Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kwenye Kila Ushindi Unaoujua Wewe Kuna Kitu Hiki Cha Kujifunza

Mpendwa Rafiki yangu, Mpaka tunaona kazi yoyote imekamilika basi jua kuwa kuna mchakato mkubwa umefanyika. Mafanikio yoyote uliyopata au unayotegemea kuyapata yana mchakato wake. Watu wengi wanapenda kufurahia mafanikio lakini hawapendi kusikia mchakato wa mafanikio. Sasa kwenye kila ushindi wowote ule unaoujua wewe kuna kitu muhimu sana cha kujifunza. Kitu hiko siyo kingine bali ni …

Sala Bora Ya Kuondoa Uvivu Duniani

Uvivu umekuwa ni tatizo kubwa miongoni mwa watu wengi. Watu wamekuwa wanaendesha maisha yao kwa mazoea sana. Utamaduni wa uvivu huwa unazaa walalamikaji wengi, watu wasipotambua kuwa jukumu la maisha yao ni lao wenyewe watakua wanawalaumu watu wengine kwa wao kuwa hivyo walivyo leo. Uvivu ndiyo adui mkubwa wa binadamu, watu wanashindwa kuwa na maisha …

Leo Acha Kufanya Yote Na Ikumbuke Siku Hii Muhimu Kwako

Mpendwa rafiki yangu, Kila mtu ana siku yake muhimu katika maisha yake, wengine huwa wanakumbuka siku zao za kuzaliwa, hivyo wanasherekea kwa namna yao wenyewe. Katika makala hii ya leo ninataka ukumbuke siku hii moja muhimu katika maisha yako, na kama kila mmoja wetu akiikumba vizuri na kuitumia hamasa hiyo kwenye kile anachofanya lazima atafanikiwa. …

Jinsi Ya Kufanya Mambo Yasiyowezekana

Mpendwa rafiki yangu, Hakuna jambo au neno gumu lisilowekana hapa duniani. Kama limeshindikana kwako basi kwa mwingine linawezekana. Hakuna mtu ambaye anapewa jambo ambalo hawezi kulikabili. Yale yote unayokutana nayo jua yako ndani ya uwezo ndiyo maana umepewa. Unaweza kusema wewe huwezi lakini watu wengine wanaweza, kama kitu hujui chukua kama changamoto ya kujifunza ili …

Usiogope Kujaribu, Jaribu Halafu Iachie Sehemu Hii Ifanye Kazi Yake

Watu wengi wanaogopa kujaribu sana, na hili linawafanya watu wengi kuendelea kubaki pale walipo. Kama hujaribu kitu utawezaje sasa kuwa na maisha bora? Utakuwa kila siku ni mtu yuyule kama hutoamua kuchukua hatua za kujaribu. Kujaribu siyo kushindwa unapojaribu kitu ndiyo unajifunza. Wako ambao wanataka kuanzisha biashara lakini wanaogopa kuna kitu kinawazuia kuanza nacho ni …

Maisha Mazuri Yanaanza Na Kitu Hiki

Mpendwa rafiki yangu, Je unataka kuwa na maisha mazuri? Kama jibu lako ni ndiyo basi hii makala inakuhusu. Kuna mtu kati yetu kila siku anaamka na kuweka mipango ya kuwa na maisha ya hovyo? Kila mtu anaamka akiwa anataka awe na maisha mazuri. Kila mtu anaweka juhudi ili awe bora, kama kuna mtu anaweka juhudi …

Maswali Saba Yatakayokuwezesha Kupata Chochote Kile Unachotaka

Rafiki, Wako ambao mpaka sasa maisha yao hawayaelewi hata jinsi yanavyokwenda, wengine ndiyo wameshakata tamaa na kuona ndiyo wamefikia mwisho wa ndoto zao. Umeshakimbizana na kila aina ya fursa, kila kinachokuja mbele yako unakimbizana nacho na matokeo yake muda unaenda unaona huna ulichofanya. Unajua katika maisha yako kama hujui nini unataka haswa huwezi kufanikiwa. Mtu …

Hiki Ndicho Kinachotokea Katikati Ya Kila Mradi

Mpendwa rafiki, Hakuna kitu ambacho unaweza kufanya hapa duniani ukakosa upinzani. Kwa sheria za asili zenyewe kadiri ya  mwanasayansi newton kitu chochote kinachokwenda mbele lazima kiwe na ukinzani wa kuvutwa chini, hebu rusha jiwe juu utashangaa linavutwa chini haraka hii ni nguvu ya uvutano. Mara nyingi wale watu wetu wa karibu wanaweza kuwa chachu ya …

Kila Siku Jifunze Kuwa Na Hiki

Mpendwa rafiki yangu, Karibu matatizo mengi yanayosababishwa na watu mengi yanaanzia kwenye midomo yetu. Midomo yetu inachangia kufanya matatizo mengi kuibuka. Hakuna mtu ambaye anaweza kwenda kugombana na mtu ambaye ni bubu eti kwa sababu amemsema vibaya. Huwezi kuangaika na bubu kwa sababu unajua bubu haongei  lakini sisi tunaoongea tunaua watu wengi kwa ndimi zetu. …

Ukicheza Namba Hii Lazima Utafanikiwa

Mpendwa rafiki, Katika mchezo wa mpira wa miguu na hata michezo mingine kila mtu ana cheza namba yake uwanjani. Kila mtu anaingia uwanjani huku akijua anakwenda kufanya nini. Kila namba ina majukumu yake uwanjani.  Na ikitokea mtu anacheza namba siyo yake anaacha namba yake lazima italeta madhara. Kwa mfano, golikipa atoke namba moja akacheze nafasi …