Design a site like this with WordPress.com
Get started

Njia Nzuri Ya Kumbadilisha Mwenza Wako

Mara nyingi sisi binadamu huwa tunapenda kujipa kazi kubwa ya kuwa viranja wa dunia. Ni kazi ambayo iko nje ya uwezo wetu kwa sababu hakuna hata anayeiweza kuifanya. Huwa tunatumia nguvu kubwa kutaka kuwabadilisha watu wawe kama vile tunavyotaka sisi kwa mara moja kitu ambacho hakiwezekani. Mabadiliko yanawezekana kwa mwenza wako lakini siyo kwa haraka …

Muulize Mpenzi Wako Swali Hili

Kwa kila mwanandoa huwa shabaha yake kuu ni kutaka kuona ndoa yake ina mafanikio makubwa. Yaani yale mazuri ambayo kila mmoja wetu anayo, tukiyachanganya kwa pamoja tunakua na maisha bora sana ya ndoa. Kinachowaumiza wanandoa wengi katika zama hizi za taarifa ni ubinafsi. Ubinafsi ni shetani anayekula ndoa nyingi. Ninashangaa kuona watu wanasema wamekuwa mwili …

Watu Huwa Hawapendi Watu Wa Namna Hii

Unapofanya kitu chochote kile, hakikisha kinatoka ndani ya moyo wako, kwa sababu watu huwa hawapendi watu wanafiki kabisa. Kama unajali, hakikisha unajali kweli na inatoka moyoni na siyo kufanya hivyo kwa unafiki ili kupata kitu fulani. Kama unamsifia mtu msifie mtu kweli inayotoka moyoni na siyo kumsifia kiunafiki ili uweze kukubaliana naye juu ya kitu …

Kabla Hujakosoa Jiulize Swali Hili

Ni kawaida yetu sisi binadamu kupenda kukosoa zaidi kuliko kupongeza. Wako watu ambao wanapenda kuona mabaya tu pale mtu anapokuwa amejaribu kufanya kitu. Badala ya kupongeza yeye atakosoa kwa nini isiwe hivi. Ukitaka kujenga mahusiano yako, usiwe mtu wa kukosoa bali kuwa mtu wa kupongeza. Ukishamkosoa mtu tayari hamtaweza kukubaliana kwenye jambo lolote lile. Katika …

Mambo Ya Kuepuka Kukumbushiana Na Mwenza Wako Wa Ndoa

Hakuna mtu aliyekamilika kwenye kila eneo la maisha yake. Binadamu tuna asili ya udhaifu. Na kila mmoja wetu anakua kadiri ya mtazamo anaokutana nao kwenye jamii yake aliyokulia. Kawaida wanandoa wengi huwa wanaingia kwenye ndoa tayari wakiwa wakubwa hivyo kila mtu anakuwa na tabia zake. Na kazi inaanza pale wawili hao wanapoanza kuishi pamoja. Kwa …

Huu Ndiyo Ujinga Ambao Wanandoa Wanapaswa Kuuacha Mara Moja

Ujinga ni nini? Ni kufanya kitu kile kile kwa mtindo ule ule halafu unategemea kupata matokeo tofauti hii ni kadiri ya mwanasayansi Albert Einstein aliwahi kunukuliwa akisema enzi za uhai wake. Huwezi kuwa na ndoa bora kama kila siku unafanya mambo yale yale yanayochangia ndoa yako kutokua vizuri. Ili mahusiano yako yaweze kukua inakupasa na …

Wape Watu Kitu Hiki Utajua Kile Wanachopitia

Wape watu muda na utajua kile wanachopitia. Watu wanaweza kupitia mengi lakini huwezi kujua kile wanachopitia mpaka pale utakapowapa muda. Muda ni rasilimali muhimu sana ambayo huwa inatibu mengi kwenye maisha yetu. Ukimpa mtu muda atafurahia na atahisi una mthamini na atakua tayari kukuambia kile anachopitia. Watu wanaweza kuwa na mengi ya kukuambia lakini hawawezi …

Kama Unataka Watu Wakukwepe Na Kukudharau Usiwe Hivi

Sisi binadamu ni viumbe vya hisia. Ukiwa ni mtu wa kujijali sana wewe mwenyewe bila kujali wengine watu watakuona wewe ni mbinafsi na itakuwa ngumu wewe kufanya jambo lako halafu wakubaliane na wewe. Kama unataka watu wakukwepe na kukudharau usiwe msikilizaji mzuri. Njia rahisi ya kuwashawishi watu wakubaliane na wewe ni kuwa msikilizaji mzuri na …

Aibu Yako, Aibu Yake

Jambo lolote la aibu ukimfanyia mwenzako jua aibu hiyo ni ya wote. Aibu yake, aibu yako. Kwa mfano; mwanandoa ukifanya kitendo cha kumfedhehesha mke au mume wako utakuwa mmejitia aibu wote na kufedheshana. Kiasili sisi binadamu ni viumbe vya hisia. Ukimfanyia mwenzako ubaya ule ubaya utakurudia na yale majuto yatakutesa. Falsafa ya karma inasema, chochote …