Design a site like this with WordPress.com
Get started

Una Uhakika Wa Kufanikiwa

Sina uhakika kama itakufaa lakini ukichagua kitu kimoja au vichache ambavyo utavifanya kwa maisha yako yote, ukawa unajifunza kila siku na kuchukua hatua, halafu ukaachana na mengine yote wanayofanya wengine,Una Uhakika Wa Kufanikiwa. Watu wengi hawajatulia kwenye kitu kimoja, wamekuwa wanahangaika na kila jambo linalokuja mbele yao. Na mwisho wa siku wanakuwa wamechoka kweli lakini …

Hiki Ndicho Kitakachopima Mafanikio Yako

Katika msingi wa falsafa ya ustoa unaamini kwamba dunia iko hivyo ilivyo yaani hakuna kitu kizuri wala kibaya na hakuna kitu kirahisi wala kigumu. Hapa tunajifunza kuwa, mtazamo wako ndiyo chaguo lako. Je, una mtazamo gani chanya kuhusu kufanikiwa kwenye maisha yako? Kwa mfano, wako ambao wanasema somo la hisabati ni gumu na wako ambao …

Rasilimali Yenye Uhaba Kwa Kila Mtu

Rasilimali yenye uhaba kwa kila mtu ni fedha. Kila mtu ana uhaba wa fedha hilo halina ubishi, ndiyo maana kila siku mtu anajituma ili kuendelea kupata fedha zaidi. Ingekuwa haina uhaba basi watu wasingefanya kazi kwa sababu inapatikana kirahisi. Angalia muda, ni rasilimali ambayo inaleta kila kitu kwenye maisha lakini haina uhaba watu wanatumia muda …

Mbinu Ya Kutokujiumiza Pale Unapopoteza Fedha

Pata picha inavyokuuma pale unapopoteza fedha, utajisikiaje? Kila mmoja wetu kuna maumivu ambayo anayapata pale anapopoteza fedha zake. Iko mbinu ambayo inaweza kukusaidia kutokuumia pale unapopoteza fedha. Ukipoteza fedha chukulia kama umetoa sadaka au umemmsaidia mtu asiyejiweza kwa kufanya hilo litakuzuia usiumizwe na kupotea kwa fedha. Bila kufanya hivyo, utajikuta unajiumiza kila wakati. Hatua ya …

Msingi Wa Kupata Fedha Zaidi

Msingi ni huu; kila unapokuwa unahitaji fedha zaidi, jiulize swali hili, ni mtu gani naweza kumsaidia apate fedha zaidi? Ukipata jibu, hapo ndipo mahali unapoweza kupata fedha zaidi. Utaweza kupata fedha zaidi pale tu utakapomwezesha mtu mwingine kupata fedha zaidi. Makosa makubwa ambayo watu wengi huwa wanayafanya kwenye kutaka kupata fedha zaidi ni kuangalia ni …

Asante Ya Mtu Huyu Inapaa Mbinguni

Huwa tunafikiri kutafuta ufalme wa Mungu ni kusali na kuhudhuria kwenye nyumba za ibada mara nyingi. Sina uhakika kama itakufaa lakini kutafuta ufalme wa Mungu ni pamoja na kusaidia watu wake. Hata yule anayesali sana hajawahi kumuona Mungu kwa macho, ni katika kusaidia watu wake ndiyo tunamuona Mungu kwa macho. Unaposaidia watu kupitia kile unachofanya, …

Jilazimishe Kuishiwa Kiakili Kwenye Eneo La Fedha

Kutoka kwenye kitabu cha Tano za Majuma Ya Mwaka, kilichoandikwa na Kocha Dr Makirita Amani, kuna dhana ambayo nilijifunza katika eneo la fedha, nimeona ni vema na wewe nikushirikishe. Karibu sana rafiki yangu, “Kilio cha wengi kwenye fedha ni kwamba, watu wakipata fedha haikai na hata wakiweka akiba, haikai. Yaani wakipata fedha au wakiwa na …

Jinsi Ya Kujua Kama Unaenda Mbele Au Unarudi Nyuma Kiuchumi

Siku moja nilikuwa nasafiri kuelekea Dodoma kwenye semina, nikakutana na rafiki kwenye gari. Alinieleza ni kwa jinsi gani amekuwa hana nidhamu ya fedha, hajui afya ya kipato chake. Siyo yeye tu, wako wengi ambao hawajijui kama wanaenda mbele kiuchumi au wanarudi nyuma kiuchumi. Nilimuuliza rafiki niliyekutana naye kwenye gari, je, unaweza kuniambia matumizi yako ya …

Kiwango Cha Fedha Kinachowatesa Watu Wengi

Kadiri ya Grant Cardone kuna aina tatu za fedha lakini mimi leo niko hapa kukuambia kiwango kinachowatesa watu wengi na kushindwa kusonga mbele kwenye eneo la fedha. Aina ya kwanza ya kiwango hiko cha fedha kinachowatesa watu ni kiwango cha hofu. Kiwango cha hofu katika fedha kikoje kwani? Kiwango cha hofu hiki ni kiwango cha …

Usichukie Mafanikio Ya Wengine

Ukiona mtu anachukia mafanikio ya wengine jua kabisa hajui maana ya mafanikio kwake ni nini. Mafanikio kwako yana maana gani?Ukishajua mafanikio kwako yana maana gani huwezi kuchukia mafanikio ya watu wengine. Mafanikio yana maana tofauti tofauti kwa kila mmoja wetu. Kwa kulijua hilo usichukie mafanikio ya watu wengine bali yapende. Hakuna kitu kinawazuia watu kufanikiwa …