Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kabla Hujaenda Kulala Hakikisha Unajivunia Jambo Hili Moja

Rafiki, Hakuna mtu anayeamka na kujua atakwenda kukutana na nini katika siku yake.  Hivyo basi mara nyingi siku inakuwa na mambo mengi, hata kufanikisha kile ulichopanga kufanya ni jambo la kushukuru sana maana kila siku huja na mambo yake ambayo mengine yapo nje ya uwezo wetu. Licha ya changamoto zote za siku, na kama tunavyojua …

Chanzo Cha Matatizo Mengi Ni Hiki Hapa

Tumepewa masikio mawili ili tuweze kusikiliza mara mbili. Angalia katika mwili wako kuna viungo ambavyo umepewa viwili na kingine kimoja. Viungo ambavyo tumepewa viwili hatuvitumii vizuri kabisa lakini vile ambavyo haviko zaidi ya kimoja ndiyo unatakuta tunavitumia vizuri kweli. Kwa mfano, mdomo. Tumepewa mdomo mmoja maana yake tunatakiwa kukaa kimya sana kuliko kuongea lakini ndiyo …

Watu wanasema nini juu yako?

Mpendwa rafiki, Kwa kila binadamu aliyehai basi hakuna ambaye hasemwi kwa namna yoyote ile, kama husemwi basi ujue umeshakufa. Ambaye hana changamito ni yule aliyelala kaburini lakini kama unaishi bado utahusika na mengi. Watu milioni 50 wakisema jambo la kipumbavu bado ni jambo la kipumbavu alisema Anatole France.  Watu wakikusema vibaya kama sivyo ulivyo hata …

Hii Ndiyo Njia Ya Uhakika Ya Kuchelewa

Mpendwa rafiki yangu, Zawadi pekee ambayo tumepewa bure hapa duniani ni muda. Hakuna mtu anayeweza kuongeza hata dakika moja ndani ya masaa haya ishirini na nne. Bila muda hatuwezi kutimiza mipango mizuri tuliyokuwa nayo. Kila mmoja wetu anategemea muda ili aweze kufanya kile anachotaka kufanya. Ni kawaida kwa watu wengi kuchelewa maeneo mengi ya maisha …

Usidharau Kile Ambacho Unacho

Rafiki, Kama unataka kuona umuhimu wa kile ambacho unacho sasa hebu kipoteze au kikose. Tumekuwa ni watu wa kutothamini kile ambacho tunacho, mara nyingi tumekuwa ni watu wa kuchukulia poa vile ambavyo tunavyo. Usichukulie poa kitu chochote ambacho unacho maana siku ukikikosa utaumia sana. Hata kama kuna kitu huwa unakichukulia poa siku usipokiona utaumia sana. …

Kama Unathubutu Kufanya Chochote Tegemea Hili

Sisi binadamu ni kazi inayoendelea, hatusimami kila siku ni kufanya kazi kama vile moyo wa binadamu unavyofanya kazi kila siku. Ukisimama na sisi hatuna maisha maana yake na maisha pia yanasimama. Asili yetu sisi binadamu ni kazi. Ndiyo maana imeandikwa kila mmoja atakula kwa jasho lake, usitegemee utakula kirahisi bila kuumia kidogo. Mambo siyo marahisi, …

Hivi Ndivyo Maisha Yako Yanapofikia Mwisho

Mtu mmoja aliwahi kusema, mwisho wa sura si mwisho wa kitabu. Fungua ukurasa mwingine. Kumbe basi, unaweza ukaona kama umefika mwisho wa maisha kwa sababu labda hujaamua kuendelea na kufungua sura nyingine. Kitabu kina sura nyingi, ya nini kung’ang’ania sura moja? Hata katika maisha yako mengi ya kufanya ambayo yataweza kukuletea mafanikio makubwa sana shida …

Haya Ndiyo Mafanikio Makubwa Unayopaswa Kuwa Nayo

Kila mtu anapenda kufanikiwa na kuhusiana na mafanikio kila mtu anaelewa vile anavyotaka yeye kuelewa. Kuna mwandishi mmoja katika kitabu chake aliandika nani atalia pale utakapokuwa umekufa? Hebu jiulize nani atalia? Ili watu waweze kukulilia unatakiwa ufanye makubwa na mpaka unaona watu wakulilie waache shughuli zao za kila siku na kukulilia wewe ni mpaka uguse …

Jinsi Ya Kulinda Nguvu Zako Na Kuwa Na Uzalishaji Bora

Mpendwa rafiki, Katika zama hizi watu wengi wamevurugwa na mitandao ya kijamii, mwandishi mmoja anasema watu wamekuwa ni kama misukule wa mitandao ya kijamii. Tafiti zinaonesha kuwa kila baada ya dakika kumi au tano mtu lazima ashike simu yake. Kwa namna kama hii unaona ni jinsi gani nguvu zetu zinakwenda sehemu ambayo siyo sahihi. Unakuta …

Haya Ndiyo Maisha Ambayo Hayana Msingi Wa Kuishi

Rafiki, Usiishi tu kama mbuzi, bali ishi kama binadamu mwenye uwezo mkubwa wa akili.  Ishi kwa malengo, unatakiwa kuwa na malengo ya siku, wiki, mwezi na hata mwaka.  Usipokuwa na malengo ya kitu chochote utapoteza siku, muda bila kujua hata muda na siku zimeishaje. Wengi hawajiongozi kwa ratiba tokea wanapoamka asubuhi na mapema bali wanaongozwa …