Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndicho Unachopaswa Kukilinda Kuliko Vitu Vingine Vyote

Mpaka hapo ulipo tayari kuna sifa ambazo umeshajijengea na unajivunia kuwa nazo kwako wewe mwenyewe na kwa watu wengine. Umetumia muda mrefu kujenga sifa na jina lako. Hivyo basi, unapaswa kulinda sifa ulizojijengea pia ili juhudi zako zisipotee bure. Usikubali kufanya jambo ambalo litakuja kuharibu sifa yako hata siku moja. Shabaha yangu kubwa leo ni …

Mabadiliko Yanaanzia Hapa

Katika familia, taasisi, kwenye biashara yako mabadiliko ya kweli kwenye jambo na eneo lolote lile huwa yanaanzia juu, yanaanzia kwenye uongozi na kisha yanasambaa kwa wengine. Samaki huwa anaanza kuozea kichwani, hii maana yake nini? Ukiona familia haiendi vizuri jua wazi wazazi ndiyo hawajasimama. Ukiona wafanyakazi wako wanaenda vizuri, jua uongozi wa juu UMESIMAMA. Wafanyakazi …

Hiki Ni Kitu Cha Uhakika Kwenye Maisha Yako

Sina uhakika kama itakufaa lakini leo nina habari njema kwako rafiki yangu nikupendaye. Moja kuwa tayari kupoteza kila kitu. Na uwe uhuru kupoteza kila kitu wala usitetereke kwa kwenye maisha kuwa huru ina maanisha kuishi utakavyo na kupata unachotaka. Mbili, chochote kile ulichonacho kwenye maisha yako utakipoteza huo ni uhakika wala halihitaji ubishi. Hiyo ni …

Usikadirie Chochote Kile

Usikadirie chochote kile, wewe weka juhudi kadiri uwezavyo lakini usilazimishe matokeo unayotaka wewe. Matokeo yako nje ya uwezo wako, lakini mchakato wa kitu chochote kile uko ndani ya uwezo wako. Usifanye kitu halafu ukakadiria matokeo maana matokeo yanaweza kukuumiza vibaya na ukachukia hata kuendelea na mchakato. Wewe weka juhudi kadiri unavyoweza lakini usilazimishe matokeo yawe …

Imani Ulizonazo Zinachangia Sana Wewe Kuwa Hivyo Ulivyo

Imani ulizonazo, zinachangia sana kwenye matatizo na changamoto unazokutana nazo. Na ubaya wa imani ni kwamba, mtu unaweza hata usijue kama ni imani iliyopo ndani yako hasa kama ni kitu ambacho umezoea kukifanya. Unahitaji kubadili imani yako juu yako mwenyewe na kile unachokutana nacho. Inawezekana kabisa imani uliyonayo ndiyo inakufanya uende mbele au urudi nyuma. …

Sheria Bora Zitakazo Kufanya Uwe Kiongozi Bora

Kabla hujasema wewe siyo kiongozi, jua kabisa makala hii inakuhusu wewe. Wewe ni kiongozi wa maisha yako binafsi, Ni kiongozi wa familia yako, Ni kiongozi wa biashara zako, Ni kiongozi kwenye eneo lako la kazi. Kifupi, wewe ni kiongozi na kuwa kiongozi siyo mpaka uwe kiongozi wa nchi. Katika kitabu jinsi ya kuendesha nchi kilichoandikwa …

Utajisikiaje Kama Watu Wakikukuta Unafanya Kitu Hiki Kabla Ya Kifo Chako

Pata picha unafanya kile unachofanya na hapo hapo unapoteza maisha yako yaani mwili na roho yako vinakuwa vimetengana. Je, utakua tayari watu washuhudie au wajue kile ulichokuwa unafanya na wakitangaze kwa watu? Kama unatumia muda vizuri katika kufanya mema na mambo sahihi utakua huru dunia kujua kile ulichokuwa unafanya kwa sababu ni kitu sahihi. Lakini, …

Kushindwa Kwenye Maisha Yako Kuna Anzia Hapa

Kushindwa kwenye maisha yako kuna anzia pale unapoipoteza siku yako moja. Kwa sababu, mafanikio ni mkusanyiko wa siku nyingi unazoishi kimafanikio kila siku. Jim Rhon anasema siku ni ghali sana na unapotumia siku moja maana yake umepunguza siku kwenye maisha yako. Maisha ndiyo haya haya, ukitumia muda wako vizuri inakuwa ni faida kwako na ukitumia …

Haimaanishi Kwamba Mambo Ni Magumu

Kwenye maisha, mambo kutokuwa rahisi kama unavyotaka wewe haimaanishi kwamba mambo ni magumu, bali ndivyo yalivyo. Kwa mfano, mtu asipopata mauzo yale aliyopanga basi anaahirisha na kusema mambo ni magumu kweli. Mambo yasipoenda vile unavyotaka wewe utaanza kulalamika na kuona kama una kisirani au huna bahati. Wewe siyo kiranja wa dunia wa kutaka mambo yaende …

Vitu Unavyopaswa Kuacha Mara Moja Kama Unataka Kuwa Na Furaha

Viko vitu vingi sana vinavyowafanya watu wasiwe na furaha, lakini mimi leo nitakushirikisha kitu kimoja tu. Kama unataka kuwa na furaha, acha kitu hiki.USIPOTEZE MUDA WAKO KWENYE VITU AMBAVYO HUWEZI KUVIDHIBITI Kwenye maisha tunayo makundi ya aina mbili. Moja, vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wako. Hivi ni vile vitu ambavyo unaweza kuvibadili kwa sababu …