Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Hamu Unayopaswa Kuwa Nayo Ili Kufikia Mafanikio Makubwa

Je, una hamu kiasi gani ya kufikia ndoto yako? Hamu kubwa  unayokuwa  nayo  kwenye  kitu  unachotaka  ndio  inapima  kama  utaweza kukipata. Kama  una  hamu  kubwa  sana  ya  kupata  kitu,  hakuna  kitu  kitakachoweza  kukuzuia kukipata.  Hata  utapokutana  na  changamoto  lazima  utapata  njia. Hamu kubwa  ya  kupata  kitu  inakupa  nguvu  ya  kulipa  gharama  ya  mafanikio. Unaweza  kujitengenezea  …

Unahitaji Fedha Zaidi

Matatizo mengi katika jamii yetu ukiyatazama mengi yanasababishwa na tatizo la fedha. Na matatizo mengi tuliyokuwa nayo siyo kwamba ni matatizo bali ni kukosa fedha ya kutatua matatizo tuliyonayo. Kama tatizo lako ulilokuwa nalo ukipata fedha linaisha basi hapo wewe huna tatizo bali tatizo lako ni fedha. Umasikini ni mbaya, pambana kufanya kazi ili kuondoa …

Vunja Utamaduni Wa Hovyo

Kwa utamaduni wa kiafrika ambao tunao, ni vigumu sana mtu kufanikiwa kwa sababu watu wengi wanafanya kazi kimazoea. Huwezi kufanikiwa kwenye kitu chochote kile kama hujaondoa utamaduni wa kiafrika ambao tunao. Utamaduni wa kiafrika hauchochei maendeleo bali unadumaza maendeleo. Pata picha kwenye jamii yako wewe unavyokuwa wa tofauti na jamii inavyokusema. Kwa mfano, jamii zetu …

Naomba Uniombee Ili Niache Hiki Hapa

Kiasili binadamu ni wavivu. Watu wengi wamekuwa hawataki kufanya kitu wanachopaswa kufanya kwa sababu ya uvivu uzembe na ujinga halafu wanaomba uwaombee ili wakae kwenye mchango. Mtu anakua anashindwa kutimiza wajibu wake anamsingizia shetani hivyo anaomba umuombee aache hiyo tabia. Yaani mambo binafsi ambayo yanahitaji nidhamu ya kuamua na kufanya mtu anataka aombewe. Tumpunguzie Mungu …

Kukubali Kwa Nje Tu

Watu huwa wanafanya kitu kama wamekubali wao wenyewe kutoka ndani ya mioyo yao. Unaweza ukawahamasisha kadiri uwezavyo na ukakubaliana nao kabisa kwamba watafanya lakini wanakuja kufanya kinyume. Ukiona mmekubaliana na mtu kufanya kitu halafu hafanyi jua alikukubalia kwa nje tu ili kukufurahisha kwa nje. Lakini ile ndiyo kutoka ndani yake haiko. Anaona ni bora akuridhishe …

Jinsi Ya Kujua Thamani Ya Utajiri Wako

Katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa ya ubilionea ni muhimu sana ujijue mpaka sasa una utajiri wa kiasi gani. Kuishi bila kujua una utajiri wa kiasi gani unakuwa kama vile mtu uko gizani. Umeshasikia tajiri fulani, utajiri wake ni kiasi gani, na wewe pia unapaswa kujua. Jinsi ya kujua utajiri wako halisi, CHUKUA THAMANI YA …

Ukiona Choo Kwenye Usingizi Usikitumie

Natumaini ilishawahi kukuta wakati uko mdogo, unaota unaona choo na ukikitumia tu unakuta tayari umeshajikojolea. Ukiona choo kwenye usingizi usikitumie, ina maana gani kwetu? Ukiona mambo ni rahisi sana shtuka.Ukiona mambo yanaenda vizuri kwenye biashara shtuka. Huenda unategwa hapo ili uingie kwenye mtego. Kama unafanya kitu na hakikusumbui, shtuka. Kama una ratiba ya siku ambayo …

Mauzo Hayaishii Pale Anaponunua Bali…

Maisha ni mauzo na yeyote anayeweza kuuza vizuri zaidi ndiye anayefanikiwa. Na utaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako kama utaweza kuuza zaidi. Tunauza muda wetu, utaalamu wetu, uzoefu wetu, huduma zetu na hata bidhaa mbalimbali. Pia tunauza mawazo yetu, ushawishi wetu na hata ndoto na maono makubwa tuliyonayo. Mauzo huwa hayaishii pale tu mteja  …

Tengeneza Fikra Hizi Kwenye Kila Kazi Na Biashara Unayofanya

Kuna watu wanaamini kwamba kuna kazi au biashara zinazolipa kuliko nyingine. Kila kazi au kwenye kila biashara kuna watu wengi tu wanaotengeneza fedha nyingi na wapo ambao hawatengenezi fedha kabisa. Je, unajua kwa nini ?Kwa sababu kinachowatofautisha wale wanaopata fedha na wale wanaokosa siyo kile wanachofanya bali ni namna wanavyofanya kile wanachofanya. Kama hupati matokeo …