Huwa tunadharau vile tulivyonavyo na kuthamini vile ambavyo hatuna.
Lakini, tunapaswa kuthamini vile tulivyonavyo kwanza kwa sababu ndiyo vitu muhimu kwetu ndiyo maana tukaanza kuwa navyo.
Kama ingekuwa siyo muhimu basi usingekuwa navyo.
Ulichonacho kinatosha kama ukifikiria vya kutosha. Fikiria una nini na je ulishafikiria vya kutosha juu ya kile ulichonacho?
Fikiria vya kutosha kwa kile ulichonacho na utaweza kuona fursa nzuri ya kuendelea kutumia kwenye maisha yako.
Thamini vile ulivyonavyo na vitumie vizuri.
Kila kitu kinawezekana kama ukikifanyia kazi.
Fikiria kupata zaidi kupitia kile ulichonacho, zalisha zaidi ili upate zaidi.
Ushindi wa kwanza kwenye maisha ni kutumia vizuri rasilimali ulizonazo.
Ukitumia vizuri kile ulichonacho kwa kufikiri vya kutosha utaweza kuwa na maisha mazuri unayotaka kuyaona.
Hatua ya kuchukua leo; kabla ya kulalamika umekosa nini, jiulize je, umetumia vizuri kile ulichoahidi?
Kumbuka, ulichonacho kinatosha kama ukifikiria vya kutosha. Fikiria vya kutosha na thamini kile ulichonacho.
Asili itakupa kile unachotaka kwenye maisha yako kama utakua ni mtu wa kutumia vizuri rasilimali ulizonazo.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog