Mzuri, Kuwa Na Tabia Hizi Mbili

Kiasili, kila mtu ni muuzaji.Kila mtu anauza kila wakati, haijalishi wewe ni nani, kila unapokutana na mtu mwingine, unapoelezea wazo lako, unapotoa maoni yako, unauza kitu muhimu sana, ambacho ni wewe mwenyewe. Kitendo tu cha kuweza kumshawishi mtu na akubaliana na wewe hapo unakuwa muuzaji. Kwa sababu umeuza mawazo yako kwa wengine. Kama unatafuta kazi …

Hawa Ndiyo Wateja Wazuri

Ukiwa katika mauzo hakuna mteja mzuri kama yule ambaye anajua nini haswa anataka. Mteja anayejua kile anachotaka ni rahisi kumhudumia na kumpatia huduma bora. Mteja anayejua kile anachotaka anakuokolea muda. Ukilinganisha na mteja ambaye hajui nini anataka mpaka umweleweshe kila bidhaa kisha achukue maamuzi inachukua muda mrefu kukuelewa na kuchukua hatua ya kufanya manunuzi. Kila …

Hawa Ndiyo Watu Ambao Wanafanikiwa Sana Duniani

Ni wale ambao wana uwezo wa kuuza, wale ambao wanaweza kuuza wanafanikiwa kuliko wasioweza kuuza. Kadiri mtu anavyokuwa bora kwenye kuuza, ndivyo anavyoweza kupiga hatua zaidi. Watu wa mauzo ni moja ya watu wenye mafanikio makubwa sana kwa ujumla ukilinganisha na watu wengine. Ndiyo maana kila mmoja anapaswa kujifunza mbinu za mauzo kwa sababu kila …