Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mbinu Bora Itakayokusaidia Kutoka Hapo Ulipo

Vita vikubwa ambavyo tunapaswa kuvitangaza ni vita dhidi ya miili yetu, hakuna upinzani mkubwa tunaopata katika maisha yetu kama upinzani wa miili yetu. Tusipokuwa makini na miili yetu basi tutaishia mahali pabaya sana. Miili yetu inapenda rah asana, inataka kile inachotaka bila sababu yoyote ile. Tukianza kuisikiliza miili yetu hakika hatutoweza kutoboa, hatutoweza kutoka hapa …

Vitu Vitatu Vyenye Uraibu Au Uteja Mkubwa Duniani

Mpendwa rafiki yangu, Kila mtu huwa ana kitu anachopenda hapa duniani, kila mtu ana ulevi wake. Kwa lugha nyingine tunaweza kusema ulevi ni kama uraibu au uteja juu kitu fulani. Huwa tunatengeneza tabia na kisha tabia zinatutengeneza. Tabia ambazo huwa tunazianzisha zinatulea uteja katika maisha yetu. Hebu leo tuende tukajifunze vitu vitatu vyenye uraibu, ulevi …

Usijisumbue Na Mambo Haya

Rafiki, Siyo kila kitu unapaswa kuhangaika nacho, mambo mengine siyo hata ya kujisumbua kabisa. Unatakiwa kuyaacha mambo yatokee kama yalivyopangwa. Hutakiwi kuogopa na kujipa msongo wa mawazo kwa mambo yanayoendelea kutokea kwa sababu ni mambo ambayo huwezi hata kuyazuia. Hutakiwi kujisumbua na mambo ambayo yako nje ya uwezo wako. Bali unatakiwa kujisumbua na mambo ambayo …

Hii Ndiyo Faida Ya Kuwa Mwanafunzi Wa Maisha

  Ili ufanikiwe katika zama hizi hutakiwi kuboboea katika kitu kimoja. Bali unatakiwa kuwa mbobezi wa mambo mbalimbali. Kuchagua kubobea katika kitu kimoja zama hizi ni kama kuchagua kuwa na chanzo kimoja cha mapato ambayo ni hatari zaidi. Hutakiwi kujifungia katika eneo moja, bali kuwa na uwanja mpana, jifunze mambo kwa upana wake na siyo …

Utaweza Kufika Pale Unakotaka Kama Ukianzia Hapa

Sehemu pekee ambayo huwa inaanzia juu na kwenda chini ni kaburi. Kaburi huwa linachimbwa kwa kuanziwa juu na kufika chini. Mara nyingi mtu yeyote anayetaka kuanza kitu kwa kuanzia juu lazima ataanguka vibaya. Chukulia kaburi, linaanzia juu na kuelekea chini hivyo basi, hata biashara unatakiwa kuanzia na siyo juu. Kama unataka kufika mbali basi kubali …

Hiki Ndiyo Kioo Bora Kuliko Vyote Duniani Katika Karne Ya 21

Mpendwa rafiki yangu, Natumaini una kifahamu kioo, Kioo huwa kinatusadia kujiangalia kama tuko sawa au la. Asubuhi kabla hatujaondoka huwa tunajiangali kwenye kioo kama tumevaa nguo zetu vizuri, kama tuna matongotongo, au la. Kioo kinatusaidia kujitathimini namna tulivyo kwa wakati huo. Kama ilivyo watu wengi walivyokuwa rafiki na kioo, hawawezi kuondoka bila kujiangalia kwanza kama …

Mambo Mawili Muhimu Utakayokutana Nayo Siku Hii Ya Leo

Mpendwa rafiki yangu, Hakuna mtu anayeamka na kujua leo akitoka nyumbani atakutana na changamoto gani. Katika maisha tunapaswa kujiandaa kwa lolote, kwa mazuri na mabaya. Kwani haya yote ni sehemu ya maisha yetu. Leo katika shughuli zako,utaweza kukutana na mambo haya mawili muhimu kwako. Nayo ni kama ifuatavyo; Utakutana na ushindi. Lazima katika mipango yako …

Hii Ndiyo Staili Bora Ya Kudai Haki Yako

  Sisi binadamu ni viumbe wa kutegemeana, kila mmoja anamtegemea mwenzake. Na hakuna ambaye anajitosheleza kwa kila kitu. Kumbe basi, tunaweza kusema kuwa kujitegemea siyo kujitosheleza.  Vitu vingi tunavyohitaji viko kwa wengine, hata kama unataka haki ya kitu fulani utaipata kutoka watu wenye mamlaka hiyo. Tunapokuwa tunadai haki zetu kutoka kwa wengine, tunatakiwa kuwa na …

Hii Ndiyo Dawa Ya Mtu Ambaye Hataki Kusikia Kile Unachomwambia

Mpendwa rafiki yangu, Waswahili wanasema kuwa asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Ni kweli kama husikii lile unaloambiwa lazima dunia itakuadhibu. Mtu ambaye hasikii lile analoambiwa na mkuu wake mwisho wake huwa unakuwa ni majuto. Pia, waswahili walisema, asiyefunzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu. Kumbe, kama wewe ni mzazi humfundishi mtoto wako kukaa katika maadili au …

Matatizo Yako Yana Afadhali Kuliko Ya Mwingine

Mpendwa rafiki yangu, Zamani watu wakitaka kujinyonga walikuwa hawajinyongi sehemu yoyote tu, ila walikuwa wanaenda kwenye sehemu maalumu. Sehemu ambayo kuna mazingira rafiki kwa wao kuweza kujinyonga. Mama mmoja alikuwa na watoto wanne, watoto hao wanne walikuwa wanamsumbua sana mama yao.  Watoto walimtesa mama yao hivyo mama yao akajisemea ya nini kujitesa na watoto ni …