Design a site like this with WordPress.com
Get started

Vikwazo  Viwili  Vinavyokuzuia  Kupata Kile Unachotaka

Kwa  haya  yote unayojifunza,  kwamba  unaweza  kupata  chochote unachotaka,  mawazo yako  yanavuta  chochote  unachofikiria,  unaweza  kuhisi ni uongo  kwa  sababu  labda wewe umejaribu  lakini hujapata  ulichokuwa  unataka. Kwa sababu kuna wengine wanapenda kuona matokeo ya haraka, hivyo wakijaribu na kuona hakuna kitu wanaacha kabisa na kukimbilia fursa nyingine. Kama  hivi ndivyo  unavyofikiria, basi  kuna  vitu  …

Ukiwa Na Utulivu Wa Akili

Utaweza kufanya makubwa na kutatua changamoto nyingi zinazojitokeza kwako. Hata ukiletewa changamoto ambayo wengine wanaona ngumu wewe unaitatua vizuri sana kwa sababu tu umekuwa na utulivu wa akili. Unapokuwa na utulivu wa akili maana yake uwezo wako wa kufikiri unakuwa juu. Hivyo hata maamuzi unayofanya yanakuwa sahihi kwa sababu hayaongozwi na hisia. Mtu mwenye hisia …

Hizi Hapa Sababu Tatu Kwa Nini Tunathamini Zaidi Tunachomiliki

Ukisoma kitabu cha Predictably Irrational, nguvu zilizojificha ambazo zinatengeneza maamuzi yetu. Mwandishi ametushirikisha sababu tatu kwanini Tunathamini zaidi kile tunachomiliki. Kwanza  tunakuwa  tunakipenda,  ukikaa  na  kitu  kwa  muda  unakuwa  unakipenda  na hivyo  kukipa  thamani zaidi. Pili, tunaangalia  kile  tunachopoteza  kuliko  tunachopata,  hivyo  mtu  anapouza  kitu, anaona  kama  anapoteza  kile  anachomiliki  na  kupenda  na  siyo  kupata  …

Dunia Huwa Inampisha Mtu Huyu

Dunia inampisha yule ambaye anajua wapi anapokwenda. Kama hujui wapi unapokwenda dunia haiwezi kukupa njia. Ni kawaida katika maisha, pale mtu anapopanga kufanikiwa na kupiga hatua zaidi kwenye yake, ndipo vikwazo vya kila aina vinaibuka. Hii ni njia ya dunia kukupima kama kweli umejitoa kufanikiwa zaidi. Na yule ambaye anaonesha nia, dunia huwa inampisha yule …

Usitake Kila Mtu Ajue Kitu Hiki Kuhusu Wewe

Si vema kila mtu ajue maisha yako binafsi ila wale ambao ni watu muhimu kwako. Usiruhusu kila mtu ajue maisha yako binafsi, kwa sababu kwa kufanya hivyo unawapa watu nafasi ya kutumia taarifa hizo kukuangamiza. Mitando ya kijamii siku hizi imekuwa ni sehemu ambayo watu wamekuwa wanaanika mambo yao binafsi. Hii inapelekea watu kukusanya taarifa …

Nilichojifunza Kwenye Haya Maisha

Pale tunapokutana na changamoto au mambo hajaenda kama vile tunavyotaka sisi huwa kitu cha kwanza tunachofikiria ni nani amesababisha lakini huwa tunajisahau na sisi tumehusikaje kutokea kwa kile kilichotokea. Hata sisi wenyewe huwa tunachangia sana kwa changamoto mbalimbali katika maisha yetu lakini huwa hatukubali tunajiona sisi ni watakatifu. Kwenye kila kitu kinachotokea kaa chini jiulize …

Tunza Uadilifu wako

Uadilifu ni kuishi kile ulichoahidi na unachosimamia kwa mfano, umeahidi utakua mwaminifu katika maisha yako. Basi unaishi kile ambacho umekiahidi na ukienda kinyume maana yake umevunja uadilifu wako. Uadilifu wako una thamani kubwa kuliko almasi hivyo basi, usifanye chochote kile cha kuharibu uadilifu wako kwa sababu ukishauchafua ni vigumu kuusafisha. Umekula kiapo cha kuwa mwaminifu …

Tabia Inayowashinda Watu Wengi

Ni uaminifu. Watu wameshindwa kuwa waaminifu kwao wenyewe na kwa wengine. Uaminifu ndiyo mtaji unaolipa kwenye kila eneo la maisha yetu. Kuanzia kazi, mahusiano, biashara na nk. Kama kila mmoja angekuwa mwaminifu tu kwenye mambo madogo ambayo anajiwekea kufanya na angeyafanya basi dunia ingekuwa sehemu salama sana. Usiishi kwa kufuata mkumbo wa watu, kama watu …

Nawasaidia Lakini Hawana Shukrani

Ukiwa ni mtu wa kutaka kurudishiwa shukrani pale unaposaidia basi utaumia sana kisaikolojia. Waswahili wanasema shukrani ya punda ni mateke. Kazi yako kubwa iwe ni kufanya kazi yako na siyo kusubiri shukrani. Wewe toa bila kuwa na matarajio ya kupokea. Pata picha kuku anavyotimiza wajibu wake wa kutaga na kutoa mayai, ulishawahi kumuona akilalamika hata …

Tahadhari; Usikosee Wito Wako

Kukosea wito wako, ni sawa na mtu anayefanya kazi sana halafu haoni matokeo anayozalisha. Na hakuna kitu kigumu kama kujua wito wako, ukikosea wito ni kama vile umepotea njia. Kitu muhimu ambacho ningependa uondoke nacho hapa leo ni kwamba utafanikiwa zaidi iwapo utafanya kazi au biashara inayoendana na wito uliopo ndani yako. Achana na kufanya …