Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kipi Bora Kati Ya Faida Na Mshahara?

Una mtazamo chanya kuhusu faida na mshahara? Kadiri ya mwanafalsafa Jim Rhon anasema faida ni bora kuliko mshahara. Kwa nini?Kwa sababu mshahara utakupa fedha ya kuendesha maisha pekee lakini faida itakupa mafanikio makubwa. Kama umeajiriwa basi hakikisha una biashara ya pembeni na usitegemee mshahara pekee yake. Kwa sababu hata mshahara uwe mkubwa kiasi gani, huwa …

Usiwe Na Mtazamo Huu Kuhusu Mteja Unayefanya Naye Biashara au Kazi

Ni imani yangu kwamba ,kila mtu anauza na kila mtu ana kitu anauza. Kama umeajiriwa basi unauza ujuzi na muda wako. Kwa namna yoyote ile kila mtu ana kitu anauza, bila kuuza maana yake hauna maisha. Na kazi ya mauzo ni kazi inayokuhusisha na watu kifupi unaweza kusema ni mteja. Usiwe na mtazamo hasi kuhusu …

Ukiwa Huna Kitu Hiki, Usifungue Biashara

Methali ya wachina inasema, kama huna tabasamu, usifungue biashara. Unapokuwa kwenye kile unachofanya kifanye huku ukiwa una tabasamu. Kwa kuvaa uso wa tabasamu utawavutia watu wengi lakini ukiwa na kisirani hutawavutia watu wengi. Hakuna mtu anayependa kusikia matatizo yako. Watu wanapenda kukuona ukiwa unafanya kazi au biashara kwa tabasamu au furaha. Watu tayari wana matatizo …

Jinsi Ya Kula Mema Ya Nchi

Kila mtu amepewa kibali cha kula mema ya nchi. Kila mtu amebarikiwa kwenye maisha yake. Unachopaswa kujua ni kwamba, baraka huwa haziji tu kwako bila kufanya kitu. Baraka huwa zinakuja kwako kwa kufanya kitu. Ukifanya kitu na utaona baraka zinakuja. Baraka haziji kwa kuweka mikono mifukoni, bali baraka zinakuja kwa kufanya kitu. Ili uweze kuchota …

Biashara Mpya Ambayo Haijawahi Kufanywa Na Mtu Yeyote Yule Na Ina Fursa Nyingi Kweli

Kifupi tu rafiki yangu, hakuna biashara mpya ambayo haijawahi kufanywa. Biashara ni zile zile lakini tatizo liko kwenye utoaji wa huduma. Unaweza ukafanya biashara yako kuwa mpya kwa kuifanya ya kipekee sana kuliko nyingine zote ambazo tayari zilikuwepo. Usipate shida kutafuta wazo la biashara, unachotakiwa kufanya angalia biashara ambazo ziko mtaani kwako au changamoto ambayo …

Vitu Viwili Vitakavyokufikisha Kwenye Utajiri

Natumaini kama unasoma hapa, huna lengo la kuwa masikini. Bali lengo lako kuu ni kuwa tajiri. Tunapaswa kuungana wote duniani kupambana na adui ambaye anatesa watu ambaye ni umasikini. Umasikini ni laana, tupambane usiku na mchana kumtokomeza adui huyu ambaye kwa sasa ameshaota mizizi. Na umasikini wa watu wengi hauko mfukoni bali uko kwenye akili. …

Kero Unayoipata Kwenye Biashara Ya Wengine

Itumie kero hiyo kuboresha biashara yako na kuwa bora. Huwa tunajifunza vitu vingi sana kwenye biashara za wenzetu pale tunapoenda kupata huduma fulani. Kuna wakati unakutana na vitu vizuri na unajiambia kabisa hiki nitaenda kukitumia kwenye kazi au biashara yangu. Na kuna wakati unaenda kupata huduma kwenye biashara nyingine unakutana na huduma mbovu kiasi kwamba …

Kwanini Ni Muhimu Kila Mfanyabiashara Kuijua Biashara Yake Kwa Undani?

Ni muhimu sana kila mfanyabiashara kuijua biashara kwa undani, Kwanini? Ili kuweza kumsaidia kufanya maamuzi sahihi kila wakati. Kuendesha biashara ni sayansi na sanaa. Na kwenye sayansi kuna vitu vina kanuni na kwenye sanaa hakuna kanuni ni kufanya maamuzi kulingana na hali jinsi inavyokwenda. Usipoijua vizuri biashara yako, ni rahisi sana kuipoteza. Ijue biashara yako …

Usikubali Kufanya Kitu Hiki

Rafiki yangu, Kwa chochote kile unachofanya,Usikubali kufanya kitu kitakachodumu kwa muda mfupi, kwa msimu, tu kisha kikapotea. Fanya kazi itakayodumu muda mrefu, itakayodumu vizazi na vizazi. Tengeneza kitu ambacho kitaishi kwa muda mrefu kuliko muda utakaoishi wewe.Na kwa kufanya hivyo, ndivyo dhana ya wewe kuishi milele. Leo hii tunatumia kazi za watu wengi ambao walishaondoka …

Maneno Ambayo Huruhusiwi Kumwambia Bosi Au Mteja Wako

Kama umeajiriwa basi kuna maneno hupaswi kumwambia mwajiri au bosi wako. Badala ya kusema siwezi au siyo jukumu langu sema tu nitafanya halafu jifunze namna gani utafanya. Au omba msaada wa namna ya kufanya lakini siyo kusema huwezi au siyo jukumu lako. Na kama umejiajiri au unafanya biashara jua kabisa bosi wako ndiyo mteja wako. …