Design a site like this with WordPress.com
Get started

Haya Ndiyo Maisha Ambayo Hayana Maana Kuishi

Ni maisha ambayo hayatathiminiwi. Mwanafalsafa Socrates aliwahi kunukuliwa akisema, maisha ambayo hayatathiminiwi, hayana maana kuishi. Watu wengi hawajifanyii tathimini kwenye kile wanachofanya ndiyo maana hawaoni matokeo mazuri, hawajui kama wanaenda mbele au wanarudi nyuma. Fanyia tathmini kazi yako. Jiulize kazi unayofanya inakulipa? Na itakufikisha kweli kule unakotaka kufika?Kazi unayofanya inasaidia jamii au ina haribu maisha …

Ukishakuwa Na Sababu Hii, Hakuna Kitakachokushinda

Mwanafalsafa Friedrich Nietzsche aliwahi kunukuliwa akisema,Yeyote mwenye sababu ya kuishi, anaweza kupambana na chochote. Kumbe basi, ukishakuwa na sababu ya kuishi, hakuna kinachoweza kukushinda. Ukishajua kile unachotaka na ukiwa na kwanini kubwa ndani yako utaweza kupambana na chochote kile. Wakati mwingine unakutana na mateso kwenye safari ya mafanikio, ukiangalia mapito unayopitia kama huna kwanini kubwa …

Kazana Na Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Kazana na kile unachotaka. Yape talaka yale yote ambayo hayakupi kile unachotaka. Zama ndani kabisa kwenye kile unachotaka, fanya kwa ubora wa hali juu kuliko mtu mwingine yeyote yule. Iko hivi rafiki yangu, kwenye maisha, tunapata kile ambacho tunapigania. Mfano mzuri jiangalie wewe mwenyewe, unapata kile ambacho wewe mwenyewe unakipigania sana na unavikosa vile ambavyo …

Samaki Huwa Anaanza Kuozea Kichwani

Ukiona familia yako haiendi wewe kama baba au mama jua shida ndiyo iko kwako kwa sababu, samaki huwa anaanza kuozea kichwani. Samaki huwa anaanza kuozea kichwani hii maana yake nini? Tatizo huwa linaanza kwenye wale watu wenye mamlaka makubwa kwenye eneo husika. Biashara inaanza kufa kwa sababu mmliki tayari alishakufa, wewe kama ndiyo kichwa cha …

Ubaya Au Uzuri Wa Kitu Unatokana Na Kitu Hiki

Unatokana na tafsiri yako. Kiasi asili hakuna kitu kibaya wala kizuri. Ubaya au uzuri ni zile tafsiri ambazo sisi wenyewe tunazitoa juu ya kitu fulani. Vitu huwa vinatokea kwa namna vinavyotokea na uzuri au ubaya wa kitu ni tafsiri yako ndiyo inatoa. Kitu kinachowaumiza watu siyo kile kinachotokea ila jinsi watu wanavyotafsiri kile kinachotokea. Kwa …

Kuwa Na Viwango Vyako Kwenye Kila Eneo La Maisha

Kujilinganisha na wengine ni kitu kigumu kufanya. Badala ya kujilinganisha unapaswa kuwa na viwango vyako ili utembee navyo kwenye safari ya mafanikio. Haijalishi unafanya nini kwenye maisha, kuna mtu ambaye ni bora kuliko wewe, ukikazana ukawa na baiskeli, kuna mwenye pikipiki, ukiwa na pikipiki kuna wenye magari na ukiwa na gari kuna wenye ndege. Hivyo …

Kila Ulichonacho Unaweza Kukipoteza Muda Wowote

Kila ulichonacho umekopeshwa. Kama unavyojua kitu cha kukopeshwa lazima ukirudishe kwa wenyewe pale wanapokihitaji. Vitu vyote ulivyonavyo, kuanzia watu wako wa karibu, mali, kazi, biashara nk umepewa kwa muda, itafikia wakati utavirudisha yaani utavipoteza. Na unatakiwa ujiandae pale vinapoondoka vile ulivyonavyo visikuumize. Jiambie kwamba, muda wake wa kuvirudisha umefika kwani niliazimwa kutumia kwa muda tu. …

Usijilaumu Kama Ulifanya Hivi

Usipoielewa misingi ya dunia utapata shida sana. Huwa tunataka mambo yaende kama vile tunavyotaka sisi. Kifupi, dunia haiendi kadiri ya matakwa yetu. Bali,Dunia inajiendesha kwa misingi yake, inafanya inavyotaka na siyo vile tunavyotaka sisi. Maisha yetu sisi binadamu ni kama biashara. Kuna wakati unapata faida na kuna wakati unapata hasara. Kama unapata faida tu, jua …

Jiulize Swali Hili Kila Wakati

Tuko katika zama za mambo mengi ukilinganisha na muda tulionao. Usipokuwa na misingi sahihi inayokuongoza utajikuta una hangaika na kila kitu, kila kitu kinakuwa ni kipaumbele kwako. Hebu fikiria kwa jinsi mambo yalivyokuwa mengi, na muda ni mdogo kila kitu ukikifanya ni kipaumbele kwako utaweza kufanikisha hata kimoja? Lazima uchague machache na muhimu zaidi na …

Usipoteze Sifa Hizi Mbili Kama Unataka Kuwa Kiongozi Bora

Kiasili kila mtu ni kiongozi wa maisha yake mwenyewe. Hata kama unajihisi wewe siyo kiongozi, basi leo jiambie kuwa wewe ni kiongozi wa maisha yako mwenyewe na jukumu la maisha yako ni lako mwenyewe kwa sababu mkurugenzi mkuu wa maisha yako ni wewe mwenyewe. Hata kama hujawahi kupata cheo sehemu yoyote ile, leo ondoka na …