Design a site like this with WordPress.com
Get started

Tafuta Mtu Wa Kukuwajibisha

Kwa sababu sisi binadamu ni wavivu kiasili. Usipokuwa na mtu anayekuwajibisha ni vigumu kuchukua hatua. Kama unaona nidhamu binafsi bado ni tatizo tafuta mtu ambaye atakuwajibisha yaani accountability partner. Mtu ambaye unamweshimu na wala hutoweza kumwangusha hata kidogo. Wakati mwingine unaweza kumpa kiasi fulani cha fedha kwamba akae na hizo fedha usipofanya kitu fulani basi …

Jinsi Ya Kujenga Nguvu Ya Ushindani

Kitu kikubwa cha kujifunza hapa ni kwamba kama huna kitu kinachokutofautisha na wengine, basi huna umuhimu. Huna nguvu ya ushindani na yeyote anaweza kukuangusha na ukaanguka.Mtu asiyekuwa na msimamo, chochote kinaweza kumwangusha. Nguvu ya ushindani inajengwa kwa kujitofautisha, kwa kufanya kile ambacho unaowalenga hawawezi kukipata mahali pengine isipokuwa kwako tu. Unapaswa kujiuliza unaweka juhudi eneo …

Huwezi Kueleweka Na Kila Mtu

Hakuna kazi ngumu sana duniani kama ya kutaka kueleweka na kila mtu. Ukichagua kutaka kueleweka na kila mtu maana yake umechagua kushindwa kabla hata hujaanza kazi. Watu hawajui unachojua, hawaamini unachoamini na hawataki unachotaka. Sentensi hiyo hapo juu isome mara mbili ili ujue watu walivyo badala ya kutaka kueleweka na kila mtu. Lakini, hilo halipaswi …

Usisubiri Mpaka Upate Kile Unachopenda

Iko falsafa ya mafanikio inayosema ukitaka kufanya fanya kile unachopenda. Ni kweli ila siyo watu wanao uwezo wa kuanza kufanya kile wanachopenda kwa sababu vingine vinahitaji mtaji lakini pia vingine hata vile unavyopenda kufanya haviwezi kulipa bili ya kuendesha maisha yako. Unachotakiwa kufanya, ni wewe kuanza kufanya chochote kile hata hukipendi ili kukusanya mtaji wa …

Popote Pale Unapokuwepo Unapaswa Kuwa Na Hiki

Haijalishi unafanya kazi ofisini, kiwandani, dukani au wito wowote ule uliochagua kuishi unahitaji kuwa na uvumilivu.Popote pale ulipo unapaswa kuwa na uvumilivu. Bila uvumilivu sijui kama kuna mtu angeweza kufanikiwa na kile ambacho anacho sasa. Karibu mafanikio yote uliyonayo umefanikiwa kwa sababu ulikuwa na uvumilivu. Kuanza na kumaliza kitu inahitaji ung’ang’anizi na uvumilivu ndiyo maana …

Kinachokufanya Usiende Mbele Ni Hiki Hapa

Hakuna kitu kingine zaidi ya kutochukua hatua. Hakuna mtu asiyejua ili afanikiwe anapaswa kufanya nini. Hakuna asiyejua ili afanikiwe kiroho, kiakili au kimwili anatakiwa kufanya nini. Watu wanajua kile wanachopaswa kufanya lakini shida iko kwenye kutokuchukua hatua. Wako watu wana kiri kabisa baada ya kuanza kuchukua hatua kwa nidhamu sasa wanaona mabadiliko chanya kwenye maisha …

Hakuna Mtu Anayependa Kukuona Wewe Ukipata Fedha

Iko wazi na siyo siri. Ukitaka ugomvi na watu ni pale wanapojua wewe unapata hela zaidi kuliko wao. Hakuna mtu anayependa kukuona wewe ukipata hela. Wako wachache sana watafurahia kukuona wewe ukipata hela nyingi lakini wengine utawakera na watakuchukia. Hakuna mtu anayependa kukuona wewe ukipata hela kwa mfano, ukiwa umeajiriwa na ukawa na miradi yako …

Tulia Kwenye Eneo Hili

Kama unataka kufikia kitu fulani kwenye maisha yako, iwe ni ndoto au lengo kubwa au kitu chochote kile unapaswa kutulia kwenye eneo la mchakato. Tulia kwenye mchakato na mafanikio yatakuja yenyewe. Kumbuka kuwa mchakato ndiyo zawadi. Ndiyo lengo la kufanya. Unafanya ili ufike kule unakotaka kufika. Mchakato ni kama mwendesha baiskeli, ili afike anapaswa kuendelea …

Huu Ndiyo Uhakika Wa Kufikia Ndoto Yako

Uhakika wa kufikia ndoto au lengo lolote ulilo nalo unakuja pale ambapo unakuwa unaifanyia kazi ndoto yako kila siku. Licha ya kuwa sisi binadamu hatuwezi kudhibiti matokeo yoyote yale, lakini tunaweza kupata matumaini ya uhakika kupitia mchakato au kazi tunayofanya kila siku. Kila siku ukijitahidi kuchukua hatua hata kama ni ndogo kiasi gani ni alama …

Mambo Ya Kuepuka Kukumbushiana Na Mwenza Wako Wa Ndoa

Hakuna mtu aliyekamilika kwenye kila eneo la maisha yake. Binadamu tuna asili ya udhaifu. Na kila mmoja wetu anakua kadiri ya mtazamo anaokutana nao kwenye jamii yake aliyokulia. Kawaida wanandoa wengi huwa wanaingia kwenye ndoa tayari wakiwa wakubwa hivyo kila mtu anakuwa na tabia zake. Na kazi inaanza pale wawili hao wanapoanza kuishi pamoja. Kwa …