Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usisahau Kumkumbuka Mtu Huyu Muhimu Sana Kwako Kama Unafanya Kazi

Usisahau kujikumbuka wewe mwenyewe. Watu huwa wanafanya kazi na kuwakumbuka watu wengine na kisha kujisahau wao wenyewe. Kuwa na mfumo mzuri wa kutenga fungu la burudani. Hili linakuwa fungu la kujipongeza au kujizawadia kitu kutokana na kazi au mafanikio uliyopata kwenye maisha yako. Kumbuka wewe ndiyo unafanya kazi hivyo unatakiwa kujipenda na kujipongeza. Kwa nini …

Haijalishi Una Roho Nzuri Kiasi Gani

Leo tuambiane tu ukweli bila kuweka unafiki. Kuwa na roho nzuri bila kuwa na fedha roho yako nzuri itakuwa haina msaada kwa mtu ambaye ana shida ya fedha kwako. Haijalishi una roho nzuri kiasi gani kama huna fedha roho yako nzuri haitakuwa na msaada kwa wengine. Kwa mfano, watu wakiwa na njaa hawatashiba roho nzuri …

Usisahau Kufanya Kitu Hiki Ukipata Mshahara Wako

Msingi mkuu wa fedha ni kutoa thamani. Hivyo basi, ukitaka upate fedha zaidi toa thamani kubwa zaidi. Fedha unayopata kwenye mshahara wako ni mbegu. Hata siku moja sijawahi kumuona mkulima anayekula mbegu hata awe na njaa vipi. Hivyo basi, usisahau kuwekeza sehemu ya fedha unayopata kutoka kwenye kipato au mshahara wako katika uwekezaji. Na uwekezaji …

Jinsi Ulivyo Mbinafsi Na Mchoyo

Utaweza kukataa wewe siyo mbinafsi wala mchoyo lakini sio kweli. Leo ninakwenda kukuonesha kwa namna gani ulivyokuwa mchoyo na mbinafsi. Ili kujua kama wewe ni mbinafsi na mchoyo hebu angalia malengo yako uliyokuwa nayo kwenye maisha yako. Ukiwa na malengo ya kununua gari na kujenga nyumba inayokutosha wewe na familia yako tu wewe ni mchoyo. …

Hatua Mbili Za Kuchukua Pale Unapoona Fedha Uliyonayo Ni Ndogo Ama Unaona Haikitoshi

Mpendwa rafiki yangu, Changamoto kubwa ya watu wengi iko kwenye fedha, kitu kikubwa kinachosumbua watu ni kukosa elimu ya msingi wa fedha. Kabla hujamiliki kiwango kikubwa cha fedha kwanza unatakiwa ujifunze sana juu ya misingi na elimu ya fedha kiujumla wake. Usipojua misingi ya fedha utakua ni kama vile mtu anayepewa samaki badala ya kufundishwa …

Hii Ndiyo Sababu Inayowafanya Watu Wengi Kushindwa Kuweka Akiba

Mpendwa rafiki yangu, Watu wengi hawana utaratibu wa kuweka akiba kwenye maisha yao. Wanaishi ile dhana ya mkono kinywani yaani ukipata tumia na ukikosa jutia. Unakuta mtu akipata  fedha anasahau kama kuna kesho, anaishi falsafa kama ya mbwa ya kutumia alichopata chote na kesho itajijua yenyewe. Akiba ni moja ya ulinzi mkubwa sana kwenye maisha …

Hii Ndiyo Mbinu Bora Ya Kutumia Pale Unapoona Gharama Za Maisha Zinapanda

Mpendwa rafiki yangu, Kila mtu anajua kuwa gharama za maisha zinapanda, na maisha yetu hayawezi kwenda bila kuwa na fedha. Fedha ndiyo mfalme katika zama hizi anatusaidia kuendesha maisha yetu na kulipa bili mbalimbali. Ukiwa mzima unavuta pumzi bure, lakini ukiumwa na hewa ya oksijeni utalipia hospitali, hivyo kwa dunia ya sasa kila kitu kinahitaji …

Njia Bora Ya Kukomesha Umasikini Kwenye Maisha Yako

Sijui kama kuna mtu huwa anakaa chini na kuweka malengo ya kuwa masikini? Bali umasikini wa mtu huwa unakuja kwa kujitakia mwenyewe kwa kushindwa kuwajibika katika kazi. Hakuna njia nyingine bora ya kukomesha umasikini kwenye maisha yako kama ya kufanya kazi. Umasikini unaondolewa kwa kufanya kazi. Lakini kama umasikini unaondolewa kwa kufanya kazi kwanini watu …

Hiki Ndiyo Kitu Chenye Nguvu Sana Katika Karne Ya 21

Mpendwa rafiki yangu, Tukiachana na pumzi hii tunayovuta kila siku basi kipo kitu ambacho ni muhimu sana baada ya pumzi. Na kitu hicho siyo kingine bali ni fedha. Fedha  ina ngumu sana katika maisha yetu. Licha tu ya kuwa na nguvu bali fedha ni muhimu sana katika maisha yetu. Fedha inakubalika kwenye kila eneo la …