Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hakuna Biashara Inayojiendesha Kwa Hasara

” ujinga ni kufanya kitu kwa mtindo ule ule huku ukitegemea kupata matokeo tofauti.” Usifanye kwa mazoea, fanya kwa kusudi. Jipime kwenye kila unalofanya je,kuna faida unayopata au hasara? Ukiona ni hasara acha kwa sababu hakuna biashara inavyojiendesha kwa hasara bali faida. Mwl. Deogratius Kessy

Kuwa Mkali Kwa Mtu Huyu Hapa

Rafiki yangu, Yako mambo mengi tu unashindwa kuyatekeleza kwa sababu ya kukosa nidhamu binafsi. Umekosa kuwa na nidhamu binafsi ndiyo maana mambo mengi huyakamilishi. Wakati unapokuwa na njaa huwa hujali kitu kingine zaidi ya kupata chakula ili ushibe. Unatakiwa kuwa na nidhamu hiyo kwenye kile ulichojiwekea kufanya yaani hutulii mpaka upate kile unachotaka kwenye maisha …

Ukipata Nafasi Hii Itumie Vizuri

Kwa chochote kile ambacho unaweza kufanya sasa kifanye. Usipeleke mambo mbele kwa kuahirisha leo kwani ya mbele huyajui yatakuwaje. Punguza mambo mapema. Kwa chochote kile utakachoweza kufanya leo fanya wala usipeleke mambo mbele kwa sababu wakati ulionao sasa ndiyo wakati muhimu na wa uhakika. Vile ambavyo unaweza kuvikamilisha leo au sasa vikamilishe.Kila siku tembea na …

Hii Ndiyo Njia Nzuri Ya Kuhubiri Injili

Siku moja Mt Fransisco wa Assis alimwambia ndugu twende tukahubiri ijili. Walitembea mpaka vijini sasa yule ndugu aliyekuwa naye akamwambia, mbona hatuhubiri injili tunapita tu? Fransisco akamjibu akamwambia ndugu kupita kwetu tu, tunahubiri injili. Rafiki, jinsi tu unavyovaa unahubiri injili ya Mungu. Je, unavaaje? Jinsi tu unavyoishi maisha yako unahubiri injili. Je, maisha yako unaishije? …

Huyu Hapa Anaona Juhudi Zako

Asili inaona juhudi zako. Na kawaida asili huwa haipendi deni la mtu. Inamlipa mtu kadiri ya thamani anayoitoa. Mungu anaona juhudi zako unazoweka katika kile unachofanya. Hivyo basi, hawezi kukuacha, endelea kumtegemea na kuweka kazi.Weka kazi na sala kwenye kile unachofanya na utafanikiwa ni suala la muda tu. Endelea kuweka bidii kwenye kile unachofanya kwa …

Hili Ndiyo Eneo Zuri La Kuwa Mbishi

Kwenye ubishi hakuna mtu ambaye anakubali kushindwa. Mtabishana lakini kila mtu atabaki kuwa katika kile anachoamini. Mabishano yako mengi, wako ambao wanabishania siasa, mpira wa miguu, na mengine ambayo sijayaorodhesha hapa. Unapobishana unakua unapoteza nguvu kubwa ambazo ungezielekeza kwenye uzalishaji ungekuwa mbali. Leo ninataka nikupe kazi ya kwenda kuwa mbishi kwenye eneo moja muhimu sana …

Jinsi Ya Kupata Kile Unachotaka Kwenye Maisha Yako

Mpendwa rafiki yangu, Ukitaka kushindwa katika maisha basi ishi bila kujua kile unachotaka. Kanuni moja ya mafanikio ni kwanza jua kile unachotaka. Ni nani kati yetu anaweza kwenda dukani kununua mahitaji halafu anafika pale hajui kile anachotaka? Hivi kama hujui kile unachotaka dunia itakusaidiaje? Kama huulizi utajibiwaje? Kama huna unachoomba utapewa nini sasa? Kama hujui …

Hiki Ndiyo Chanzo Cha Kutokuwa Na Matokeo Mazuri Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako

Mpendwa rafiki yangu, Kama bado hujapata kile unachotaka kuna chanzo kimoja ambacho ndiyo ninakwenda kukuelezea hapa kwanini bado hujakipata. Sisi binadamu ni wazuri sana kwenye kupanga lakini kuchukua hatua ndiyo kuna shida kubwa, kama ingekuwa tunakuwa vile tunavyotaka kwa njia ya mdomo tu basi kila mtu angekuwa tajiri kwenye kila eneo analotaka kwenye maisha yake. …

Hii Ndiyo Asili Ya Tabia Zote Unazojua

Mpendwa rafiki yangu, Hakuna mtu anaamka anajikuta anadaiwa milioni kumi. Mwanzo wa kitu chochote ulianza kidogo kidogo. Hakuna mtu aliyezaliwa na tabia fulani ila tabia zote tulizonazo tumezitengeneza sisi wenyewe. Asili ya tabia zote tunazojua ni matokeo ya kuanza kufanya kidogo kidogo na matokeo yake kuja kuwa tabia ya kudumu. Waulize watu wote walioingia kwenye …

Ushuhuda Wa Miaka Mitatu Ya Kuandika Kila Siku Na Mambo Matano Ya Kujifunza

Mpendwa rafiki yangu, Safari yangu ya kuandika kila siku kupitia mtandao wa Kessy Deo ilianzia tarehe moja octoba mwaka 2016. Hivyo basi, leo hii namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuandika kila siku bila kuacha tokea mwaka 2016. Kuandika kila siku ni kazi, lije jua au mvua ,kuwepo na changamoto au la lazima makala iende hewani.  Leo …