Design a site like this with WordPress.com
Get started

Acha Jioni Yako Iwe Hivi

Usikubali kuanza siku yako kwa kisirani hata siku moja. Anza siku yako ukiwa na furaha yaani unapopata tu zawadi ya kuamka salama shukuru na jiambie kuwa leo ni siku bora na ya kipekee sana kwangu na nimechagua leo kuwa siku ya furaha kwangu. Kila kitu ni kuchagua kwenye maisha, je wewe umechagua kuianza siku yako …

Kauli Ya Kishujaa Unayopaswa Kujiambia Kila Siku

Kila siku unapoamka salama jiambie kila kitu kinawezekana.Mwanzoni ulikuwa unajiuliza utawezaje kuwa hivyo ulivyo leo lakini mbona leo umekuwa hivyo ulivyo leo? Kumbe kila kitu kinawezekana. Endelea kuwa na ndoto kubwa halafu kila siku jiambie inawezekana kuwa mtu fulani. Kwa mfano, jiambie inawezekana kuwa tajiri, yaani weka uwezekano kwenye kile unachotaka kufanya. Maisha yanakupa kile …

Haya Ndiyo Maisha Unayopaswa Kuishi

Ukiwa unatembea njiani ukikutana na ng’ombe mwenye rangi nyeupe, nyeusi hutoweza kushtuka kwa sababu unajua ni kitu cha kawaida tu ng’ombe kuwa na rangi tajwa hapo juu. Lakini;Ukikutana na ng’ombe mwenye rangi ya zambarau yaani purple cow lazima utashangaa kwa sababu siyo kitu cha kawaida ng’ombe kuwa na rangi ya zambarau. Lazima utaacha kile unachofanya …

Yaonee Huruma Maisha Yako

Maisha tayari ni magumu lakini watu wanayafanya kuwa magumu zaidi. Tafadhali, naomba uyaonee huruma maisha yako. Acha kuyafanya kuwa magumu zaidi. Kwenye kitabu cha Follow Your Heart mwandishi anasema kuwa, maisha yakiwa rahisi, huwa tunatafuta njia ya kuyafanya kuwa magumu zaidi. Na ukiliangalia hilo liko wazi. Mtu akiwa hana kipato kikubwa ataishi kwa nidhamu kubwa …

Huu Ndiyo Ujinga Ambao Wanandoa Wanapaswa Kuuacha Mara Moja

Ujinga ni nini? Ni kufanya kitu kile kile kwa mtindo ule ule halafu unategemea kupata matokeo tofauti hii ni kadiri ya mwanasayansi Albert Einstein aliwahi kunukuliwa akisema enzi za uhai wake. Huwezi kuwa na ndoa bora kama kila siku unafanya mambo yale yale yanayochangia ndoa yako kutokua vizuri. Ili mahusiano yako yaweze kukua inakupasa na …

Tafadhali, Usihangaike Na Watu Hawa

Usihangaike na wasioamini kile unachofanya. Wewe hangaika na wale ambao wanakuelewa. Maisha ni biashara, kumbuka siyo kila mtu atanunua kile unachouza, watu wanaouhuru wa kuamini na kutaka kununua kile wanachojisikia kununua. Hivyo usilazimishe kueleweka na wale ambao hawajui mchakato unaopitia. Wako watu ambao hawataamini kwenye kile unachofanya, na siyo kwa sababu ni wabaya au hawakupendi …

Ona Kama Vile Umepata Yote Kwa Bahati Tu

Kinachowaangusha watu chini ni kiburi walicho nacho. Watu wanaona vitu vyote walivyonavyo wamevipata kwa nguvu na ujanja wao wenyewe. Lakini hawajui hata vile tulivyopata ni kwa bahati tu. Isifikie mahali ukawa na kiburi kwa chochote kile ulichonacho. Ona kama vile umepata kwa bahati tu hata wengine nao wangestagili kupata ila bahati imekuangukia wewe. Ukiishi kwa …

Unapoingia Kwenye Biashara Angalia Kitu Hiki Kwanza

Watu wanapoingia kwenye biashara huwa wanafikiria kitu kimoja tu na kitu hicho ni kiasi gani cha fedha atapata. Lakini, nakushauri kitu rafiki yangu, usiangalie ni fedha kiasi gani utapata, bali pia angalia ni thamani gani unakwenda kuzalisha. Ukiangalia fedha tu, hutazipata. Lakini unapoangalia thamani, unapata fedha nyingi kadiri unavyozalisha thamani kubwa. Pale unapotaka fedha zaidi …

Hawa Ndiyo Watu Ambao Unapaswa Kutembea Nao Kwenye Safari Ya Mafanikio

Ni rahisi kuwaswaga kondoo na kwenda njia moja lakini ni ngumu kuwaswaga paka na kwenda pamoja. Kuwaongoza watu ni kama kuswaga paka kila mtu atakimbilia njia yake. Katika safari yako ya mafanikio hakikisha unakuwa na watu sahihi utakao fanya nao kazi. Chagua watu sahihi wa kufanya nao kazi kwenye kila eneo la maisha yako. Eneo …