Design a site like this with WordPress.com
Get started

Haya Ndiyo Majibu Unayopaswa Kumpatia Mteja Wako Pale Anapokuuliza Kuhusu Washindani Wako

Wafanyabiashara wengi huwa wanajua njia pekee ya kukubalika na mteja ni kumsema vibaya mshindani wake. Baadhi ya wafanyabiashara huwa wanachukiana na hata kujenga uadui kabisa hasa zaidi pale anapoona mteja wake ameenda kupata huduma sehemu nyingine au mshindani wake anauza zaidi au anapata wateja zaidi. Kumekuwa hakuna habari njema dhidi ya washindani tunaofanya nao biashara …

Kazi Kubwa Ya Muuzaji Katika Mauzo

Maisha yetu ni mauzo na kila siku tuko katika mchakato wa mauzo. Mauzo ndiyo habari ya mjini kwa kila binadamu, kwa sababu mauzo ndiyo yanatufanya tuweze kupata kitu ambacho tulikuwa hatuna. Kila anayeuza kuna thamani anaitoa kwa mtu mwingine na mtu anapotoa thamani kwa wengine anapaswa kulipwa. Kumbe basi, hakuna mtu ambaye anatengeneza bidhaa kwa …

Vitu Viwili Vya Kumwelezea Mteja Wako

Kama tunavyojua mteja ndiyo mfalme kwenye biashara yoyote ile. Siyo tu ni mfalme bali pia mteja ndiyo bosi. Mteja anaweza kukufukuza kazi hata kama biashara ni yako. Unaweza kujiuliza biashara ni yangu iweje mteja anifukuze? Akiacha kununua kwako na akiwaambia na mwenzake mpaka hapo anakuwa ameshakuharibia biashara yako. Na unapaswa kujua kwamba, mteja huwa hakosei …

Agiza Tukuletee

Maisha yamebadilika, zama zimebadilika na watu wamekuwa na mambo mengi huku muda ukiwa mchache sana ukilinganisha na mambo wanayotakiwa kufanya. Ili ufanikiwe kwenye mauzo unatakiwa kupiga pale kwenye maumivu. Huwezi kuuza kama unapiga kwenye uimara wa mtu bali utaweza kuuza kama ukipiga kwenye udhaifu wa mtu. Ili upate ushindi wowote ule, usikimbilie kwenye uimara wa …

Nitakutafuta Nikiwa Tayari

Nitakutafuta nikiwa tayari, ni jibu ambalo watu wengi wanaouza wanakutana nalo sana kwa wateja. Hakuna kazi ngumu kama ya mauzo kwa sababu mauzo ni kitendo cha mteja kujitenganisha na fedha zake. Hivyo inahitaji kazi kumshawishi mteja mpaka atoe fedha yake kwa amani bila kinyongo. Fedha ni rasilimali yenye uhaba kwa kila mmoja wetu. Na kutoa …

Ifahamu Siri Muhimu Kuliko Zote Kwenye Mauzo

Biashara zote ambazo hazifanyi vizuri tatizo lake moja linakuwa kwenye mauzo. Kama biashara haina mauzo mazuri maana yake haina maisha. Mauzo ndiyo kila kitu kwenye biashara, yaani pumzi kwenye biashara. Mauzo yanapokuwa vizuri, biashara inakuwa vizuri maana itapata fedha ya kujiendesha. Kwenye kitabu cha How I Raised Myself From Failures to Success in Selling, mwandishi …

Sababu Mbili Zinazowapelekea Watu Kununua

Kwanza unapaswa kujua kwamba watu hawanunui kwa sababu ya bei. Watu wananunua kwa sababu ya thamani na mapenzi. Usijidanganye kwamba watu wananunua kwa sababu ya bei kuwa chini. Kwenye mauzo watu wamekuwa wanajidanganya kwamba sababu za watu kutokununua ni kwa sababu hawana fedha au kitu ni bei ghali. Hivyo wengi hukimbilia kupunguza bei wakiamini ndiyo …

Ukitaka Kuuza Sana Gusa Hisia Hizi Za Mteja Wako

Watu huwa wanaongozwa na hisia kuu mbili.Moja hisia ya kupata na mbili ni hisia ya kupoteza. Ukitaka kuuza, hakikisha unagusa hisia za wateja wako. Hisia kama za maumivu, kupoteza, matumaini, hofu nk. Unapaswa kujua kwamba, watu hawafanyi manunuzi kwa njia ya fikra bali hisia. Unagusa hisia za wateja wako pale biashara yako inapokuwa halisi na …

Changamoto Zote Kwenye Biashara Zinatatuliwa Na Kitu Hiki Kimoja

Ni mauzo tu. Mauzo ndiyo yanayotatua changamoto kwenye biashara. Kama biashara haina mauzo lazima itakua na changamoto nyingi. Kwa sababu mauzo ndiyo yanaleta fedha kwenye biashara. Na fedha ikiwepo kwenye biashara, biashara lazima itaenda vizuri. Fedha itakusaidia kujilipa, kulipa gharama za biashara, kuajiri watu bora, kulipa kodi na gharama zingine ambazo fedha inaweza kutatua. Mauzo …

Kitu Kimoja Muhimu Sana Cha Kujifunza Kuhusu Mauzo Kutoka Kwa Aliyekuwa Muuzaji Bora Wa Magari Duniani

Joe Girard alikuwa ni muuzaji bora wa magari na alifanikiwa kuingia kwenye kitabu cha maajabu ya dunia GUINESS kwa sababu ya kuuza sana. Ni muuzaji ambaye hajawahi kutokea duniani, na kwa kuwa maisha ya binadamu ni mauzo nasi pia tunatakiwa kujifunza mbinu za mauzo. Kila mtu ni muuzaji, kila mtu ana kitu anauza. Kwenye kitabu …