Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kuanza Siku  Yako Ukiwa Na  Fikra Nyingi Za Kifedha

Mpendwa rafiki yangu, Kila siku dunia inabadilika, hivyo usipokuwa ni mtu wa kubadilika na wewe lazima utaanguka vibaya. Uchumi unabadilika hata asili siku hizi ibadilika, watu waliokuwa wanategemea mvua ili wa lime lakini mwaka mambo yamekwenda tofauti. Kwahiyo, tuwe tunajiandaa na chochote kinaweza kutokea hakuna hali ya kudumu. Usiwe kama mti, kuwa mtu unayeweza kubadilika, …

Jiandae Kuwa Mbahili Katika Msimu Huu Wa Sikukuu

Rafiki yangu, Katika msimu wa sikukuu watu ndiyo wanaongoza sana kutumia hela, wako wanaoingiza sana na wako wanaotumia sana fedha. Huwa wengi wanaongozwa sana na hisia katika matumizi ya fedha. Usikubali kutumia hisia katika matumizi ya pesa katika msimu wa sikukuu. Ukiruhusu hisia zikutawale, utajikuta unanunua vitu ambavyo huna hata uhitaji nao, sijakuambia usinunue kitu …

Kwanini Umasikini Siyo Mpango Wa Mungu

Rafiki, Umasikini siyo haki yako ya kuzaliwa bali utajiri ndiyo haki yako ya kuzaliwa. Ni haki ya kila mmoja wetu kufanikiwa, kuwa tajiri. Kila mtu ana uwezo wa kuwa vile anavyotaka kuwa kadiri apendavyo yeye. Umasikini ni adui mkubwa sana wa binadamu, tunaalikwa kumpiga vita vikali, siyo rafiki mzuri kwani hatupatii kile tunachotaka. Lakini utajiri …

Eneo Muhimu Unalopaswa Kulidhibiti Katika Fedha

Fedha ni muhimu sana katika maisha yetu hilo halina ubishi. Watu wengi wamekuwa ni masikini wa fedha katika eneo la matumizi. Ukiangalia matumizi ya watu wengi unakuta matumizi yako juu ukilinganisha na kipato. Hii ni alama ya hatari sana. Kama mtu kipato chake ni 10 halafu matumizi yake ni 15 basi huyo yuko hatarini sana. …

Hiki  Ndiyo Kitu Kinachowaponza Watu Wengi Pale Wanapoahidi Kutoa Fedha

Mpendwa rafiki, Kutoa fedha kunauma sana, ni rahisi kuahidi ukiwa huna fedha lakini ukishaipata ugumu ndiyo unaanzia hapo. Mara nyingi watu huwa wanaahidi kutoa fedha kwa hisia, lakini katika utoaji mambo yanakuwa ni mengine. Unapokuwa katika hisia usiahidi kutoa fedha, hisia zitakuongoza utaahidi kiasi cha fedha ambacho huwezi kukitoa. Watu wengi wanapoalikwa katika mambo ya …

Kitu Pekee Ambacho Huruhusiwi Kufanya Pale Unapopata Fedha

Mpendwa rafiki, Kila mmoja wetu kila siku anajituma kufanya kazi ili apate kipato kitakachomwezesha kuendesha maisha yake. Wote tunaamini kuwa fedha ndiyo inaendesha maisha yetu, karibu kila eneo la maisha yetu, fedha imetawala na huwezi kuikwepa kwa namna yoyote ile. Ni kweli miongoni mwa watu wengi vipato ni vidogo huku vipato hivyo vikiwa vidogo bado …

Tofauti Kuu Tatu Kati Ya Tajiri Na Masikini

Mpendwa rafiki yangu, Sidhani kama kuna mtu ambaye amekuja hapa duniani na kujiwekea ndoto ya kuwa masikini. Kila mmoja wetu anapenda maisha mazuri na vitu vizuri. Tunakuja kupata changamoto ya kuwa na maisha hayo tunayotaka pale katika utafuti wa kuwa na vile tunavyotaka. Wote tunajua kabisa ili tufanikiwe tunahitaji kufanya nini lakini njia ya kufanikiwa …

Hii Ndiyo Fedha Ambayo Huruhusiwi Kuitumia

Mpendwa rafiki yangu, Kila mwanadamu ambaye ana akili timamu hawezi kubisha kuwa fedha siyo muhimu kwenye maisha yake. Watu wengi wanafanya kazi lakini wamekuwa ni watu wa madeni makubwa.  Mtu anakuwa hana anachopata mwisho wa mwezi fedha yote inaenda kwenye madeni. Madeni ni mabaya yanawafanya watu kuwa watumwa. Fedha ambayo huruhusiwi kuitumia ni ile ambayo …

Heshima Mbili Muhimu Za Kujijengea Eneo La Kazi

Kila kazi ina taratibu zake lakini tukija kwenye matokeo pia kila kazi ina matokeo yake kadiri ya utendaji wake wa kazi. Kazi ndiyo rafiki yetu mzuri, Kwani anatupatia kile tunachotaka katika maisha yetu. Tukifanya kazi tunazalisha thamani na watu wanakwenda kutulipa kadiri ya thamani tunayoitoa eneo la kazi. Kazi ndiyo inatuletea heshima na utu wetu. …

Usitegemee Kufanikiwa Kwa Fedha Hii

Rafiki, Kazi ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu kipato. Na tukirudi katika msingi wa fedha tunaambiwa kuwa fedha ni zao la thamani hivyo kama huna unachotoa, basi ni wazi kwamba hutoweza kupata kitu. Kumbe basi, fedha ni kutoa na kupokea. Usitegemee utafanikiwa kifedha kwa njia ya dhuluma. Fedha ya dhuluma huwa haikai itaondoka kwako kama …