Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usiridhike Na Mafanikio Haya Hapa

Ni kawaida watu wakifanikiwa kidogo, mafanikio madogo huwa ni kikwazo kwao. Kamwe usiridhike na kupata mafanikio kidogo, badala unapaswa kujiweka kwenye hatari mara zote. Watu waliofanikiwa kidogo, wanakuwa wanaridhika mapema na mafanikio waliyopata na kuendelea kuyalinda. Badala ya kukazana wafanikiwe zaidi, wao wanakazana kuyalinda zaidi. Kwa mfano, timu ya mpira inapopata goli moja na kuendelea …

Chochote Unachokisema Vibaya Kinakukimbia

Ukiisema fedha vibaya, itakukimbia. Na mara nyingi, watu wasiokuwa na fedha, ndiyo wanaongoza kwa kusema vibaya kuhusu fedha. Iko hivi hivi, chochote ambacho unakisema vibaya kinakukimbia, pata picha umeshavisema vibaya vitu vingapi? Kama ulishawahi kuisema fedha na matajiri vibaya ilishawahi kukusaidia kupata fedha zaidi? Badala yake? Inakufanya uzikose zaidi. Watu wasiokuwa na fedha ndiyo wanaongoza …

Kimbia Haraka Sana Ukisikia Neno Hili

Viashiria vya utapeli viko vingi, na watu wengi wanatapeliwa sana. Utajisikiaje kama leo ukijua kiashiria kimoja cha utapeli? Ukisikia neno HAKUNA KUFANYA KAZI, kimbia haraka sana maana hapo kuna dalili za kupigwa. Ukisikia mtu anakuambia kwamba fursa fulani unapata mafanikio bila ya wewe kufanya kazi kabisa, mwambie asante sana kisha ondoka haraka sana na ikiwezekana …

Kama Unataka Kuacha Kitu, Acha Kwa Sababu Hii Hapa

Kifupi tu rafiki yangu, maisha ni maumivu, , kwa namna yoyote ile huwezi kukwepa maumivu kwenye hii dunia. Watu wengi wanapenda kupata vitu bila maumivu, mtu anataka maisha yake yabadilike bila kuweka kazi au juhudi yoyote ile. Wengi wanajiambia kabisa hawezi kujitesa, na ukishindwa kujitesa kwa sababu ya kupata kitu kizuri utakuja kupata maumivu ya …

Hakuna Njia Rahisi Ya Kupoteza Hela Kama Hii

Kuigiza una hela. Watu wengi wanaopoteza fedha sana ni wale wanaotaka kuonekana au kuigiza kama wana hela au kitu fulani. Kumbuka maisha ni maigizo , kadiri unavyoigiza una hela lazima kuna gharama utaingia ili uonekane una hela. Utaigiza uko na kitu fulani, utaigiza uko mazingira fulani ambayo unataka watu wengine wakuone kama vile una hela …

Kadiri Unavyoweka Juhudi Za Kuongeza Kipato, Kuwa Makini Na Matumizi Yako

Fedha ikiwepo huwa haikosi matumizi. Unapokuwa na fedha mara nyingi inatafuta matumizi na sasa usipokuwa makini utajikuta huna unachofanya. Lazima uwe mjanja, kwani kuna kawaida ya matumizi kuongezeka pale kipato chako kinapoongezeka. Ukitaka uione hela, ongeza kipato chako na punguza matumizi yasiyokuwa na ulazima. Usipokuwa makini na matumizi, utashangaa mwanzoni ulikuwa na kipato kidogo na …

Usiende Mahali Ukiwa Fedha Hii Tu

Kwenye maisha lolote linaweza kutokea. Na maisha ni safari huwezi kujua nini kitatokea katika ya safari. Hivyo basi, unapoishi lazima uishi kwa tahadhari kwamba ujiandae kukabiliana na lolote lile litakalojitokeza. Kwenye fedha, ninao ushauri mzuri ambao napenda kukuambia leo rafiki yangu. Ushauri huu nilijifunza kutoka kwa mwandishi Grant Cardone ambaye ni mwandishi wa mambo ya …

Jinsi Ya Kutengeneza Deni Ili Ulipwe

Kwenye maisha lazima utengeneze madeni mengi kwa watu wengine ili ulipwe. Unatengenezaje sasa madeni hayo? Ni kwa njia ya utoaji. Utoaji huwa unatengeneza deni ambapo upande uliopokea huwa unasukumwa kulilipa kwa namna yoyote ile. Kwa mfano, mtu akikusaidia kitu, utatafuta namna yoyote ile ya kurudisha fadhila kwa sababu amekusaidia. Ndivyo binadamu walivyo, ukimpa kitu anatafuta …

Kitu Pekee Ambacho Huwezi Kukopa Hapa Duniani

Tumeshazoea kukopa, wengine kukopa imeshakuwa ni tabia, mtu asipokopa anakuwa anajiona kama vile hajakamilika. Pale mtu anapokuwa hana fedha anaweza kukosa kwa mtu wake wa karibu na akamsaidia lakini kuna kitu ambacho wote hapa duniani hatuwezi kukopa. Kitu chenyewe ambacho hatuwezi kukopa ni muda.Huwezi kukopa masaa 24 yajayo uyatumie kwa mambo yako leo na utakuja …

Faida Ya Juhudi Unazoendelea Kuweka

Kiasili juhudi yoyote unayoweka, huwa haipotei bure. Kila juhudi unayoweka kwenye eneo lolote lile la maisha yako litazaa matunda mazuri. Ukiweka juhudi kwenye kuongeza kipato chako zaidi, utapata matokeo mazuri unayotaka kuyaona. Hata kama kwa sasa huyaoni yatakuja kukulipa baadaye. Jipatie nakala yako leo kwa bei ya ofa shilingi elfu 5 tu, 0717101505/0767101504 piga namha …