Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndicho Kinachotokea Pale Mtu Anapoweka Kipaumbele Kwenye Kazi Tu

Jana tulijifunza madhara ya kufanya kazi bila kuwa na mapumziko. Na tuliona ni kwa namna gani mwili wa binadamu unavyohitaji mapumziko. Kwenye maisha lazima uwe na mlinganyo sawa,ukisema unaweka kazi tu mambo mengine yataharibika. Kwa kuweka kipaumbele mbele kikubwa kwenye kazi tu , utayapuuza maeneo mengine ya maisha yako ambayo yanakuwa dhaifu na kuathiri maisha …

Ujumbe Muhimu Wa Leo Kuhusu Mahusiano Yako

Rafiki yangu, Shabaha yangu ya leo ni kutaka kukuambia kuwa furahia kuwaona watu. Kwa nini ?Kwa sababu, tunaishi kwenye zama za ajabu sana. Watu wanaweka umakini wao kwenye teknolojia kuliko kwenye watu halisi. Ni kawaida kwa sasa kuwakuta watu wakiwa pamoja lakini kila mtu akiwa anaangalia simu yake. Tunaipa simu umakini kuliko hata watu halisi. …

Usilazimishe Matatizo Haya Kwenye Mahusiano Yako

Kila mtu anajua wazi kwamba kuna vitu akivifanya katika mahusiano ya mke na mume basi vinakwenda kuharibu amani ya ndoa. Na watu wanalijua hilo lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kukubali kusukumwa na hisia za hasira ndani yake. Kwa mfano, kuna baadhi ya makosa ambayo mwenza wako akikufanyia unaweza ukayapuuzia kwanza na ukaja kuongea …

Jambo Muhimu La Kuzingatia Katika Maisha Ya Wanandoa

Nilipokuwa nasoma kitabu The Prohet kilichoandikwa na Khalil Gibran nilikutana na sentensi moja ambayo nimependa kukushirikisha siku hii ya leo, katika shairi hilo kuna mahali mwandishi anawashauri Wanandoa kuwa imbeni na kucheza pamoja kwa furaha lakini kila mmoja awe na wakati wa peke yake. Ni kweli, maisha ya ndoa yanahitaji muda mwingine uwe na wakati …

Hiki Ndicho Kitu Ambacho Watu Wengi Wanakitoa Kwa Wengine

Mara nyingi watu huwa wanauza kile walichonacho kwa lugha rahisi tunaweza kusema watu wanajaribu kutoa kile ambacho tayari kipo ndani yao. Usiumie na wale wanaokufanyia mabaya badala yake waonee huruma. Kwa sababu watu wanatoa kile ambacho kipo ndani yao. Kwa mfano, ukiona mtu anakupa upendo jua upendo ndiyo upo ndani yake. Ukiona anakuuzia chuki jua …

Njia Mbili Unazoweza Kuzitumia Kama Huoni Mchango Wako Kwenye Tatizo Lolote Ambalo Upo

Ni kawaida na tabia ya binadamu kupenda kujipendelea. Pale wewe unapofanya kosa ni rahisi kujipa sababu nzuri kwanini umefanya kosa hilo. Kwa sababu sisi binadamu ni wagumu kukubali kwamba na sisi tumechangia kutokea kwa matatizo ambayo tunayo. Matatizo mengine huwa yanatokea huenda labda ulikuwa umechoka au ulipitiwa au hukuwa na taarifa za kutosha. Lakini, inapotokea …

Hili Ndilo Sharti Namba Moja La Msamaha

Watu wanakosea namna ya kuombana msamaha hii inawasababisha watu kubaki na manung’uniko, chuki na hasira ndani ya mioyo yao. Kusema naomba msamaha peke yake, bado hujamaliza kiu ya yule uliyemkosea. Kila anayeombwa msamaha kuna sauti ambayo anataka kuisikia kutoka kwa yule aliyemkosea. Kwenye mahusiano yetu migogoro haiishi kwa sababu ya namna watu wanavyoombana msamaha. Mtu …

Sababu Kuu Moja Kwa Nini Umchukulie Kila Mtu Kwa Heshima

Sisi ni binadamu na maisha yetu kwa asilimia kubwa yanawategemea wengine. Kile ambayo tunahangaika kukitafuta tayari kipo kwa wengine. Mafanikio yote tunayotaka tunapata kwa watu wengine. Hivyo basi watu ni rasilimali muhimu sana.Mchukulie kila mtu unayekutana naye kwa adabu na heshima kwa sababu huwezi kujua ni wakati gani utamwitaji sana kwenye maisha yako. Kila mtu …

Njia Nzuri Ya Kumbadilisha Mwenza Wako

Mara nyingi sisi binadamu huwa tunapenda kujipa kazi kubwa ya kuwa viranja wa dunia. Ni kazi ambayo iko nje ya uwezo wetu kwa sababu hakuna hata anayeiweza kuifanya. Huwa tunatumia nguvu kubwa kutaka kuwabadilisha watu wawe kama vile tunavyotaka sisi kwa mara moja kitu ambacho hakiwezekani. Mabadiliko yanawezekana kwa mwenza wako lakini siyo kwa haraka …

Muulize Mpenzi Wako Swali Hili

Kwa kila mwanandoa huwa shabaha yake kuu ni kutaka kuona ndoa yake ina mafanikio makubwa. Yaani yale mazuri ambayo kila mmoja wetu anayo, tukiyachanganya kwa pamoja tunakua na maisha bora sana ya ndoa. Kinachowaumiza wanandoa wengi katika zama hizi za taarifa ni ubinafsi. Ubinafsi ni shetani anayekula ndoa nyingi. Ninashangaa kuona watu wanasema wamekuwa mwili …