Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usiwe Na Wasiwasi Na Kitu Hiki Hapa

Kabla hatujafanya kitu chochote kile, ndani ya nafsi zetu huwa kuna sauti tunazisikia. Wakati mwingine nafsi zetu zinatuambia hapa tunaweza au hatuwezi. Kinachowazuia wengi kufanikiwa ni kuwa na wasiwasi juu ya nafsi zao wenyewe.Mtu anataka ushindi wa kitu fulani, lakini hajiamini kabisa kama atashinda, kimdomo anasema anataka kitu fulani lakini nafsi haimaanishi. Kwa sababu walijaribu …

Kitu Pekee Kitakachokuwezesha Kuendelea Mbele

Kuna wakati unachoka na unaona ni sahihi kwako kuishia hapo ulipofika. Safari  ya  kupata  kile  unachotaka  kwenye  maisha  yako  haitakuwa  rahisi,  dunia haitakuachia  kirahisi ufanye  kila  unachotaka.  Utakutana  na  vikwazo,  changamoto  na magumu mbalimbali.  Kuna  wakati utajiona  kama  umekosea  kila  ulichokuwa  unafanya. Utafikia  hatua  ya  kukata  tamaa  na  kuona  haina  haja  ya  kuendelea  tena. Kitu  …

Chukua Karatasi Yako Na Weka Sahihi Yako

Leo nataka kukuonesha ni kwa jinsi gani wewe uko tofauti na wengine na wakati mwingine nakushagaa pale unapotaka kuwa kama wengine badala ya kuwa kama wewe. Pata picha unachukua kalamu na karatasi yako halafu unaandika saini yako. Kisha angalia saini yako inafanana na ya mtu mwingine yeyote hapa duniani? Utajisikiaje kama hakuna mtu ambaye ana …

Hakuna Mtazamo Wa Hovyo Duniani Kama Huu

Kwenye kitabu chake jinsi ya kuuza chochote mwandishi Joe Girard anatuambia hakuna mtazamo wa hovyo duniani kama kuamini kwamba kitu hakiwezi kufanyika kwa sababu hakijawahi kufanywa. Mtazamo huo ndiyo umewafanya wengi kushindwa kupiga hatua, kwa kuendelea na mazoea. Hata kama hakuna mtu mwingine amewahi kufanya kitu fulani, kama umeona ndiyo unapaswa kukifanya ili kupata matokeo …

Usiwe Na Wasiwasi

Mara nyingi kinachowazuia watu kufanya maamuzi kwenye maisha yao ni wasiwasi wanaokuwa nao juu ya kitu fulani. Kitendo cha watu kuwa na wasiwasi, kinawafanya wasifanye maamuzi kwa kuona bado hawajawa na uhakika wa kutosha. Rafiki yangu, niko hapa kukuondoa wasiwasi, usiwe na wasiwasi juu ya kitu fulani unachotaka kuanza kwenye maisha yako. Usiwe na wasiwasi …

Kila Wakati Kuwa Na Kitu Hiki

Kuwa na kitu cha kufanyia kazi. Kila wakati kuwa na namba ambayo unapaswa kuifanyia kazi. Usikubali kuwa na maisha ambayo unakuwa na muda halafu huna kitu cha kufanyia kazi. Kila wakati jipe kazi, jipe jukumu moja la kufanyia kazi na ukilimaliza jipe jukumu lingine tena. Hakuna kupoa, ni kazi kazi. Siyo kwamba usiwe na muda …

Usiogope Kukosea Pale Unapochagua Kufanya Kitu Hiki

Usiogope kukosea pale unapochagua kufanya maamuzi. Ni bora ufanye maamuzi ukosee kuliko kutokufanya maamuzi. Kwa sababu utarekebisha makosa yako kuliko kutokufanya maamuzi kabisa. Sijui kwa nini watu wanaogopa kufanya maamuzi, usipofanya maamuzi maana utaendelea kubaki na kile unachokiamini lakini ukifanya maamuzi itakusaidia kupata kitu kipya. Maamuzi ndiyo yanaleta mafanikio makubwa kwenye kila eneo la maisha …

Jifunze Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Hakuna kitu ambacho binadamu wanapenda kwenye maisha yako kama kuthaminiwa. Hali ya mtu kuonekana ni wa muhimu au wa thamani inawafanya watu wajisikie vizuri sana. Sisi binadamu ni viumbe vya hisia, hakuna kiumbe ambaye hapendi kusifiwa, kila mtu anapofanya kitu kizuri, anakuwa anahitaji kupongezwa au kusifiwa. Wakati mwingine watu wanavunjika moyo hata wa kufanya kazi …

Ingekuwa Wewe Ungefanya Nini?

Kiasili sisi binadamu ni wavivu, ni viumbe ambavyo tunapenda kusukumwa kufanya vitu. Ni watu wachache sana ambao wana nidhamu binafsi ambao wanaweza kupanga kitu na kufanyia kazi. Kupanga ni rahisi sana ndiyo maana kila mtu anapanga lakini kufanya imekuwa ni kipengele kingine. Tunao watu wa mfano ambao wanafanya makubwa sasa unapaswa kuwatumia kama watu wako …

Sifa Inayolipa Sana Duniani

Mwandishi mmoja wa kitabu cha How I Raised Myself From Failures to Success in Selling alikuwa ni mchezaji wa kikapu, alikuwa anachezea timu moja huko Marekani. Siku moja kocha wake wa timu ya kikapu akamwita, akamwambia tumeamua kukufukuza katika timu yetu ya kikapu. Frank akauliza, ni kwa sababu gani mmeamua kunifukuza kazi? Kocha wake akamjibu …