Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mapinduzi Huwa Hayaletwi Kwa Kukumbatia Kilichopo

Ukienda sehemu yoyote ile kuna mazoea ambayo tayari yameshajengeka kwenye eneo hilo na wanayachukulia kama ukweli na kiwango chao ambacho kila mtu anapimwa nacho. Ukienda wewe na ukafanya kwa utofauti utaletewa upinzani na kuonekana kama ni adui unafanya vitu ambavyo uliowakuta walikuwa hawafanyi. Utaweza kuulizwa hata yale unayofanya, unayafanya kwa mamlaka au amri ya nani? …

Kitu Ambacho Watu Wengi Wanakisubiria Kwenye Maisha Yao

Kwenye haya maisha utachelewa kufika kule unakotaka kwenda kama ukisuburia kupewa ruhusa ya kufanya kile unachotaka kufanya. Watu wengi wanakaa huku wakisubiria mtu fulani aje awape ruhusa ya kufanya kile wanachotaka kufanya. Dunia haiko hivyo, ukitaka kupata kile unachotaka, usisubiri kupewa ruhusa, jiruhusu mwenyewe kuingia kwenye kile unachotaka kufanya. Watu wengi waliofanya makubwa hawakusubiri ruhusa …

Siri Ya Kushinda Mchezo Wowote Ule

Watu huwa wanafikiria mambo ni marahisi sana, mambo siyo marahisi ndiyo maana watu wengi hawafanyi na hawajapata kile wanachotaka. Ukiangalia ndani ya mwaka huu biashara zilizoanzishwa ni nyingi, na tafiti za biashara zinasikitisha sana. Kati ya biashara kumi zilizoanzishwa mwaka huu zinazokua ni mbili au moja. Na ukitaka kuliona hilo angalia mtaani wangapi walianza biashara …

Kwenye Maisha Yako, Hakikisha Unakuwa Na Kitu Hiki

Hakikisha unakuwa na viwango vya juu. Yaani kwenye kila eneo la maisha yako jiwekee viwango vya juu. Ukishajiwekea viwango vya juu kabisa usikubali chochote chini ya viwango vyako. Kwenye maisha huwa unapata kile unachokubali na siyo kile unachostahili. Jiwekee viwango vya juu kabisa vya ufanyaji na hakikisha unajisukuma kila wakati kuvifikia viwango hivyo. Kwa sababu …

Hatua Ya Kuchukua Pale Unaposhindwa Kitu

Kaa pembeni na waachie wale wanaoweza kufanya wafanye. Ukiona umeshindwa kitu, siyo kwamba kila mtu ameshindwa. Wako ambao wanaona kitu fulani ni kigumu na kwa sababu wao wameshindwa wanaona wote wanaweza kushindwa pia. Kama wewe ni kiongozi sehemu fulani na unaona kabisa uwezo wako umefikia kikomo kaa pembeni waachie wengine. Unapotoa nafasi kwa wengine wanaweza …

Vitu Viwili Unavyopaswa Kuwa Navyo Ili Ufanikiwe

Siyo kwamba watu hawajui kile wanachopaswa kufanya, ila watu hawana ujasiri wa kufanya kile wanachopaswa kufanya. Kama kila mtu angekuwa na ujasiri wa kusimamia malengo yake basi tungezidi kuiona dunia inazidi kuwa sehemu salama ya kuishi kwa kila mmoja wetu. Ili ufanikiwe kwenye kitu chochote kile kuwa na vitu hivi viwili. Moja, maamuzi. Kama huendi …

Pampu Mpaka Maji Yatoke

Ukiwa kwenye kisima cha kupampu, ukipampu mara moja maji hayawezi kuja juu, ila ukipampu mara nyingi maji yatakuja juu. Na ukipampu na kuishia njiani bila kuona maji kama yale maji yalikuwa karibu kutoka yote yatarudi chini. Ukija kuanza tena utaanza upya. Katika maisha unapaswa kuwa na msimamo. Uwe na nguvu ya ung’ang’anizi. Kuwa na ung’ang’anizi …

Njia Rahisi Ya Kubadili Fikra Zako

Mwanasaikolojia mmoja amewahi kusema ni rahisi kubadili fikra zako kwa kuchukua hatua kuliko kubadili hatua zako kwa kufikiri. Huwa tunataka kubadili maisha yetu kwa kufikiri kumbe siyo sawa. Unapochukua hatua unakuwa siyo yule wa mwanzo tena. Kwa mfano, unasema unataka kuanza biashara kila siku na huanzi, unalalamika mtaji unakusumbua ambao ndiyo umekuwa wimbo wa watu …

Kuna Mtu Anakutegemea, Endelea Kufanya

Kila mmoja wetu ana upekee wake. Hata mtu akufananishe na mtu mwingine bado utabaki kuwa wewe. Tena watasema uko kama fulani lakini siyo. Ndiyo maana katika maisha yako, furahia kuwa wewe maana kila mtu ana hadithi yake ambayo mtu mwingine hana. Endelea kuishi vile unavyoishi, endelea kufanya yale unayofanya kwa sababu kuna watu wananufaika na …

Unapoendelea Na Mapambano Dunia Itakupatia Hiki

Kitu ambacho hatupaswi kufanya katika maisha yetu ni kukata tamaa. Usiharibu maisha yako ya kesho kwa sababu ya hali unayopitia sasa. Hali uliyonayo sasa haitoweza kudumu milele, bali ni ya muda tu. Watu wote waliowahi kufanikiwa duniani hawajawahi kukata tamaa, leo hii hata mimi binafsi ningekata tamaa katika kazi yangu ya uandishi huenda hata usingenijua. …