Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hakuna Aliyewahi Kushinda Kwenye Huu Mchezo Duniani

Mchezo mwenyewe ni mchezo wa kufurahisha watu wengine. Hakuna aliyeshinda mchezo wa kuwafurahisha watu kwa sababu ni kazi ngumu duniani ambayo hakuna aliyowahi kufanya akafanikiwa. Kwa jambo lolote utakalofanya ili uwafurahishe watu basi umejiandaa kushindwa kabla hata ya kuanza mashindano yenyewe. Mtu pekee ambaye unaweza kumfurahisha kwenye haya maisha ni wewe mwenyewe.Huwezi kuwa sawa na …

Jinsi Ya Kuwa Na Maisha Tulivu

Katika jamii yetu ya sasa iko njia nzuri sana ya wewe kuwa na maisha ya utulivu, huna haja ya kujisumbua na watu wakati kiasili tayari maisha yanakusumbua halafu tena mtu aje akusumbue, utahangaika na vingapi? Watu wamekuwa ni watu wa kukimbizana na mambo ambacho yako nje ya uwezo wao wakifikiri watayaweza. Wako ambao wanakazana kutaka …

Hiki Ndicho Kitu Kinachoathiri Maisha Yako

Maisha yetu yameathiriwa na kitu kimoja kikuu nacho ni maamuzi. Maamuzi tunayofanya kila siku ndiyo yanayoweza kuathiri maisha yetu kwa kiasi kikubwa. Je ni nini kilichokufanya uwe hapo ulipo leo? Bila shaka ni maamuzi ambayo tayari ulishayafanya huko nyuma. Kinachowafanya watu wasiendelee au kuendelea basi eneo linalowasumbua ni maamuzi tu na wala siyo kitu kingine. …

Hivi Ndivyo Vitu Saba Unavyopaswa Kuvilinda Kwenye Karne Hii 21

Viko vitu vingi sana ambavyo tunapaswa kuvilinda katika maisha yetu. kazi yetu kubwa katika maisha yetu ni kutengeneza, kukuza na kisha kukitunza. Haifai kutengeneza na kisha kuacha, hapana unapswa kutunza na kukuza kile ambacho umekianzisha au kukitengeneza ndani yako. Leo nakwenda kukushirikisha vitu saba unavyopaswa kuvilinda kwenye maisha yako na vitu hivyo ni kama ifuatavyo; …

Hizi Ndizo Aina Mbili Za Kupoteza Nguvu

Kama tunavyojua ili ufanikiwe kitu chochote unahitaji nguvu. Nguvu ni rasilimali muhimu sana ambayo itusukuma kwenye kile tunachotaka katika maisha yetu. Kuna wakati unaweza kuwa na muda lakini huna nguvu za kufanya kazi. Kumbe basi, nguvu ni kitu cha kutumia mapema wakati ukiwa na nguvu. Kama wewe ni kijana basi una fursa sasa ya kutumia …

Jinsi Ya Kutumia Utani Ili Kukuzuia Usipate Hasira Na Kutumia Nafasi Yako Vibaya

Binadamu sisi  ni viumbe wa hisia, hivyo vitu kama hasira ni kitu cha kawaida sana. Na wako ambao wanatumia nafasi zao vibaya kwa sababu ya kuwa na chuki na mtu fulani sasa ikitokea mtu huyo ni kiongozi anatumia nguvu yake ya uongozi kumuumiza yule wa chini yake. Katika falsafa ya ustoa tunaalikwa kujiandaa na lolote …

Ogopa Kuwa Mtu Wa Namna Hii Kwenye Maisha Yako

Mpendwa rafiki yangu, Matokeo yoyote unayopata sasa kwa asilimia kubwa ni wewe mwenyewe umechagua kuwa nayo. Wewe ndiyo mchangiaji mkubwa wa kila kitu katika maisha yako. Kwa kuwa wewe ndiyo mkurugenzi wa maisha yako hivyo unatakiwa kuwajibika na maisha yako kwani hakuna anayekosa usingizi kwa sababu ya maisha yako. Kwenye maisha yako unatakiwa kuepuka kuwa …

Mambo 13 Unayopaswa Kuyajua Kabla Ya Kufika Miaka 30( Sehemu Ya Pili)

Rafiki, kama nilivyokueleza jana leo tutaendelea na sehemu ya pili ya yale mambo 13 , ambapo jana tuliweza kujifunza mambo sita leo hii tutamalizia yale saba yaliyobakia. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala ya jana ambayo ndiyo ilikuwa sehemu ya kwanza basi nakusihi usome hapa Namba saba, unatakiwa kuweka bajeti; vijana wengi na watu wengi …

Mambo 13 Unayopaswa Kuyajua Kabla Ya Kufika Miaka 30

Mpendwa rafiki yangu, Mtu yeyote ambaye hana mwelekeo basi mwelekeo wowote humchukua, mtu mwa namna hii anakuwa hana tofauti na bendera. Mahali ambapo upepo unakwenda naye anaenda, usiwe mtu wa kuishi bila misingi sahihi ya maisha. Leo nakwenda kukushirikisha mambo 13 ambayo kila kijana anapaswa kuyajua na mambo hayo ni kama ifuatavyo. Kuwa na marafiki …

Jinsi Ya Kukabiliana Na Mtu Asiyejielewa

Rafiki, Siyo kila mtu unayekutana naye anajielewa na kujitambua. Tunakutana na watu wa aina mbalimbali kuna wengine wana hekima na kuna wengine hawana kabisa hekima wala busara. Kuishi na watu ni kazi sana kwa sababu kila mtu ana mitazamo yake. Ukitaka kuishi vile watu wanavyotaka hapo utakua unaishi maisha ya kuwafurahisha watu ambayo ni kazi …