Design a site like this with WordPress.com
Get started

Haya Ndiyo Maisha Ambayo Hayana Msingi Wa Kuishi

Rafiki, Usiishi tu kama mbuzi, bali ishi kama binadamu mwenye uwezo mkubwa wa akili.  Ishi kwa malengo, unatakiwa kuwa na malengo ya siku, wiki, mwezi na hata mwaka.  Usipokuwa na malengo ya kitu chochote utapoteza siku, muda bila kujua hata muda na siku zimeishaje. Wengi hawajiongozi kwa ratiba tokea wanapoamka asubuhi na mapema bali wanaongozwa …

Hivi Ndivyo Vitu Ambavyo Hupaswi Kushukuru Kwenye Maisha Yako

Rafiki, Tunaalikwa kushukuru kwa kila jambo, lakini siyo kila jambo tunapaswa tu kushukuru nitakuambia baadaye kivipi. Kushukuru ni utamaduni wa kila mwanadamu, tukikosa kushukuru basi tutakuwa hatuna fadhila. Tunaposhukuru ndiyo tunatengeneza nafasi ya kupata zaidi. Kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako halafu umeshindwa kukifanya hupaswi kukaa chini na kusema nashukuru kwa kila jambo. Unashindwa …

Hiki Ndiyo Kipimo Cha Kuonesha Kama Umeelewa Kitu

Mara nyingi unapokuwa unafundisha unatakiwa kuwaelezea wanafunzi kwa lugha rahisi ili waweze kukuelewa. Kumfundisha mtu kwa lugha ngumu ambayo haielewei huo ni ujinga. Aliyekuwa mwanafizikia Einstein aliwahi kusema, kama huwezi kuelezea kitu kwa lugha rahisi basi hujakielewa. Kwahiyo, kipimo cha kuonesha kama wewe umeelewa kitu ni kuwaelezea wengine kwa lugha rahisi. Ukiona huwezi kuelezea kwa …

Ukienda Sokoni Nunua Mahitaji Usinunue Maradhi

Ukienda sokoni jitahidi sana kununua mahitaji muhimu sana na siyo maradhi. Wengi huwa tunaenda sokoni lakini hatuendi kununua mahitaji bali tunaenda na mengi ambayo yanatusababishia kuyapata ambayo siyo muhimu. Ukiwa na fedha mkononi unatakiwa kuwa makini sana, maana fedha uliyonayo inaweza kukusaidia kununua maradhi au uhai. ‘’ nimewapeni uchaguzi kati ya uhai na kifo, kati …

Hiki Ndiyo Kitakachoweza Kukutoa Hapo Ulipo

Kila mtu anapenda kutoka katika maisha yake. Tunapenda mafanikio kwenye maisha yetu lakini mafanikio haya tunayoyataka yanaletwa na kitu kimoja ambacho mtu akikubaliana nacho ataweza kufanikwa sana. Matendo yetu huwa hayaendani na kile tunachokipenda kwenye maisha yetu. Hatuweki juhudi za kweli zinazoendana na kile tunachotaka hasa. Tunaishia tu kuongea kwa mdomo. Kama unataka kufanikiwa jiambie …

Kitu Muhimu Cha Kufanya Kabla Ya Kutatua Tatizo

Rafiki, Huwa ni kawaida ya binadamu kukutana na changamoto, kama unaishi basi huwezi kulikwepa hilo kwenye maisha yako. Huwa tunapopatwa na matatizo muda mwingine tunayatatua matatizo hayo kwa njia ya hisia na siyo kwa kutumia akili. Na kitu kinachotatuliwa kwa hisia huwa kinakuja kuwa na athari baadaye, tukiwa ni watu wa kutatua au kufanya maamuzi …

Hiki Ndiyo Kitu Unachopaswa Kukiamini Na Kukithibitisha

Mpendwa rafiki, Kila mmoja wetu anakosea, na anafanya makosa pia. Hakuna binadamu aliyekamilika na ambaye hafanyi makosa. Watoto wadogo wanapojifunza katika shule za awali huwa wanatumia penseli na ufutio kwa sababu wanapojifunza huwa wanakosea sana, wanapokosea wanafuta na ndiyo maana hawatumii kalamu kujifunza. Jiamini kuwa wewe ni mtu bora katika ufanyaji wa kitu fulani, ila …

Kabla Hujaendelea Na Safari Ya Mafanikio Yako Soma Hapa Kwanza

Kila mmoja wetu anasafiri safari yake ya mafaniki, kila mtu ana njia yake ya kupita kule anakotaka kufika. Lakini kabla hatujaendelea na safari zetu hebu tukae chini tujiulize hili swali. Je uko kwenye njia sahihi? Kama hauko kwenye njia sahihi tafadhali usiendelee kuongeza mwendo. Kwa sababu kuendelea kuongeza mwendo kwenye njia ambayo siyo sahihi ni …

Hii Ndiyo Sababu Inayokufanya Wewe Usifanikiwe

Kila mmoja wetu anapenda kufanikiwa lakini siyo kila mmoja wetu yuko tayari kulipa gharama za mafanikio anayotaka. Kufanikiwa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine, ingekuwa ni rahisi kila mtu angefanikiwa kwa sababu ni ngumu ndiyo maana wachache ndiyo wanafaidi matunda ya mafanikio hapa duniani. Mafanikio yana kazi sana, kwanza tunapotaka mafanikio fulani katika maisha yetu …

Huyu Ndiyo Mtu Wa Kuwa Naye Makini Zama Hizi

Rafiki, Zama zimebadilika sana, watu wamekuwa na tabia ambazo huwezi kuziamni. Changamoto ya sasa kila mtu anaweza kuwa rafiki yako na adui yako. watu wanavaa ngozi ya kondoo kujifanya wao ni watu fulani kumbe siyo ili waweze kukutapeli. Katika zama hizi unapaswa kuwa makini kwanza na wewe mwenyewe. ukishakuwa makini kwanza wewe mwenyewe utaepuka kutapeliwa …