Design a site like this with WordPress.com
Get started

Watu ni Wazuri Sana Kwenye Kitu Hiki

Watu ni wazuri sana kwenye sababu. Waulize watu kwanini hawajafanya au kwanini maisha yao yako hivyo walivyo watakupa sababu. Ukiwapa watu majukumu fulani usipowapa namba ya kuifikia lazima watakupa sababu. Na nimekuja kugundua sababu hizi tunazojipa ni sababu za uvivu na uzembe. Yaani sababu ndiyo imekuwa kificho cha watu wengi ambao hawataki kuchukua hatua kwenye …

Kama Hupati Matokeo Kuna Kitu Hukifanyi

Hakuna watu ambao wana maigizo mengi kama binadamu. Ni wazuri wa kutengeneza sababu za kile ambacho wao wanaona zitawalinda. Na kama mtu kitu ana kitaka kweli atakifanya na matokeo yataonekana. Na kama mtu kitu hakitaki hatokifanya na ataanza kutafuta sababu. Maisha ni kuuza kile unachokiamini, sasa kama wewe unajidanganya kwa sababu unafikiri utapata matokeo gani? …

Umejitoa Kwa Lipi Haswa?

Utaishia kupata matokeo ya kawaida kama hujajitoa haswa kupata kile unachotaka. Binadamu ni watu wazuri sana kufanya pale wanapokuwa wanasimamiwa au wanapokuwa wamepewa namba au lengo la kufanyia kazi. Unaweza ukajiona umefikia ukomo na ukaweka nukta lakini nakuhakikishia ukiweza kujisukuma na ukapata mtu anayekusimamia utashangaa pale ulipoweka nukta panabadilika na kuwa mkato. Usiishi bila kuwa …

Tengeneza Maoni Yatakayokupa Hamasa Binafsi

Yapo maoni mengi ambayo huwa tunajitengenezea kwenye fikra zetu. Yapo maoni ambayo tunajipa sisi wenyewe na yapo maoni ambayo yanajitengenezea kwenye fikra zetu. Wako ambao wanajipa maoni chanya na wako ambao wanajipa maoni hasi. Maoni yanayotengenezwa kwenye fikra zetu yana mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yetu kimaisha. Kujitengenezea maoni ni hamasa binafsi. Vile unavyofikiri upo …

Kitu Kinachomfanya Mtu Achukue Hatua Haraka

Huwa tunalalamika kwanini watu wengine tukiwaambia wafanye kitu fulani hawachukui hatua.Siyo tu watu wengine, wakati mwingine hata sisi wenyewe tunakuwa ni wagumu kuchukua hatua. Unafikiri ni kwanini watu wanakuwa wagumu kuchukua hatua? Kwa sababu hujagusa maslahi yao binafsi. Kitu kinachomsukuma mtu kuchukua hatua haraka ni maslahi. Mtu anakuwa ana hamasika kuchukua hatua pale anapokuwa anaona …

Usiangalie Maumivu Unayopitia Bali Angalia Hiki Hapa

Jiunge na Klabu ya Mimi Ni Mshindi Nimezaliwa Kushinda ili upate maarifa sahihi yatakayokuwezesha kupiga hatua kwenye kile unachofanya. Kiasili sisi binadamu ni watu wa kukata tamaa, kuchoka, kuahirisha mambo. Pale mambo yanapokwenda kinyume na sisi tunaruhusu hali za kushindwa. Watu huwa hawapendi kujitesa, hata katika kazi mtu akiona kazi au kile anachofanya kinamchosha anaamua …

Dunia Itafanya Njama Na Wewe

Pale unapojitoa kweli kupata kile unachotaka kwenye maisha yako, dunia inakuwa inafanya njama na wewe kuhakikisha unapata kweli kile unachotaka kwenye maisha yako. Jitoe sana kwenye kile unachotaka hata kama hujui utapateje lakini wewe amini, nia yako na uthubutu wako utaifanya dunia kufanya njama na wewe upate kile unachotaka. Amini kweli, kila kitu kinawezekana kama …

Kila Mtu Anakwenda Kujua Jina Langu

Maisha bila hamasa hayawezi kwenda vizuri sana. Kwa sababu sisi ni binadamu tunapaswa kupata hamasa ili tuweze kujisukuma kufanya kile tunachopaswa kufanya bila kukata tamaa. Kwa kuwa mimi ni Muuza Hamasa, Afisa Mhamasishaji Mkuu CIO (Chief Inspiration Officer na kwenda kukuuzia hamasa ambayo itafanya kila mtu ajue jina lako kupitia kile unachofanya. Kwenye maisha kila …

Usiishi Bila Kuwa Na “Target”

Kwenye kila eneo la maisha yako unapaswa kuishi kwa “target”. Jiwekee target, kwanini ujiwekee target? Kwa sababu tageti inakusaidia kukusukuma na kukuwajibisha ili ufikie malengo yako. Kwenye kazi jiwekee ufikie tageti fulani yaani lengo fulani ufikie. Kwenye eneo la kifedha, jiwekee tageti kwamba kwa mwezi unapaswa kuingiza kipato kiasi fulani. Na ukishaweka tageti pambania kufikia …

Kuwa Mtu Wa Namna Hii Kama Unataka Kupiga Hatua Kubwa

Iko kauli moja ambayo nimejifunza hivi karibuni inayosema, ni rahisi kuyavumilia maisha magumu kuliko kupambana kupata maisha bora. Unapata nini kwenye kauli hiyo? Hapo anamaanisha kwamba, ni kazi zaidi kupambana kupata maisha bora kuliko kuvumilia maisha magumu. Hii iko wazi kabisa kwenye maisha, angalia watu wengi wana maisha magumu na hakuna hatua za tofauti wanazochukua …