Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usitawanye Nguvu Zako

Rafiki, jihusishe na kitu kimoja pekee na komaa na kitu hicho mpaka utakapofanikiwa au pale uzoefu wako unapokuonesha kwamba ni wakati wa kuachana nacho. Kwa mfano, kugonga nyundo kwenye msumari mmoja kwa kurudia rudia kunafanya msumari huo uingie ndani. Pale ambapo umakini wa mtu unawekwa kwenye kitu kimoja, akili yake inakuwa inamletea njia za kuboresha …

Watu Wengi Wamekosa Kitu Hiki Kwenye Maisha Yao

Leo asubuhi katika kipindi cha Billionaires in training, nimejifunza kitu kimoja kwamba watu wengi hawafanikiwi kwa sababu ya kukosa ustaarabu wa hali juu. Ni watu wachache sana katika jamii yetu ambayo wana ustaarabu wa hali ya juu, watu wamezoea kufanya kitu mpaka waambie kufanya. Ni kitu cha ajabu sana kwamba mtu anajua wajibu wake lakini …

Anzia Mahali Fulani

Kwenye maisha ili upate uzoefu wa kitu chochote kile, unapaswa kuanzia mahali fulani ili upate uzoefu. Ukienda sehemu wanakuhitaji utoe uzoefu wako juu ya kile unachofanya, hutakiwi kubaki unatoa macho tu, bali unatoa uzoefu wako kwa kile ulichowahi kufanya. Maisha siyo visingizio visivyokuwa na maana, bali ni kuonesha matokeo ya kile unachofanya au ulichofanya. Ili …

Sanaa Iliyosaulika Lakini Yenye Nguvu Kubwa

Kusikiliza kwa makini ni Sanaa Iliyosaulika lakini yenye nguvu kubwa sana ya ushawishi. Ndiyo maana una mdomo mmoja na masikio mawili, kwamba unapaswa kusikiliza zaidi kuliko kuongea. Watu wengi huwa ni waongeaji sana na kitu kinachowazuia wasiweze kuwajua wengine na kuwashawishi. Kwenye kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling, mwandishi …

Jifunze Kwa Mtu Aliyepitia Magumu Na Akafanikiwa Ndoto Yake

Tabia huwa zinatengenezwa pale tunapopitia magumu. Katika magumu, ndiyo watu huwa wanatumia uwezo wao mkubwa uliopo ndani yao. Na uzuri ni kwamba hakuna mtu ambaye hana changamoto yaani yeye nyumbani kwake amebandika bango mlangoni kwamba hapa hakuna matatizo. Ulishawahi kuona nyumba ya namna hiyo? Kama hujawahi kuona, jua kwamba kila binadamu anapitia magumu yake. Leo …

Ufunguo wa Kushindwa

Bill Cosby aliwahi kunukuliwa akisema, sijui ufunguo wa mafanikio ni upi, lakini ufunguo wa kushindwa ni kujaribu kumridhisha kila mtu. Sidhani kama nitakuwa na maneno mengine zaidi ya hayo. Ukitaka kushindwa kwenye maisha yako, basi jaribu kumridhisha kila mtu. Na ukitaka kufanikiwa kwenye maisha yako ishi vile utakavyo lakini usivunje sheria za asili na za …

Miaka 200 Ijayo

Kuwa na kiasi kwenye maisha yako, haijalishi umefanikiwa kiasi gani miaka 200 ijayo huenda hakuna atakayejua hata kama uliishi hapa duniani. Kila unapoanza kujiona wewe ni muhimu kuliko wengine kumbuka kitakachotokea MIAKA 200 ijayo na dunia itakua imekusahau kabisa. Rafiki, ishi maisha yenye maana kwako na siyo maisha ya kujionesha na kutaka wengine waone wewe …

Maisha Bora Ni Kufanya Vitu Hivi

Vitu tunavyofanya kwenye maisha yetu vina pande mbili; Moja raha naMbili maana. Tunasukumwa kufanya vitu kwa sababu labda vina raha kwetu kufanya au vina maana kwetu. Maisha bora ni kufanya vitu ambavyo vina raha na maana na siyo kuegemea upande mmoja pekee. Kuna wakati unahitaji kufanya vitu vya raha na ukijisikia kufanya hivyo fanya kwa …

Jiwekee Ukomo

Kila kitu kinahitaji ukomo kwenye maisha yako.Na usipokuwa na ukomo kwenye vitu unavyojihusisha navyo utajikuta unachoka na kupoteza nguvu kubwa pia. Jiwekee ukomo kwenye vitu utakavyojihusisha navyo, jua ni maeneo gani uko vizuri na weka juhudi kwenye hayo, mengine yote achana nayo. Huhitaji kufanya kila kitu ndiyo ufanikiwe, unahitaji kufanya machache kwa ubora wa hali …

Utaishia Kuwa Hivi

Kama unafanya vitu ili wengine wakuone na kukusifia, nakuhakikishia kuwa utaishia kuwa mtumwa wa wengine. Acha kupima umuhimu wako kwa namna wengine wanavyokuchukulia, fanya kile kilicho sahihi kwako na usijali wengine wanasema au kuchukuliaje. Haya siyo maisha ya kujali sana watu wanasemaje, bali jiangalie wewe mwenyewe. Nataka kukuuliza swali? Unafikiri nani anayejali maisha yako?Nani anakosa …