Siyo tu bila maumivu mteja hawezi kununua bali pia bila maumivu huwezi kuuza. Maumivu aliyonayo mtu ndiyo yanamsukuma kuchukua hatua katika mauzo. Kama mtu hana maumivu hakuna chochote kitakachomshawishi kuchukua hatua kwa mfano, wewe unauza dawa ya kufunga kuharisha na mteja anakuja kwako akiwa anaumwa sana, na wewe umeshajua maumivu ya mteja ni kupata dawa …
Category Archives: Masoko Na Mauzo
Mauzo Hayaishii Pale Anaponunua Bali…
Maisha ni mauzo na yeyote anayeweza kuuza vizuri zaidi ndiye anayefanikiwa. Na utaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako kama utaweza kuuza zaidi. Tunauza muda wetu, utaalamu wetu, uzoefu wetu, huduma zetu na hata bidhaa mbalimbali. Pia tunauza mawazo yetu, ushawishi wetu na hata ndoto na maono makubwa tuliyonayo. Mauzo huwa hayaishii pale tu mteja …
Anza Na Soko
Wafanyabiashara wengi wanakosea kitu kimoja, wanaanza na bidhaa badala ya kuanza na soko. Kabla hujazalisha tafuta kwanza soko la kwenda kuwauzia kile unachozalisha. Unapaswa kutafuta kundi ambalo tayari lina njaa, kisha unaliuzia kundi hilo chakula. Kwa kuwa watu wengi wanakosea kwa kuanza na bidhaa kisha kutafuta soko,wewe anza na soko kisha bidhaa. Ukishakuwa na watu …
Usiuze Sifa, Uza Manufaa
Kwenye mauzo, usihangaike sana kutaja sifa za bidhaa zako, jitahidi sana kuuza manufaa ambayo mteja atapata baada ya kununua bidhaa yako. Huwa tunafanya makosa sana kwenye mauzo, unamwambia mteja sifa za bidhaa zako ambazo kiuhalisia sifa hazimsaidii mteja kwa changamoto alizonazo. Mteja atafarijika pale bidhaa yako itakapokwenda kumtatulia changamoto zake. Pale bidhaa itakapokuwa suluhisho la …
Wakati Mwingine Unashindwa Kuuza Kwa Sababu Hii Hapa
Kuna wakati utajiona kama vile una kisirani, huna bahati kwa sababu kila unavyopambana kuuza huuzi. Kuna kosa moja ambalo unafanya na kosa hilo ni kukosa shauku. Shauku ndiyo sifa namba moja inayolipa duniani. Yeyote anayeongea kwa shauku au kufanya kitu chochote kwa shauku anakuwa anauza kile anachofanya. Shauku ni ile hali ya uungu ndani yako, …
Continue reading “Wakati Mwingine Unashindwa Kuuza Kwa Sababu Hii Hapa”
Sina Uhakika Kama Itakufaa Lakini Kama Ungetumia Muda Wako Kufanya Hivi Ungekuwa Mbali Sana Kibiashara
Binadamu wote tuna asili ya uvivu na uzembe. Ili maisha yako yaende vizuri lazima kwanza uzikatae dhambi hizi mbili ambazo ni uzembe na uvivu. Unakuta mtu analalamika hana fedha, mauzo ni madogo kwenye biashara, mshahara ni mdogo lakini hachukui hatua yoyote itakayomwezesha kuwa bora. Kwa wale ambao ni wauzaji, najua hata wewe ni muuzaji kwa …
Hiyo Hela Tuma Kwenye Namba Hii
Matapeli ni watu wazuri sana kwenye mauzo. Wanapotuma meseji kila siku kwa watu elfu moja wanajua wazi kabisa hawawezi kukosa wateja ambao wanaenda kutuma hela na wakafanikiwa kuwapata. Ndiyo maana watu wakipata ujumbe wa matapeli kwenye simu zao wengine huwa waingia laini, wananaswa. Kwa sababu gani? Wanajua ni kanuni ya asili kwamba, katika watu wengi …
Njia Za Kuongeza Thamani Ya Maisha Ya Wateja Wako
Wateja wako wanapokaa na wewe kwa muda mrefu ndivyo unavyonufaika zaidi. Ili ukae na mteja muda mrefu unatakiwa uendelee kumfuatilia mpaka pale atakapokufa. Na hata pale atakapokufa bado unaweza kuwafuatilia wale watu wake wa karibu na kuwafanya kuwa wateja wako. Unahitaji kuweka juhudi kuhakikisha wateja wanabaki na wewe muda mrefu. Yafuatayo ni mambo muhimu ya …
Continue reading “Njia Za Kuongeza Thamani Ya Maisha Ya Wateja Wako”
Kosa Moja Ambalo Wauzaji Wengi Wanafanya
Mwandishi na aliyekuwa muuzaji mzuri sana wa magari Joe Girard, ambaye aliingia kwenye kitabu cha maajabu cha dunia, GUINESS, kama muuzaji bora sana kuwahi kutokea hapa duniani, anatushirikisha jinsi gani KILA MTU, ANAWEZA KUUZA CHOCHOTE KWA MTU YEYOTE kupitia kitabu chake cha jinsi ya kuuza chochote kile kwa mtu yeyote. Kupitia mauzo tunapata zawadi mbili, …
Vitu Vya Kuzingatia Kwa Muuzaji
Kitu cha kwanza kinachowasukuma watu kununua ni haiba ya muuzaji. Na haiba ya mtu inatokana na tabia ambazo mtu anazo. Ili kufanikiwa kwenye jambo lolote, unahitaji kuwa na tabia nzuri ambazo zinawafanya watu kukubaliana na wewe. Kumbuka ndege wanaofanana huruka pamoja, hivyo kuwavutia watu wa aina fulani, lazima uwe kama wao. Hatua ya kuchukua leo; …