Design a site like this with WordPress.com
Get started

Njia Ya Kushawishi Watu Kukubaliana Na Wewe

Ukitaka watu wakubaliane na wewe usiwakosoe. Kisaikolojia mtu akiona umeshamkosoa huwa anatafuta namna ya kujilinda. Watu wanataka wafanye ambacho wao wanaona wameamua wao kufanya maamuzi na siyo kulazimishwa. Kwa mfano, mtu mmoja alikuwa ni kiongozi wa kiwanda fulani alikuwa anawalazimisha wafanyakazi wa kiwanda hicho kuvaa kofia.Alikuwa anatumia mamlaka yake kila anapokutana na mtu ambaye hajavaa …

Vita Viwili Unavyopambana Navyo Kwenye Jamii Yako

Mafanikio ni kazi kweli. Kwenye jamii yetu yule mtu ambaye ameaua kubadilika na kuishi misingi yake na kuachana na maisha ya mkumbo huwa anachukiwa sana. Jamii yetu huwa haipendi kumuona mtu anayekwenda hatua ya ziada. Waambie watu unataka kuajiriwa na kulipwa mshahara wa kawaida hawatakua na shida na wewe. Waambie watu unataka kuwa tajiri na …

Huwa Unapendelea Kuwekeza Eneo Gani Zaidi Kati Ya Haya?

Maisha ya binadamu yana utatu. Utatu huo ni mwili, akili na roho. Na kufanikiwa kwenye maisha ni lazima ufanikiwe kwenye maeneo hayo yote matatu, kimwili, kiroho na kiakili. Watu wengi huwa wanapendelea kuwekeza kwenye eneo moja zaidi ambalo ni eneo la mwili. Je, wewe mwenyewe unapendelea kuwekeza eneo gani zaidi? Maisha yako yanapaswa kuwa na …

Ukisikia Watu Wanasema Hivi Uje Hiyo Siyo Fursa Tena

Siyo mara yako ya kwanza kusikia neno fursa. Huenda ulishawahi kupigwa au kusikia mtu kapigwa kwenye fursa fulani. Hakuna zama ambazo watu wanakimbizana na fursa kama hizi. Tokea mwaka huu uanze mtu ameshakimbizana na fursa nyingi na ukimuuliza mafanikio aliyopata hakuna. Na kila siku hajatulia kwenye hizi fursa. Sababu ni nini? Ni kwa sababu ya …

Aibu Yako, Aibu Yake

Jambo lolote la aibu ukimfanyia mwenzako jua aibu hiyo ni ya wote. Aibu yake, aibu yako. Kwa mfano; mwanandoa ukifanya kitendo cha kumfedhehesha mke au mume wako utakuwa mmejitia aibu wote na kufedheshana. Kiasili sisi binadamu ni viumbe vya hisia. Ukimfanyia mwenzako ubaya ule ubaya utakurudia na yale majuto yatakutesa. Falsafa ya karma inasema, chochote …

Hii Ndiyo Nidhamu Ambayo Watu Wengi Hawana

Hakuna mtu ambaye anaweza kukaa chini na kuwa na ndoto ya kuwa mtu masikini. Hakuna. Kila mmoja wetu anatamani kuwa vizuri kwa namna yoyote ile. Wengi hutamani kuwa mtu fulani lakini changamoto kubwa iko kwenye mchakato wa kuishi kile wanachotamani kutoka kwa wengine. Mtu anaweza kutumia muda wake wote duniani kutamani kuwa na maisha mazuri …

Hii Ndiyo Maana Ya Bahati

Kila mtu ana bahati hapa duniani. Hata wewe una bahati kwa sababu bahati huwa zinatengenezwa. Hata nuksi nazo huwa zinatengenezwa. Ukisema huna bahati hilo ni chaguo lako mwenyewe. Kwenye maisha kila kitu unachagua wewe mwenyewe. Aliyekuwa maandishi na mwanafalsafa wa ustoa Lucius Annaeus Seneca aliwahi kunukuliwa akisema, bahati huwa inatokea pale maandalizi yanapokutana na fursa. …

Hii Ndiyo Njia Ambayo Watu Wengi Wanapenda Kujifunza

Waswahili wanasema majuto ni mjukuu. Watu ni wagumu kujifunza kwa njia rahisi na somo likawaingia. Ni mpaka mtu ajifunze kupitia maumivu ndiyo somo litaingia vizuri. Bila maumivu soko huwa haliingii vizuri. Kumbe basi, ni kawaida ya binadamu kupenda kujifunza kupitia maumivu. Kwa mfano, hata shuleni kitu ambacho umejifunza kwa njia ngumu na ya maumivu ni …

Hii Ndiyo Hofu Unayoweza Kuikwepa

Zeno mwanafalsafa wa kistoa aliwahi kunukuliwa akisema, siwezi kukwepa kifo bali; ninaweza kukwepa hofu ya kifo. Usipoteze muda wako kama utaweza kukwepa kifo. Hutaweza ila utaweza kukwepa hofu ya kifo. Hofu ya kifo inaua wengi kuliko hata kifo chenyewe. Wewe ishi maisha yako na kifo kitakukuta kwa namna kitakavyokukuta. Usiache kufanya mambo makubwa kwa kuhofia …