Design a site like this with WordPress.com
Get started

Tengeneza Anuani Yako

Watu wakitaja jina lako wanapata picha gani?Ukisikia majina ya wengine unapata picha gani kwenye maisha yako? Majina yetu yana nguvu sana. Majina yetu ndiyo anuani yetu. Hakuna ambaye anaweza kututengenezea majina yetu isipokuwa sisi wenyewe. Andika jina lako vizuri sana. Tengeneza anuani nzuri unayotaka na uamuzi ni wako wala si mtu mwingine. Anuani inayokutambulisha sasa …

Huyu Ndiye Mwajiri Mzuri Duniani

Kinachokufanya uende mbele au urudi nyuma ni kwenye kile unachofanya au unachoamini. Huenda kile unachofanya unakifanya vizuri sana ndiyo maana unasonga mbele au unakifanya vibaya ndiyo maana unarudi nyuma. Kinachowafanya watu wabaki kama walivyo au waendelee ni imani. Imani inawafanya watu waishi maisha bora kabisa au ya hovyo kabisa. Imani inaunganika na akili. Yaani kile …

Ushuhuda Wa Msomaji Kitabu Cha Ijue Njaa Ya Wanandoa-1

Mpendwa rafiki yangu, Kazi yangu leo ni kukupa ushuhuda kutoka kwa Msomaji wa Kitabu Cha Ijue Njaa Ya Wanandoa. Kama inavyojionesha hapo kwenye screenshot ndivyo inavyoonesha majadiliano yetu baada ya kukipata kitabu. Kitabu hiki kinapatikana kwa mfumo wa nakala ngumu. Bei ya kitabu hiki ni 15000 na haijalishi uko wapi tutakutumia kwa njia ya basi …

Jinsi Ya Kuwanasa Wateja Kwenye Biashara Yako

Biashara ni wateja. Kama hauna wateja maana yake biashara yako haina fedha. Na fedha kwenye biashara ni kama vile damu, pata picha mtu akikosa damu kwenye mwili wake nini kinatokea? Kumbe basi, biashara ikikosa wateja itakufa kabisa. Ni jukumu lako wewe kuhakikisha kila siku unafanya masoko. Masoko mazuri unayofanya lazima yatakuletea matokeo mazuri sana kwenye …

Kama Unataka Watu Wasikupuuze Fanya Hivi

Kuwa bora sana kwenye kile unachofanya kiasi kwamba hakuna anayeweza kukupuuza. Hii ndiyo sentensi ambayo ina nguvu kubwa sana. Ukitaka watu wakupuuze, usiwe bora sana kwenye kile unachofanya. Narudia tena, kuwa bora sana kwenye kile unachofanya kiasi kwamba hakuna anayeweza kukupuuza. Sasa jiulize wewe unaweka ubora kwenye kile unachofanya? Unafikiria kwa jinsi unavyofanya kazi watu …

Mpango Mzuri Wa Kufikia Fedha Nyingi Unazotaka

Kila mmoja wetu anajua kuwa fedha ni muhimu wala hilo halihitaji ubishi. Fedha ni jawabu la mambo yote. Matatizo mengi waliyokuwa nayo watu siyo matatizo bali hawana fedha. Kama tatizo linalokusumbua linatatulika na fedha basi wewe tatizo lako ni fedha. Tafuta fedha utatue matatizo yanayokukabili. Wale ambao wanawasema vibaya wenye fedha nyingi ni wale ambao …

Faida Namba Moja Ya Kujua Kitu

Kama unajua kitu vizuri utafanya kwa ubora. Matokeo anayozalisha mtu ndiyo kipimo cha ubora wake. Kama utazalisha kazi nzuri basi itapima ubora wako. Ndiyo maana unatakiwa kufanya kazi yoyote ile inayopita kwenye mikono yako kwa ubora wa hali ya juu. Ukifanya hovyo, watu watakuchukulia hivyo hivyo. Faida namba moja ya kujua kitu ni kufanya kwa …

Njia Nzuri Ya Kufuta Makosa Yako Pale Unapokuwa Umekosea

Hakuna mtu ambaye hakosei. Siyo tu kukosea hakuna mtu ambaye yuko sahihi asilimia 75. Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuwa sahihi mara zote. Hili linadhihirishwa na aliyekuwa raisi wa Marekeni Theodore Roosevelt aliwahi kunukuliwa akisema, kama angeweza kuwa sahihi asilimia 75 tu angeweza kufanya makubwa sana. Ukitaka watu wakuheshimu zaidi hata kama umefanya kosa ni …

Hiki Ndiyo Kitu Kitakachokusaidia Kwenye Maisha Yako

Ni ukweli. Ukweli siku zote utakusaidia kwenye maisha yako lakini siyo uongo. Watu wengi wanasema ukweli unaumiza lakini ukweli hauumizi bali unasaidia. Kinachowaumiza watu ni ujinga na siyo ukweli. Ukiwa na ujinga utakuumiza sana mpaka utaiona dunia siyo sehemu salama kuishi kwako. Mtu akikuambia ukweli mshukuru sana na wala usimnunie kwa sababu amekusaidia. Ondoa ile …

Haya Ndiyo Matokeo Ya Kukataa Kubadilika

Kwenye historia uingereza ni nchi ambayo ilikuwa na makoloni mengi kuliko mataifa mengine yenye nguvu duniani kwa wakati ule. Uingereza lilikuwa ni taifa lenye nguvu duniani mpaka kufikia karne ya 20 kwenye miaka ya 1945 walikuja kuanguka. Na sababu kubwa iliyowafanya kuanguka ni kutokubadilika yaani conservative. Tukiachana na utangulizi huo wa historia turudi sasa katika …