Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usitegemee Kufanikiwa Kwa Fedha Hii

Rafiki, Kazi ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu kipato. Na tukirudi katika msingi wa fedha tunaambiwa kuwa fedha ni zao la thamani hivyo kama huna unachotoa, basi ni wazi kwamba hutoweza kupata kitu. Kumbe basi, fedha ni kutoa na kupokea. Usitegemee utafanikiwa kifedha kwa njia ya dhuluma. Fedha ya dhuluma huwa haikai itaondoka kwako kama …

Hiki Ndiyo Kiwango Sahihi Cha Fedha Unachopaswa Kupata Kila Mwezi

Rafiki, Fedha ni muhimu katika maisha yetu hilo halina ubishi kabisa. Karibu kila kitu kinahitaji fedha ili mambo mengine yaende katika maisha yetu bila fedha mambo yanakuwa ni magumu lakini tukiwa na fedha mambo mengi yanawezekana. Kileambacho tunakipata kila mwisho wa mwezi, kila siku, wiki ambacho ni kipato tunachopata kutoka katika kazi au biashara. Ni …

Jijengee Tabia Hii Muhimu Katika Mambo Ya Fedha

Rafiki, Kila kitu katika maisha yetu ni tabia. Tabia tulizonazo leo tulizianzisha sisi wenyewe hivyo katika kila jambo huwa tuna vuna kile tulichopanda. Matokeo unayopata sasa hivi ni kutokana na kile ulichopanda. Hata katika mambo ya fedha tabia ulizonazo leo ni kutokana na tabia ulizojijengea huko nyuma. Unachotakiwa sasa ni kuvunja tabia zote hasi ambazo …

Sehemu Pekee Ambayo Unapaswa Kuweka Nguvu Zako Ili Upate Mafanikio

Rafiki, Kuna vitu viwili muda na nguvu. Unaweza ukawa mzee una muda wa kutosha lakini huna nguvu ya kufanya kazi. Hivyo basi, tunatakiwa kulinda sana nguvu zetu sasa, maisha yetu yawe bora tunatakiwa kutumia nguvu zetu vizuri na kuzielekeza sehemu sahihi na siyo vinginevyo. Huwa tunakosea kitu kimoja, watu wengi wanatumia nguvu kutafuta mali na …

Jambo Muhimu La Kufanya Katika Safari Ya Mafanikio Ili Ujisikie Raha

Mpendwa rafiki yangu, Kila siku tunafanya kazi, tunakusanya fedha, tunapiga hatua moja kwenda nyingine hata umri wetu tulionao unabadilika kila siku. Kumbe mafanikio tunayopata kila siku ni makubwa sana katika safari ya mafanikio. Kama leo uko mbele zaidi ya jana hayo nayo ni mafanikio. Nimeona watu wengi wamejikinai wao wenyewe dhidi ya maisha yao. Wanaona …

Hii Ndiyo Zawadi Ya Matatizo Unayotatua

Kama tunavyojua kuwa msingi wa fedha duniani ni kutoa thamani. Hivyo basi, Tusitegemee kupata fedha kama hakuna thamani yoyote tuliyopanga kuitoa. Kila mmoja wetu anamiliki kiwango cha fedha kadiri ya aina ya matatizo anayotatua kila siku. Kwa mfano, mwalimu anatatua tatizo la ujinga, askari anatatua tatizo la usalama. Je wewe unatatua tatizo gani ili uweze …

Punguza Matumizi Haya Ya Kifedha Ili Uweze Kufanikiwa Kiuchumi

Mpendwa rafiki yangu, Bado suala la nidhamu ya fedha imekuwa ni tatizo miongoni mwa watu wengi. Hata uwe mtu unayepata kipato kikubwa kiasi gani na ukawa unatumia zaidi ya kile unachopata bado wewe ni masikini mkubwa. Watu wamekuwa ni watu wa kutumia kile walichopata mpaka kiishe kwanza. Hakuna falsafa mbaya kwenye matumizi ya fedha kama …

Njia Bora Ya Kujiandaa Kifedha Ili Kukabiliana Na Matukio Na Sikukuu Za Mwisho Wa Mwaka

Mpendwa rafiki yangu, Dunia huwa inatupa kalenda ya matukio ya karibu mwaka mzima. Hapo ulipo tayari umeshakuwa na kalenda yako na unajua tukio fulani ni lini au siku gani. Hivyo, kama umeshakuwa na utambuzi huo unatakiwa sasa uchukua hatua ya kujiandaa kukabiliana na hayo. Mwezi unaongozwa kwa matumizi makubwa huwa ni mwezi wa mwisho wa …

Hili Ndiyo Eneo Lenye Utajiri,Fedha Na Mafanikio Makubwa

Rafiki, Kama umeamka na hujui nini unatakiwa kwenda kufanya rudi kitandani ukalale. Hivi mpaka leo hii kuna mtu bado hajajua kusudi la maisha yake? Kama bado hujajua kusudi la maisha yako basi nakusihii sana usome kitabu kinachoitwa ONGEA LUGHA YAKO, SAUTI YAKO YA NDANI NDIYO MAFANIKIO YAKO.  Hivyo kuwa huru kuwasiliana na mimi ili uweze …

Njia ya uhakika ya kupata mafanikio makubwa

Rafiki, Najua unahitaji mafanikio, ila siri ya mafanikio iko wazi kabisa ni kuwawezesha wengine kupata kile wanachotaka na wewe utapata kile unachotaka. Ila watu shida yao moja ni kwamba hawataki kujitoa kwa ajili ya wengine hawajui kuwasaidia wengine ndiyo wao kufanikiwa. Njia ya uhakika ya kupata mafanikio ni kuweka maslahi ya wengine mbele, toa thamani …