Design a site like this with WordPress.com
Get started

Sala Dhidi Ya Kuwasema Wengine Vibaya

Usiwaongelee  wengine  vibaya, najua kuna watu wengine hawawezi kumaliza siku bila kuwasema WENGINE vibaya. Midomo yao iko kama vile bata ambaye hawezi kujizuia pale anapotaka kujisaidia. Nakusihi sana acha kusema watu vibaya, wewe siyo kiranja wa dunia ambaye unataka watu wawe kama vile unavyotaka wewe. Ukikosa mazuri kwa mtu ya kusema, basi kaa kimya na …

Ukitaka Kuoa Au Kuolewa Olewa Au Oa Mtu Huyu

Kwanza kabisa nikuambie tu kitu rafiki yangu nikupendaye, Huwezi kubadilisha asili ya mtu hata siku moja. Kama ulioa au kuolewa ukiwa na lengo la kutaka kumbadilisha mtu awe kama unavyotaka wewe hapo umejidanganya. Ukweli ni kwamba, ukitaka kuoa au kuolewa, oa au olewa na mtu ambaye hutaki kumbadilisha. Matatizo mengi kwenye mahusiano huwa yanayokea pale …

Watu Wanakupendea Vitu Hivi Viwili

Sisi binadamu tuna asili ya unafiki, huwa tupo kimaslahi zaidi. Tunaanzisha mahusiano na mtu fulani kwa sababu tunajua tutapata kitu fulani. Siyo watu wote wanaoanzisha mahusiano na wewe na unaona watu wanakupenda kweli, siyo kweli kwa sababu wengine wanakuja kwako kwa sababu ya maslahi kitu fulani na ataonesha anakupenda kwa sababu apate kile anachotaka. Watu …

Kila Kitu Kinategemea Hiki

Kadiri ya mwanafalsafa Seneca, mwanafalsafa wa falsafa ya ustoa anasema kwamba, kila kitu kinategemea maoni. Vile mtu alivyo ni jinsi anavyojiona yupo, maisha yako ni matokeo ya maoni uliyonayo juu yako. Una maoni gani juu yako? Kama una maoni chanya au hasi juu yako basi utakua kadiri ya maoni uliyonayo juu yako. Pata picha umevaa …

Fedha Hainunui Furaha, Je, Umasikini Unanunua nini?

Nilishajifunza sana na naendelea kujifunza zaidi juu ya misingi ya fedha. Kwa mtu ambaye hana hela huwa anaisema vibaya kwa sababu hana. HAKUNA mtu ambaye ana fedha halafu akaisema vibaya fedha. Naipenda fedha siyo kwa ubaya kwa sababu fedha ni jawabu la mambo yote. Tafuta fedha siyo kwa ubaya ila kwa uzuri. Ukishakuwa na fedha …

Kwenye Uhalisia Hiki Kitu Hakipo Kabisa

Watu wengi wanapenda kujiita watu fulani lakini hawapendi kuwa. Ni rahisi sana kujiita mwandishi, mjasiriamali, msanii na majina mengine unayoyajua. Ukiangalia kwenye mitandao ya kijamii, watu wengi wameandika kwambwa wao wamejiajiri au ni waandishi au wajasirimali. Lakini nikuambie kitu, hilo halina uhalisia. Ukitaka kujiita, mwandishi basi unapaswa kweli uwe unakaa kwenye mchakato na unaandika na …

Chochote Unachotaka Kufanya Kwa Namna Hii Kitakusumbua

Chochote unachotaka kufanya kwa urahisi kitakusumbua. Na chochote unachotaka kufanya kwa ugumu hakitakusumbua baadaye. Kwa mfano, unataka kufanya biashara kwa urahisi itakuja kukusumbua baadaye lakini, ukiifanya biashara kwa namna ugumu yaani unajitesa kwa hiyari kuhakikisha unajenga biashara na mifumo yake haitakusumbua baadaye lakini ukiendesha biashara kwa urahisi bila mifumo itakuja kukusumbua baadaye lakini mwanzo ukifanya …

Kuwa Mwendesha Farasi Usiwe Farasi

Watu wengi wanachagua kuendeshwa na farasi badala ya wao kumwendesha farasi. Unaweza kujiuliza je farasi na mwendesha farasi ni akina nani? Farasi ni hisia na mwendesha farasi ndiyo akili. Kumbe basi,  unatakiwa kuendeshwa na akili na siyo hisia. Hatua ya kuchukua leo; tumia akili na usikubali hisia ikuongoze. Kuwa mwendesha farasi na usiwe farasi. Usiendeshwe …

Kama Hasara Haikuhusu, Hupaswi Kunufaika Na Faida

Tumeshazoea kuona katika mahusiano na makubaliano mengi baina ya watu yapo kwenye hali kwamba inapopatikana faida basi pande zote zinanufaika na kufurahia. Lakini, inapopatikana hasara, upande mmoja unakuwa hauhusiki kabisa na hasara hiyo. Kama unanufaika na faida na hasara pia inakuhusu. Linapotokea jambo ambalo linaleta hasara unapaswa kuwajibika kama ulivyokuwa unawajibika kwenye faida. Unapaswa kujua …

Ukitaka Uhuru Mkubwa Unapaswa Kulipa Gharama Kubwa

Je, unataka uhuru? Rafiki yangu nikupendaye, kila aina ya uhuru unaotafuta kwenye maisha yako, ipo gharama ambayo utapaswa kulipa ili kupata uhuru huo. Kifupi tu, hakuna uhuru wa bure, na kadiri unavyotaka uhuru mkubwa , ndiyo unahitajika kulipa gharama kubwa. Uhuru ni kitu kigumu sana kukifikia na watu wengi hawaielewi dhana hii ya uhuru. Kwa …