Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kuwa Mkali Kwa Mtu Huyu Hapa

Rafiki yangu, Yako mambo mengi tu unashindwa kuyatekeleza kwa sababu ya kukosa nidhamu binafsi. Umekosa kuwa na nidhamu binafsi ndiyo maana mambo mengi huyakamilishi. Wakati unapokuwa na njaa huwa hujali kitu kingine zaidi ya kupata chakula ili ushibe. Unatakiwa kuwa na nidhamu hiyo kwenye kile ulichojiwekea kufanya yaani hutulii mpaka upate kile unachotaka kwenye maisha …

Huna Mkataba Wa Kuishi Naye Milele

Vitu vyote ambavyo tunafanya hatuna uhakika navyo asilimia mia moja. Kitu ambacho kwa kila mmoja ana uhakika nacho asilimia mia moja ni kifo tu. Haya mambo mengine yote hatuna uhakika nayo kwa sababu ni vitu ambavyo viko nje ya uwezo wetu. Wazazi kuwapenda watoto wao ni kitu kizuri sana. Lakini, baadhi ya wazazi wanajisahau sana …

Kitu Ambacho Huwa Hakikosi Matumizi

Binadamu sisi ni watu wa kujisahau pale maisha yetu yanapobadilika. Ukiwa huna fedha utakuwa na mipango mizuri sana lakini fedha ikishapatikana mipango mizuri yote inapotea na inakuja kurudi pale ambapo huna kitu mfukoni. Rafiki, kitu ambacho huwa hakikosi matumizi kama ukiwa nacho ni fedha. Fedha ikiwepo tayari matumizi hujitokeza yenyewe. Unatakiwa kuwa makini na fedha …

Ukipata Nafasi Hii Itumie Vizuri

Kwa chochote kile ambacho unaweza kufanya sasa kifanye. Usipeleke mambo mbele kwa kuahirisha leo kwani ya mbele huyajui yatakuwaje. Punguza mambo mapema. Kwa chochote kile utakachoweza kufanya leo fanya wala usipeleke mambo mbele kwa sababu wakati ulionao sasa ndiyo wakati muhimu na wa uhakika. Vile ambavyo unaweza kuvikamilisha leo au sasa vikamilishe.Kila siku tembea na …

Hiki Ndiyo Kiunganishi Muhimu Cha Kukuwezesha Kupata Kile Unachotaka

Sisi binadamu ni viumbe vya hisia. Na karibu kila mmoja wetu ana husiana na wengine. Kitu kimoja kinachotuwezesha sisi kupata kile tunachotaka kutoka kwa wengine ni mawasiliano mazuri. Hakuna kitu ambacho unaweza kukipata bila kuwa na mawasiliano na wengine. Mawasiliano ndiyo kiunganishi muhimu kinachotuwezesha sisi kupata kile tunachotaka. Chochote unachotaka kutoka kwa wengine utakipata kwa …

Mambo Matatu Ya Kuepuka Kuyaanika Kwenye Mitandao Ya Kijamii

Unaruhusiwa kuanika vitu vyote lakini siyo hivi vitatu ninavyokwenda kukuambia leo. Moja ni hali yako ya afya. Watu hawapaswi kujua juu ya hali yako ya kiafya. Kwa sababu watu wakishajua uimara au udhaifu wako wa kiafya wataweza kutumia mtego huo kupata kile wanachotaka kutoka kwako. Masula ya afya yako binafsi ni siri na wala siyo …

Hii Ndiyo Sehemu Pekee Ya Kuanzia Kutengeneza Utajiri

Ukiwa unataka kwenda sehemu fulani huwezi kusema utaanzia wapi? Kwa mfano, uko nyumbani na unataka kwenda kazini huwezi kujiuliza hivi utaanzia wapi ili ufike eneo la kazi bali utaanzia hapo hapo nyumbani kutoka na hatimaye utafika kazini. Vile vile katika safari ya kuanza kutengeneza utajiri unaianzia hapo hapo ulipo. Anza na kile ulichonacho badala ya …

Watu Huwa Wanapenda Kujihusisha Na Watu Hawa

Iko wazi kuwa watu huwa wanapenda kujihusisha na watu wanaowajua. Ni ngumu sana watu kujihusisha na watu wasiowajua. Wewe hushangai ule usemi unaosema haijalishi unajua nini bali unamjua nani. Huu msemo huwa unasema kweli. Kama unataka kufanikiwa hakikisha unakuwa na watu. Kwani utajiri wako ni wastani wa watu unaojihusisha nao. Mafanikio unayotafuta yako tayari kwa …

Njia Mbili Za Kuepuka Kujivuruga Kwenye Maisha Yako

Maisha tayari ni magumu lakini watu tunayafanya maisha kuwa magumu zaidi kwa kulazimisha mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu. Siku moja nilikuwa nasoma kwenye mtandao wa kisima cha maarifa nikakutana na vitu viwili ambavyo huwa vinawavuruga watu. Kwa lugha rahisi msongo ni hali ya kuvurugwa. Sasa kuna vitu ambavyo huwa vinawafanya watu kuvurugwa zaidi. …

Hii Ndiyo Njia Nzuri Ya Kuhubiri Injili

Siku moja Mt Fransisco wa Assis alimwambia ndugu twende tukahubiri ijili. Walitembea mpaka vijini sasa yule ndugu aliyekuwa naye akamwambia, mbona hatuhubiri injili tunapita tu? Fransisco akamjibu akamwambia ndugu kupita kwetu tu, tunahubiri injili. Rafiki, jinsi tu unavyovaa unahubiri injili ya Mungu. Je, unavaaje? Jinsi tu unavyoishi maisha yako unahubiri injili. Je, maisha yako unaishije? …