Design a site like this with WordPress.com
Get started

Aina Mbili Za Ushindi Kwenye Mauzo

Mpendwa muuzaji,

Kila mtu ni muuzaji, iwe umejiajiri au umeajiriwa basi wewe ni muuzaji kwa sababu kupitia mauzo ndiyo yanafanya maisha yako yaweze kwenda.

Kwenye mauzo kuna ushindi wa aina mbili,

Moja, kuuza.
Kwenye kuuza hapa ni pale mteja anapotoa hela yake mfukoni na kununua kile unachouza.

Mbili, kuuziwa.

Kuuziwa ni pale mteja anapokupa sababu ya yeye kutonunua.
Mteja asiponunua kwako maana yake umeuziwa.

Na kwenye mchezo wa mauzo, kukamilisha mauzo ndiyo magoli yenyewe.

Kama ilivyo kwenye mpira wa miguu, kuna sare lakini kwenye mauzo hakuna sare wala kipindi cha pili.

Kama hujauza basi jua umeuziwa moja kwa moja.

Unatakiwa kupambana kuuza kile ulichoahidi kwa sababu kama una kitu kizuri ni wajibu wako wa kimaadili kabisa wewe kuuza.

Pata picha usipouza kile unachouza ni dhambi. Utakuja kuulizwa kwa nini ulikuwa na kitu kizuri ambacho kingewasaidia watu na hujakiuza?

Hatua ya kuchukua leo; Uza, Uza, Uza kwa sababu ni wajibu wako wa kimaadili kuuza.

Usikubali kuuziwa bali UZA.

Kumbuka, ni wajibu wako kama mtu wa mauzo kumsaidia mteja kufanya maamuzi. Hivyo, nenda leo kawasaidie wateja kufanya maamuzi ya kununua.

Wateja hawanunui kwa sababu kutoa hela kunauma hivyo ni wajibu wako kumpatia thamani kubwa kupitia kile unachouza ili aone thamani na asiumie.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: