Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndiyo Kinaweza Kukutofautisha Na Wengine Kwenye Biashara, Kazi Au Kile Unachofanya

Kinachoweza kukutofautisha na wengine wote ambao mnafanya biashara zinazofanana, kazi au huduma zinazoendana ni utoaji wa huduma bora sana kwa wateja. Kumbuka yoyote yule unayempatia huduma ni mteja wako. Jihoji tu, kuanzia kwenye biashara, kazi, mahusiano je, huduma ninayotoa hii kwa mteja wangu anaweza kuipata sehemu nyingine? Kama anaweza kuipata je, mimi natoaje huduma bora …

Unafikiri Ni Nini Kinakuzuia Usifanikiwe?

Watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba kinachowazuia kufanikiwa ni vile walivyo. Lakini, ukweli ni kwamba, kinachokuzuia wewe usifanikiwe ni kile ambacho unajaribu kukikimbia.Kile ambacho unafikiria siyo ndicho kinachochukua muda na nguvu zako nyingi na kukuzuia kufanikiwa. Unachotakiwa kufanya ni, kujijua wewe ni nani, na unataka nini, kisha ukafanya maamuzi sahihi ya kuendesha maisha yako kwa kufanyia …

Unaweza Kuwadanganya Mashabiki Lakini Siyo Watu Hawa

Biashara ni mchezo na wafanyakazi ndiyo wachezaji wenyewe. Na watu wa nje ni mashabiki tu. Sasa kama biashara ni mchezo, unaweza ukawadanganya mashabiki lakini huwezi Kuwadanganya wachezaji. Unaweza kuwadanganya mashabiki kuhusu mwenendo wa biashara yako, au familia yako, au kitu fulani kwa kuigiza kwamba mambo yanakwenda vizuri, lakini wale walio ndani wanajua kama mambo yanaenda …

Kosa Ambalo Wauzaji Wengi Huwa Wanalifanya Kwenye Biashara

Unaweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, kama utaweza kuuza zaidi. Ni kweli hilo halina ubishi, mauzo ndiyo kila kitu kwenye biashara na maisha kiujumla. Mauzo ndiyo moyo wa biashara, ambapo yanasukuma damu ya biashara ambayo ni fedha. Bila mauzo hakuna fedha kwenye biashara, na bila fedha hakuna biashara. Unaona hapo mauzo yalivyokuwa muhimu? …

Jinsi Ya Kuendelea Kuvuna Kwa Mteja Wako

Wale watu ambao wanategemea kupata huduma yako kupitia kazi au biashara yako ndiyo wateja wako. Hata kama wewe ni mzazi basi watoto ni wateja wako, unatakiwa kuwapa huduma bora ya malezi kuwahi kutokea duniani. Wewe kama ni mke au mume unatakiwa kutoa huduma bora kwa mteja wako ambaye ni mke au mume wako. Wewe kama …

Tahadhari; Ijue Sheria Ya Mafanikio Kabla Hujapata Anguko

Waandishi Al Ries na Jack Trout kwenye kitabu chao cha THE 22 IMMUTABLE LAWS OF MARKETING wanaelezea sheria za masoko ni namna gani watu wakishapata mafanikio makubwa wanajisahau na baadaye kupata anguko. Maisha ni mauzo yaani kifupi kila kitu kwenye maisha ni mauzo sasa ili uendelee kubaki kwenye mauzo mazuri unapaswa kuwa na masoko endelevu. …

Mbinu Bora Ya Kujiamini Na Kuaminika Na Wengine Kwenye Kile Unachofanya

Kama unataka kujiamini na kuaminika na wengine kwenye kile unachofanya, basi jua vizuri kile unachofanya na kuendelea kujifunza. Kwa mfano, Ijue biashara yako na endelea kujifunza kuhusu biashara yako. Ijue kazi yako na endelea kujifunza kuhusu kazi yako. Na kitu muhimu zaidi ni kwamba kujifunza hakuna mwisho. Hivyo basi endelea kujifunza kuhusu kile unachofanya na …

Njia Bora Ya Kutawala Soko Kwenye Biashara

Huwezi kuingia kwenye ushindani wa kutawala soko kama huna bidhaa bora. Kumbe basi, njia bora kabisa ya kutawala soko ni kuwa na bidhaa bora. Lakini pia, haitoshi kuwa na bidhaa bora pekee yake. Kama ingekuwa ni bidhaa bora peke yake basi watu wengi sana wangeuza. Ukishakuwa na bidhaa bora, unachotakiwa kufanya ni kupambana na vitu …

Vitu Viwili Pekee Muhimu Kwenye Biashara

Kuna vitu viwili muhimu kwenye biashara sina uhakika kama itakufaa lakini ukivijua vitakusaidia kufikia mafanikio makubwa kwenye biashara yako. Moja ni jinsi gani ya kupata wateja. Biashara yako haiwezi kupata wateja kama hujaifanyia masoko. Masoko ni kuifanya biashara yako ijulikane, kama hujawaambia watu unauza nini watu siyo malaika kuweza kubashiri kile unachouza. Pambana sana ili …

Juhudi Unazoendelea Kuweka Zitakufikisha Kweli Kule Unakotaka Kufika?

Kila siku unapaswa kujitathimini ili uweze kujijua kama unaenda mbele au unarudi nyuma.Kwenye maisha hakuna kusimama, ukiona huendi mbele, basi jua unarudi nyuma. Unapofanya tathimini inakusaidia kukupa mrejesho wa kile unachofanya. Hivi ukijitafakari, juhudi unazoweka kwenye kazi, biashara zitakufikisha kweli kwenye malengo yako? Unataka kuwa Bilionea, je, utafikia kweli ubilionea kwa kuhudumia wateja wale wale …