Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jilazimishe Kuishiwa Kiakili Kwenye Eneo La Fedha

Kutoka kwenye kitabu cha Tano za Majuma Ya Mwaka, kilichoandikwa na Kocha Dr Makirita Amani, kuna dhana ambayo nilijifunza katika eneo la fedha, nimeona ni vema na wewe nikushirikishe. Karibu sana rafiki yangu, “Kilio cha wengi kwenye fedha ni kwamba, watu wakipata fedha haikai na hata wakiweka akiba, haikai. Yaani wakipata fedha au wakiwa na …

Jinsi Ya Kujua Kama Unaenda Mbele Au Unarudi Nyuma Kiuchumi

Siku moja nilikuwa nasafiri kuelekea Dodoma kwenye semina, nikakutana na rafiki kwenye gari. Alinieleza ni kwa jinsi gani amekuwa hana nidhamu ya fedha, hajui afya ya kipato chake. Siyo yeye tu, wako wengi ambao hawajijui kama wanaenda mbele kiuchumi au wanarudi nyuma kiuchumi. Nilimuuliza rafiki niliyekutana naye kwenye gari, je, unaweza kuniambia matumizi yako ya …

Kiwango Cha Fedha Kinachowatesa Watu Wengi

Kadiri ya Grant Cardone kuna aina tatu za fedha lakini mimi leo niko hapa kukuambia kiwango kinachowatesa watu wengi na kushindwa kusonga mbele kwenye eneo la fedha. Aina ya kwanza ya kiwango hiko cha fedha kinachowatesa watu ni kiwango cha hofu. Kiwango cha hofu katika fedha kikoje kwani? Kiwango cha hofu hiki ni kiwango cha …

Usichukie Mafanikio Ya Wengine

Ukiona mtu anachukia mafanikio ya wengine jua kabisa hajui maana ya mafanikio kwake ni nini. Mafanikio kwako yana maana gani?Ukishajua mafanikio kwako yana maana gani huwezi kuchukia mafanikio ya watu wengine. Mafanikio yana maana tofauti tofauti kwa kila mmoja wetu. Kwa kulijua hilo usichukie mafanikio ya watu wengine bali yapende. Hakuna kitu kinawazuia watu kufanikiwa …

Usiridhike Na Mafanikio Haya Hapa

Ni kawaida watu wakifanikiwa kidogo, mafanikio madogo huwa ni kikwazo kwao. Kamwe usiridhike na kupata mafanikio kidogo, badala unapaswa kujiweka kwenye hatari mara zote. Watu waliofanikiwa kidogo, wanakuwa wanaridhika mapema na mafanikio waliyopata na kuendelea kuyalinda. Badala ya kukazana wafanikiwe zaidi, wao wanakazana kuyalinda zaidi. Kwa mfano, timu ya mpira inapopata goli moja na kuendelea …

Chochote Unachokisema Vibaya Kinakukimbia

Ukiisema fedha vibaya, itakukimbia. Na mara nyingi, watu wasiokuwa na fedha, ndiyo wanaongoza kwa kusema vibaya kuhusu fedha. Iko hivi hivi, chochote ambacho unakisema vibaya kinakukimbia, pata picha umeshavisema vibaya vitu vingapi? Kama ulishawahi kuisema fedha na matajiri vibaya ilishawahi kukusaidia kupata fedha zaidi? Badala yake? Inakufanya uzikose zaidi. Watu wasiokuwa na fedha ndiyo wanaongoza …

Kimbia Haraka Sana Ukisikia Neno Hili

Viashiria vya utapeli viko vingi, na watu wengi wanatapeliwa sana. Utajisikiaje kama leo ukijua kiashiria kimoja cha utapeli? Ukisikia neno HAKUNA KUFANYA KAZI, kimbia haraka sana maana hapo kuna dalili za kupigwa. Ukisikia mtu anakuambia kwamba fursa fulani unapata mafanikio bila ya wewe kufanya kazi kabisa, mwambie asante sana kisha ondoka haraka sana na ikiwezekana …

Kama Unataka Kuacha Kitu, Acha Kwa Sababu Hii Hapa

Kifupi tu rafiki yangu, maisha ni maumivu, , kwa namna yoyote ile huwezi kukwepa maumivu kwenye hii dunia. Watu wengi wanapenda kupata vitu bila maumivu, mtu anataka maisha yake yabadilike bila kuweka kazi au juhudi yoyote ile. Wengi wanajiambia kabisa hawezi kujitesa, na ukishindwa kujitesa kwa sababu ya kupata kitu kizuri utakuja kupata maumivu ya …

Hakuna Njia Rahisi Ya Kupoteza Hela Kama Hii

Kuigiza una hela. Watu wengi wanaopoteza fedha sana ni wale wanaotaka kuonekana au kuigiza kama wana hela au kitu fulani. Kumbuka maisha ni maigizo , kadiri unavyoigiza una hela lazima kuna gharama utaingia ili uonekane una hela. Utaigiza uko na kitu fulani, utaigiza uko mazingira fulani ambayo unataka watu wengine wakuone kama vile una hela …

Kadiri Unavyoweka Juhudi Za Kuongeza Kipato, Kuwa Makini Na Matumizi Yako

Fedha ikiwepo huwa haikosi matumizi. Unapokuwa na fedha mara nyingi inatafuta matumizi na sasa usipokuwa makini utajikuta huna unachofanya. Lazima uwe mjanja, kwani kuna kawaida ya matumizi kuongezeka pale kipato chako kinapoongezeka. Ukitaka uione hela, ongeza kipato chako na punguza matumizi yasiyokuwa na ulazima. Usipokuwa makini na matumizi, utashangaa mwanzoni ulikuwa na kipato kidogo na …